Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini


Tutaanzisha christian green card ambayo itatumika kwa wakristo na tutalipa half price .halafu waislam watalipa full price .hakuna lisilowezekana.
 
Napenda kuwapongeza wanaharakati wa kiislam kwa kuibua madudu (njama) za serikali na kanisa ya kuwadhulumu na kuwabagua waliapa kodi wa kiislam wa taifa hili. Kwani wanaibua hoja zenye vielelezo ambazo zililifanywa kuwa siri. Hongereni na endeleeni kufanya upekuzi na bila shaka mtagundua mengine mengi.
 




Nitaisoma tena kwa makini. Ila pia niweke sawa kwamba niliandika neno "afya" katika aya ya pili ya post yangu kimakosa. Kusudio langu ilikuwa ni neno "elimu". Kwamba mapungufu katika MOU kwa mazingira tuliyonayo ni kipengele cha elimu ambacho kinapaswa kuondolewa ili ruzuku zipelekwe zaidi katika kuboresha shule za serikali hasa za kata. Kwa upande wa huduma za kiafya hoja yangu ilikuwa ni kupanua uwigo kutokana na uwepo wa taasisi nyingine zisizo za kidini zilizowekeza kwenya huduma za afya.

Ila maoni yako juu ya huduma za afya na elimu kutolewa kwa wafuasi wa dini husika ni makali sana naomba ushuke chini kidogo. Zingatia pia kwamba mawazo yanayotolewa na wachangiaji humu hayawezi kuchukuliwa kama yanawakilisha watu wote au wengi wa kundi fulani. Ulimwengu wa media siku zote huwa sio ulimwengu halisi.

Ukisema kwa sasa hospitali kama Bugando au KCMC itibu walutheri au wakatoriki peke yake utakuwa unatengeneza watanzania wa aina gani? Mjadala huu utakuwa unajenga au umebomoa? Mimi nilidhani tungeendelea kuutumia mjadala huu kwaajili ya kuelimishana na kupeana taarifa. Huwenda baadhi yetu tunakosa taarifa za kutosha ili kuhalalisha hoja zetu. Au wengine hatuna taarifa sahihi kuhusiana na mantiki ya suala zima. Kama tulio na taarifa za kutosha tutakuwa na hasira na kutoa masuluhisho ya mkato bila kujali matokeo yake hatutakuwa na tofauti na wasio na taarifa za kutosha au sahihi kuhusiana na suala hili. Na pengine mtu akawa na taarifa sahihi ila akakosa uhuru wa kuzijadili kwa uaminifu kutokana na ushabiki au upendeleo wa kidini. Ni bora tukaendelea kujadiliana kwa hoja na kwaajili ya kujenga hata kama baadhi ya hoja zinatukera.

Hata DR SLAA katika andiko lake ameanzia kwa kututanabaisha kutolijadili hili kwa ushabiki wa kidini. Hamna haja ya kuwa na asira sana pale unapoona hoja ya mtu imekwaza msimamo wako wa kidini, maana Mungu mwenyewe kama angekuwa na hasira kama zetu tungekuwepo?
 
Mkuu tunajua issue ni dini ndiyo maaana nilisema huko nyuma kwamba viongozi wao wanajua ukweli halisi ila wanawadanganya wafuasi wao kwa sababu wana agenda fulani.

Leo hii Kikwete alikuwa anafungua kitengo au tawi fulani la Hindu mandal hospital. Dr. Hussein Mwinyi waziri wa afya naye alikuwepo. Mwinyi kasema serikali ipo tayari kutoa ushirikiano na taasisi binafsi(bila shaka na za dini) kuboresha huduma za afya. Lakini ndugu zetu bado wanasema MoU ni ufisadi. Wengine baada ya kuambiwa ukweli sasa wanaanza kusema Dr. Slaa akiingia ikulu ataufuta Uislam.

Kama Dr. Slaa kwa kutoa tu maelezo yake anaonekana ataufuta Uislam. Hebu tuone mifano michache ya waislam halisi wanaosimamia kuufuta Uislam kwa kuusimamia, kuuendeleza na kuahidi kuendeleza huo ushirikiano wa Kanisa na Serikali unaofuta Uislam.

