Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini


Weka data we gasho nini
 
Nimeyapenda maelezo ya Dr.W.Slaa, ila kuna sehemu ameniacha. Sijajua kama aliwahi ulizwa na kufafanua hapo aliponiacha. Mwanzo kulikuwa na Utatu wa TEC, BAKWATA na CCT ukatengeneza umoja ulokuwa unaongea na serikali na wote changamoto zao zilifanana kwa mujibu wa kauli yake. Mie niulize tu, BAKWATA walibakia wapi kwenye hilo basi lililoundwa? Ni hapo tu ndo sijamuelewa.
 
Ilipokuja issue ya maslahi nadhani wao bakwata walikua wameenda kunywa chai basi likawaacha msamvu
 
kwahiyo Edward Lowassa ndie aliedondoka signature hapo??? Daaah hatariii
 

Wanawaza elimu ya mbinguni wasijue kuwa bila elimu dunia ni sawa na bure
 
Napata shida sana mtu anapotoa takwimu kwa kugawa wakristo wangapi na waislamu wangapi?Hivi huu udini udini utaisha lini?Ni takwimu za kibaguzi zenye mlengo wa kugawa watu.Kimsingi mtoaji takwimu hana nia njema!
 
Dini hizi zitusaidie kumjua Mungu,kumpenda na kumtumikia ili mwisho tuione pepo ya milele.Maana yake "dini hizi" daraja la kutufikisha huko tu BASI!!Haya mengine ni MANJONJO tu ya duniani.Ukiwa "religionalist" sana kila jambo utaligawa kwenye ukristo na uislamu.Tumepandikizwa mbegu mbaya kuona dini ni jambo kubwa kuliko hata MUNGU mwenyewe!
 
Kwahiyo serikal na tec na cct mliona bora mou muweke nyinyi tu waislamu wasialikwe?..., huon hilo ndo tatzo?
 
Mimi nafikiri tatizo labda ni kwa sababu dini na madhehebu mengine ukiachilia mbali wakristo na madhehebu yao hazikuwekeza sana katika huduma muhimu za kijamii hasa elimu na afya na kujikuta wamejikita zaidi kwenye elimu ahera na kuusahau ustawi wa mwili kiafya na kimaarifa.

Laiti wangekuwa ktk mstari kama huu wa wenzao wakristo, ni wazi sera ya serikali ya Nyerere JK ya utaifishaji ya wakati ule nao isingewaacha, miundombinu yao ya elimu na afya ingechukuliwa tu na serikali kwa manufaa ya watu wote pasipo kujali dini ya mtu.

Mimi pia nimemwelewa Dr Slaa kwa nyongeza ya maelezo yake juu ya MoU. Kimantiki haina tafsiri ya shughuli za kidini moja kwa moja tofauti na waislamu wanavyoitafsiri na kuelewa.

However, mimi napendekeza kwamba, kama waislamu wanaona kuwa serikali kwa kuchukua (kutaifisha) miundombinu ya huduma za kijamii i.e elimu na afya iliyojengwa kwa nguvu na jasho la waumini wa dini ya kikristo ili iwe ya kitaifa ni tatizo kwao na inawapa picha kwamba nchi hii inaendeshwa kwa mfumokristo, basi serikali iwarejeshee wenye mali hizo (wakristo wa TEC na CCT) mali zao na wakati huo serikali irejeshe majengo yale ya Morogoro na kwingineko mikononi mwa wananchi/serikali iliyowapa waislamu kuanzisha Chuo kikuu chao!.

Najua hili halipo na haliwezekani chini ya CCM na pengine hata kama ni chama chochote kinachoweza kutwaa madaraka ya uongozi wa serikali na dola iwe CHADEMA au CUF au chochote.

Na ni kwa kuwa sbb ziko wazi sana, kwa mfano, katika sekta ya elimu ukiachilia mbali shule za sekondari nyingi, duni na za hovyo za kata sina hakika kama serikali imewahi kujenga shule za maana kama zilivyo Iliboru, Mzumbe, Msalato, Tabora Boys, Tabora Girls na zingine nyingi zilizozagaa nchi nzima ambazo zote zilikuwa za makanisa lakini leo zinaitwa za umma wa wote na dini zote!

Vivyohivyo ktk sekta ya afya. Hospital kama hii ya Muhimbili, Bugando, KCMC na nyingine nyingi Tanzania nzima.