Hii tumeshaiona lakini si vibaya kuirudia.
Hapa kikwete anaahidi ushirikiano na taasisi ya kanisa tena anakwenda mbali zaidi na kuwaomba waende kusaidia wanawake wa vijijini...anaahidi ushirikiano wa miaka mingi ijayo. Sijui Uislam utakuwa umefutika??
Habari kamili gonga hapa chini:
http://www.dailynews.co.tz/index.php/local-news/6881-kikwete-pledges-support-to-holy-ghost-fathers

Hapa Kikwete anazindua mradi wa umeme wa Kanisa Katoliki. Anaahidi tena ushirikiano wa serikali na Kanisa
Habari kamili gonga hapa chini:
https://www.jamiiforums.com/busines...i-wa-umeme-uliojengwa-na-kanisa-katoliki.html

Hapa Kikwete anazindua mradi wa maji wa Kanisa. Nadhani hapa uislam utakuwa umetokomea kabisa.
Maisha kiasi

Kuna miradi mingine sijaiweka hapa.

Hivi hawa watu akina Basaleh , Ilunga, Mohamed Saidi na wengine wanaohubiri mfumo kristo kupitia hii MoU wanajiona ni waislam zaidi kupita Rais Kikwete na Dr Hussein Mwinyi wanaoahidi ushirikiano wa serikali na taasisi binafsi na za dini kuboresha mfumo wa afya nchini?
Yaani Rais Kikwete na Dr Hussein Mwinyi wanaoweza kuona nyaraka /mikataba yoyote ndani ya wizara ya afya washindwe kuona ufisadi wa MoU ila akina Basaleh ,Ilunga na Mohamed Saidi wanaoshinda wakipiga porojo kwenye mihadhara wajue kila kitu?

Naona wapinga MoU wanaanza kutoa hoja hafifu sasa maana ukweli unaanza kuwaingia taratiibu. MoU ambayo ni kama oxygen ya Mfumo Kristo inaanza kupungua. Dhana ya Mfumo Kristo ipo hatarini kutoweka. Watu hawana pa kushikia kujustify chuki zao kwa wakristo.
Sisi hatutachoka kuwaelewesha hata kama wana vichwa vigumu kama barubaru...
 

Na mimi huwa macho yangu yanauma nikifika mtaani kwangu na kuona kuna majengo yana alama ya mwezi na nyota. Huwa nadhulika kisaikolojia nikiwa kwenye gari lenye maandishi yanayoanzia kulia kwenda kushoto au nikiingia kwenye nyumba yenye hayo maandishi huwa nadhulika pia. Sasa sijui tufanyeje ili pasiwepo mtu anayedhulika kisaikolojia?
 
Ulishuhudia kwa kuona kwenye TV live?

Au ulikuwa karibu na tukio?

Umesema minara ilibomolewa? kwa ndege au mabomu?


Nilikuwa ng'ambo ya pili ya mkondo wa mwunganiko wa bahari ya Atlantic na mto Hudson unaotenganisha NY State na NJ State, hali kadhalika unaotenganisha jiji la NY na baadhi ya majiji ya NJ kama Jersey City, Union city, kwa ujumla ningesema Essex County, Union County, Passaic County kwa upande wa NJ ambazo hupakana na viunga vya jiji la NY.

Kwa taarifa yako wiki mbili tu kabla ya tukio nilikuwa mmojawapo wa visitors pale na kupanda mnara mmoja ambao visita walikuwa wanaruhusiwa na mnara mwingine visitors walikuwa hawaruhusiwi kupanda.

Siku ya tukio nilikuwa kibaruani kwa vile darasa lilikuwa kipindi cha alasiri. Jamaa alinishtua kwa kuniambia ndege imegonga mnara mmoja wa World Trade Center, kwa vile tulizoea kutaniana sikumtilia maanani, na mara bosi akaja kuniambia, she is serious, get out and see whats going on, the bulding burning totally, oh my God, full of smoke all over NY city. Niliacha keyboard na kutoka nione just a minute nilishuhudia dege likipita kwa kasi na kuishia kwenye mnara mwingine. Nilifikiria njia ipi itanifikisha Tanzania, maana hali ilishakuwa si ya kutumainisha tena Marekani. Nilikuwa si mbali sana na Lincolin Tunnel na daraja la George Washington likiwa tupu baada ya kufungwa magari kutopita hali kadhalika Lincolin Tunnel na Holland Tunnels hakuna kupita tunnels ambazo magari hupita chini ya mkondo wa bahari uliounganika na Hudson River.

Baada ya minara yote miwili kuanguka, masaa matatu baadaye nilipata akili kumtafuta mtanzania mwenzangu ambaye alikuwa anafanya kazi bank moja si mbali sana kutoka pale ni kama blocks nne hivi. Nilitulia alipoambia ameshavuta Hudson River na yuko tayari NJ salama. Jamani tusichezee amani, Tanzania hayajatupata tutajuta kuzaliwa. Watu walionekana na kila dalili ya kukata tamaa na kukosa matumaini na kuonyesha kila dalili ya kwamba kuna zaidi yanakuja.

Nimejaribu kukueleza kirefu kidogo nadhani utakuwa umenipatapata, hapa JF tuna wengi, usije fikiria watu tunapiga story za vijiweni, tunaandika mengi ya kushuhudia si kusimuliwa. Thanks for good understanding.
 
Last edited by a moderator:

Unajua pia kuwa mnara wa tatu pia ulianguka siku hiyo hiyo.

Huu hapa Three Towers Fell on 9/11... How Did the Third Tower Fall?! : Free Download & Streaming : Internet Archive

Lakini pia kuna hii thread hapa, kuna mambo/vitu havikubaliani na masimulizi ya tukio hilo. https://www.jamiiforums.com/international-forum/125362-ugaidi-wa-serikali-ya-marekani.html

Katika hili sitaendeleza mjadala, sitaki kuchafua mada husika.

Asante kwa maelezo yako, mkuu
 

World Trade Center ilikuwa ni jengo la minara miwii, si mitatu kama unavyosema wewe. Kama ni kuanga zaidi ya minara hiyo basi ni majengo yaliyokuwa kando yake ambayo hayakuwa marefu hata hayakufikia theluthi moja ya urefu wa WTC.

Sina nia ya kuendekeza hili, nimeandika tu kukujibu swali lako, maana ulionekana kutia shaka na kuniona niliona tu kwenye TV kumbe kwa aina fulani nilikuwa mwadhirika wa tukio lile ingawa sikuwapo ndani ya jiji la NY, lakini uwepo wa viunga vya jiji hilo kisaikolojia niliathirika.
 
Kwa hiyo tamko la Dr.Slaa haliwahusishi Wakristo wengine hivyo inabidi wajisemee wenyewe ni mashirika gani yanayowasaidia?
 
Kwa hiyo tamko la Dr.Slaa haliwahusishi Wakristo wengine hivyo inabidi wajisemee wenyewe ni mashirika gani yanayowasaidia?

hitimisho langu ni kuwa:

  • hakuna dini yoyote itakayoweza kutawala dunia yote yaan hakuna namna ambayo dini moja inaweza kuwa ndiyo dunia ya wakazi wote wa dunia, unless patokee mabadiliko makubwa-rapid radical changes, mfano kama maangamizi ya atomic bomb-ambayo yataleta mabadilko makubwa na ya ghafla yasiyoweza kuelezeka kwa namna ya kawaida kwa namna ambayo dunia na/au ulimwengu mzima itabidi vianze upya.


  • KATIKA HALI YA KAWAIDA, Mtu atapata kwa kadri ya kiwango chake cha kujituma. ikiwa unajituma kwa kiwango cha baiskeli basi utapata baiskel, ukijituma kwa kiwango cha pikipiki utapata pikipiki tu huwezi pata gari.