Na ni kwa sababu gani turudi huko, anyway???
 

nenda nae taratibu; cha'gamoto zilikua ni ardhi iloporwa pamoja na majengo lkn pia hali mbaya ya majengo yaliyokua yamechukuliwa na serikali
Kwa bahat mbaya bakwata hawakua sehem ya changamoto hizo kwa kua hawakua na shule wala hpspital au ardhi walokua wanaidai; So naturally wakawa hawana la kudai na hivyo hawakua na sababu ya kuingia kwenye mazungumzo na serikali
 
Kwa muda mrefu sana nilijaribu sana kujizuia kuingia mada kama hizi kwa sababu kila nitakacho andika kitatafsrika kama hisia badala ya watu kuutazama UKWELI kisha wakapima maelezo yangu juu ya mada kama hizi, lakini maadam mada hii imekuwa ikirudishwa hapa ukumbini imenilazimu niseme yangu na kwa mtazamo wangu mimi binafsi kwa faida ya wale wanaotaka kutazama pande mbili..

Swala la UTAIFISHAJI wa mali za watu ulikuwa ni mpango wa Kitaifa ambao ulitokana na AZIMIO LA ARUSHA na sii tu mali za makanisa zilitaifishwa bali hata mali za watu binafsi kwa malengo makubwa zaidi ya Kisiasa na Kiuchumi kwa sababu tuliweka malengo juu ya Taifa gani tulotaka kulijenga na hivyo siasa za UJAMAA na KUJITEGEMEA uliwalenga Watanzania wenyewe kumiliki njia kuu za Uchumi na utoaji huduma sawa kwa wananchi wote.

Swala la MOU ni swala tata sana na haliwezi kupembuliwa kwa mjadala finyu kwa sababu sheria ya nchi ni moja tu. Iliposemwa KUTAIFISHA mashirka yote yalokuwa mikononi mwa wageni yalitaifishwa. Na Hivyo hivyo inapotokea sheria mpya ya Ubinafsishaji sheria hiyo itatumika kwa misingi ile ile kwa vyombo vyote vya serikali aidha kurudishwa kwa wenyewe ama kuuzwa. Serikali haiwezi kuingia Muafaka na kuunda chombo cha ushirika na kanisa nje ya sheria, maana Memorundum ni maridhiano. MOU ni muafaka baina ya serikali na Kanisa nje ya sheria mama kuunda chombo cha ushirika baina ya serikali na vyombo vya dini.

Pili, Chini ya misingi tuloiweka wakati ule, serikali yetu ndiyo ilokataza Wahisanii wa Kiislaam walotoka Misri kwa makusudio ya kujenga University ya Kiislaam nchini kutokana na Azimio la kuondoa ama kuzuia vyombo vya kidini kuhodhi, kusimamia na kuendesha utoaji huduma ya ELIMU na AFYA kwa wananchi wake, isipokuwa vyombo hivyo vinaweza kutoa elimu za kiimani za dini na madhehebu kama kama vile Seminaries ili kuwapa wananchi uhuru wa kuabudu na kujielimisha kiimani pasipo serikali kuingilia ibada zao.

Tukiacha wakati ule wa siasa za Ujamaa, hivi majuzi tu baada ya mageuzi ya kiuchumi, serikali imeendelea kupinga wahisani wa kiislaam kutoka nje kama OIC walotaka kuisaidia BAKWATA katika maswala utoaji huduma za ELIMU na AFYA kwa visingizio kwamba OIC iklitaka taifa liwe mwanachama na nchi yetu haiwezi kuwa wanachama wa chombo cha kidini wakati Tanzania ni mwanachama wa YMCA, Red Cross na kadhalika, licha ya kwamba serikali imeingia mufaka na chombo cha kidini kuendesha kwa pamoja shughuli za Elimu na Afya kinyume cha sheria..

Kwa hiyo, Kiongozi wa Chadema mkuu Dr.Slaa anapotumia sababu za serikali kushindwa kuziendesha Shule na vituo vya Afya vilivyokuwa chini ya serikali lakini serikali hiyo hiyo imeweza kuendesha Shule na vituo vyake vya Afya ambavyo havikuwa mali ya makanisa hadi leo hii inanipa wasiwasi mkubwa juu ya siasa gani anazosimamia, yaani anataka tuamini kuwa serikali hii iliweza kuendesha Hospital ya Muhimbili lakini walishindwa kuendesha Hospital ya Bugando!..