  • Historia, na aina ya elimu kwa ujumla, wanayofundishwa waafrika ina mapungufu makubwa sana kwa sababu haiwasidii waafrika kujitambua. kwa makadidrio yangu, 99.9% ya waafrika wasiosoma hawajitambui wakati wasomi ni kama 85% hawajitambui wao kama waafrika ni kina nani hasa. Kuna haja ya Historia na elimu kwa ujumla vipewe maono ya kiafrika(to be informed by african philosophy, values and believes) ili elimu iweze kumkomboa mwafrika ambaye bado amefungwa na minyororo mizito ya fikra mfu za kikoloni.

tchao kwa hili wana JF.
 

makubaliano yakihusisha mkataba wa maandishi mpaka hapo sio siri ni suala la wazi.

kuhusika kwa BAKWATA kwenye mazungumzo ya awali mpaka hapo sio siri .

kama kweli kuna fedha zinatoka serikalini kwa ajili hiyo bado hiyo sio siri (hazina sio ya kanisa).

ni mtazamo wangu tu.
 
Ipo siku watanzania tutaulizana ni dini ipi inalipa kodi nyingi serikalini? kisha tukatafuta usawa wa kulipa kodi? alisiyefanya kazi na asile!!!!!!!!! kila mtu apewe hudumu kulingana na mchango wa kodi kidini ili tu kuhalisha kubaguana.

mabishano ya kijinga yatatupeleka kuulizana mbona wasanii wa bongo movie wengi ni dini fulani? kuna upendeleo? kisha tutataka kuwepo na uwiano,

Timu ya taifa ya mpira tutasema kuna Tenga anapendelea dini yake. Kisha tutaomba nusu ya wachezaji waislamu na nusu wakristo.

Tunaelekea wapi?
 

Acha chuki na jazba amekwambia ukweli. Hivi suala ni mkataba au ni kushindwa kujenga? Kama suala ni mkataba, kwa nini Bakwata muliilazimisha ijiondoe kwenye MOU kwa madai kuwa haiwakilishi waislamu? Hivi ninyi mnashindwa nini kujenga hospitali na shule alafu mkawekeana mkataba na serikali wa kutotaifishwa au hata akili za kuweka mkataba hamnazo? Nakushauri uachane na mawazo finyu kama hayo; fanyeni kazi mjenge hospitali na shule za kutosha ili kuhudumia watanzania maana kama si mashirika ya dini ya kikristo serikali isingeweza kuokoa maisha ya watanzania ambao wangekufa bila kuwepo hospitali zao. Na kama suala ni ruzuku mkijenga hospitali kubwa zenye hadhi ya wilaya, mikoa au rufaa, hospitali hizo zitapewa ruzuku tu.
 
Kwa hiyo tamko la Dr.Slaa haliwahusishi Wakristo wengine hivyo inabidi wajisemee wenyewe ni mashirika gani yanayowasaidia?

Nadhani wewe sijui tukurudishe darasa la kwanza? Yaani kama umesoma vizuri maelezo ya Dr. Slaa na bado huelewi basi una uelewa hafifu sana. KWANZA maelezo ya Dr. Slaa ktk sehemu ya 7 yanasema hivi: ".....Ndipo tukaanzisha [yaani wakristo] mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani....". Hapo tu tayari anaeleza shirika la Kirutheri la ujerumani ambalo nalo ni moja ya wahisani. PILI anaeleza wao kama wakathoriki waliwakilishwa na TEC wakati wakristo wengine (yaani waprotestant) waliwakilishwa na CCT ambayo anaeleza ni muunganiko wa madhehebu ya Kikristo zaidi ya 60. Ktk maelezo ya Dr. Slaa sehemu ya 6 anasema "......Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania)....." Na kila dhehebu linapata misaada kutoka nje ktk mashirika ya dhehebu hilo. Ilikuwa hivyo na inaendelea kuwa hivyo. Haijawahi kutokea kwa mfano Mashirika ya Wasabato ya nje yakatoa misaada kwenye dhehebu la wakatholiki wa hapa. Au Mashirika ya Kikatholiki ya nje yakatoa misaada kwa Warutheri au Waanglikana wa hapa! Kwa hiyo ebu kuwa mwelewa si kulalama tu wakati hata maelezo ya Dr. Slaa hujayaelewa. Tatizo ni kama mna tatizo ktk kusoma mambo yaliyotolewa na wakristo. Badala ya kusoma vizuri mkaelewa mnajaa jazba na kutafuta pa kukosoa wakati hata hamjaelewa. Poleni sana. Ni vema hata waislamu wajifunze kwa Wakristo ili mashirika ya nje ya Kiislamu yatoe misaada kwa Waislamu wa hapa ili waweze kushiriki kikamilifu ktk kutoa huduma za kijamii ktk shule na hospitali. JK aliwaambia jengeni na nyie msikalie kulalamika tu! Malalamiko hayatawasaidia zaidi mtajenga chuki na uhasama usio na sababu za msingi matokeo yake nchi yetu mtaifanya iwake moto na kuuana kama ilivyo Nigeria na kwingineko kwenye vita ya kidini.
 
Na wewe hata sijui umesomea kitu gani cha kujitapa Mr know it all?

Suala si kuniuliza nimesoma nini cha msingi ni kuwa niliyoeleza kuhusu sheria na makubaliano yoyote ya kisheria ni kweli kama hujui uliza uambiwe. Ila kwa kukata kiu yako nina Msc. Chemical Engineering ya chuo kikuu cha Dar es Slaam.
 
shetani anapata ushindi wa kishindo anapoona Mungu anatuelekeza kumchukia yeye na matendo yake lakini binadamu tunachukiana sisi kwa sisi.

Kwa mustakabali huu, hakuna dini itakayomshinda shetani.

mwislamu angependa kumchukia mkristo kuliko shetani na mkristo angependa kumchukia mwislamu kuliko shetani............... dini iko wapi hapo.

dini zote zilikuja ili kumtokomeza shetani.
 

Mnabore kwa kulalamika nyie wakati wenzenu wanaenda shule mlikuwa wapi? Kila kitu kidogo mnlalamika mnaonewa shame on u
 

Nyumba nyingi za msajili wa majumba hazikuwa za taasisi zilikuwa za wahindi mmoja mmoja na wazungu na waswahili matajiri wachache.

Kwa asili wahindi ni waoga sana kukabiliana na serikali lakini ku-mobilize madai ya mtu mmoja mmoja ni ngumu sana lakini wapo waliorudishiwa nyumba zao baada ya kutaifishwa akiwemo mzee Oscar kambona watoto wake na mke wake Florah wamedai nyumba za baba yao ikiwemo ya mikocheni aliyokuwa anaishi mzee Rashid kawawa, Ghorofa la masaki karibu na nyumba ya Lowassa( ubalozi wa afrika kusini wamepanga) na nyumba ya Morogoro. Kila mtu anadai kivyake mifano ipo ya kutosha.

Shule kama za waislamu Isimailia ( aga khan) kama Mzizima, Tambaza, zanaki, azania na nyingine hazikuwa chini ya bakwata lakini pia waislamu wa madhehebu ya suni na shia hawakuwa na shule na hospitali na wengi ni waafrika weusi inawezekana aga khan hawana hoja ya kutaka shule zao lakini bado zipo.
 

wakati mwingine takwimu zinapotosha kwani hazielezi chanzo zinaeleza matokeo ya mwisho.

ukitaka kujua kwa nini waislamu hawako wengi kwenye ajira au kwa nini wakristo ni wengi ni lazima ufuatilie watoto wanaoanza la kwanza mashule ya umma na binafsi wa dini zote hadi chuo kikuu. sababu haiwezi kuwa moja ni nyingi tu.

Niliwahi kutoa mfano kwamba darasa analosoma mwanangu ( grade 2) katika shule binafsi eneo la upanga lina watoto 31 lakini watoto wa kiislamu ni 3 tu. Nilijua kupitia siku ya wazazi nilipokuwa nafuatilia maendeleo ya mtoto wangu ( Parent's day) mwalimu alinipa orodha ya watoto wa darasa kisha nikapata picha za watoto hao kwa mchanganyiko wa dini zao. NECTA sio iliyochagua watoto wetu kusoma shule hii.

Hakika nilimuuliza mwalimu kama shule hiyo inazuia waislamu akasema hapana. Je, jibu lake nini hapo wana JF? nenda kwenye shule nyingi hasa binafsi ambazo zinatoa elimu bora kwa sasa kuliko hizi za serikali tunazogombania zitupe elimu bora utakuta watoto wa kiislamu ni wachache sana. Hii ina athari ya muda mrefu kwa maisha ya watoto wa jamii ya kiislamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…