Ikumbukwe kuwa ni serikali hii hii ya CCM ilodai tulibinafsisha viwanda na mashirika ya UMMA kwa sababu serikali ilishindwa kuviendeleza lakini la ajabu, Ubinafsishaji wenyewe umerudisha mali hizo kwa WATAWALA walokuwa wameitawala nchi hii KiUCHUMI huku wakitugawa ktk matabaka ya makabila na dini tukasahau kwamba hii ndio asili ya kuweka maazimio yetu ya Kitaifa ili kuvunja misingi hiyo. Leo hii imefikia mahala watu tunajipongeza kurudi ujenzi wa misingi ile ile ya Taifa tegemezi na utengano tukasahau hotuba ya mwisho ya baba wa Taifa Mwl. Nyerere akihutubia mkutano mkuu wa NEC Dodoma mwaka 1995 kabla ya uchaguzi wa rais wa awamu ya 3 (Mkapa) akikemea mambo manne yalojitokeza ndani ya utawala wa Mwinyi kuwa ni RUSHWA, UDINI, UKABILA na UKANDA. Leo tunadiriki kutumia mifano inayopuuza hotuba ile tukijenga hoja zinazotugawa pasipo aibu..

Msema kweli kipenzi cha Mungu, Hotuba ile siku hizi naisikiliza mara nyingi kuliko wakati wowote ule na kutambua nini mwalimu alikuwa akizungumzia na kwamba watu wameazimia kuturudisha nyuma. Maajabu ya kisiasa ilinishangaza sana kiongozi kama Dr.Slaa alokuwa akipiga vita kimfumo - 1. Ufisadi, 2. Taifa hili kuendelea kuwa tegemezi la misaada ya wahisani wa nje, 3. Kiongozi aliyepinga ubinafsishaji holela wa mashirika na viwanda ambavyo vilikuwa vyanzo vyetu vya Ujenzi wa jamii hii ya Kitanzania, leo afike mahala ageuke na kutazama nyuma kuonyesha msimamo kinzani na itikadii yake kisiasa kwa sababu maswala ya elimu na Afya yamehusiana na imani yake ya dini.

Pamoja na yote hayo nimalizie kwa kusema namshukuru Dr.Slaa kwa maelezo yake mazuri sana yanayotoka moyoni mwake akisema ukweli ambao yeye aliujua na kuamini ama kuonyesha ni kiasi gani alihusika na mkataba huo maana kama sikosei nimemsoma mahala akitumia neno SISI tulipoongea na wahisani akiwa upande wa kanisa. Sehemu nyingi kajiweka yeye upande wa Kanisa pengine kwa sababu alikuwa mtumishi wa Mungu ama mwenye mamlaka ndani ya muafaka baina ya washirika akiwakilisha kanisa lake..

January 12, 2013 ni siku ambayo nilifanya maamuzi magumu japo sijui kama yalikuwa maamuzi sahihi...
 

Wakati fulani Benjamini W. Mkapa alipounda Parorle aliona sawa lakini baada ya muda mfupi kabla hajaiapisha ili ianze kazi akagundua au alishauriwa kwamba haiko sawa kwa sababu haina Uwiano, ikabidi aifumue na kuipanga upya, kama utawala uko vizuri na unatendea mema Wananchi wake hutasikia chokochoko lakini pale unapotenda kinyume na matarajio yao lazima manung'unuko yatasikika na chokochoko zitaanza.

Ukiona hayo yanaanza kujitokeza elewa kuna shida anza kushughulikia kwa taratibu na kwa hadhari kubwa kwani hali hugeuka na kua mbaya pale ambapo Upande wa wale wanaona kwamba wanakandamizwa Watabezwa na kudharauliwa.

kugawa Keki ya Taifa kwa upendeleo hakuwezi kuiacha nchi salama, kuacha Watu wengine waishi maisha ya juu kwa UFISADI wa kuiba mali ya Umma huku wananchi wakishindwa kupata Dawa kwenye hospitali za UMMA hatutabaki salama kinachotakiwa ni UADILIFU na kufanya UPEMBUZI YAKINIFU Je? mpaka sasa baada ya miaka yote hii MoU bado inatakiwa iendelee au Wakati sasa umefika wa Serikali kujenga Miundo mbinu yake ya AFYA na ELIMU kwa ajili ya wananchi wake na kuacha kutegemea Taasisi za Dini.
 
Juzi kuna Muhasibu wa KCMC alimuandikia barua rais Kikwete kuwa wasitishe kutoa ruzuku KCMC Hospital watu wanagawana tu hizo pesa za ruzuku!!!.

Kuna jamaa wiki iliyopita analalamika Bugando Hospital wamegoma kumpa maiti ya kaka yake mpaka alipe milioni moja deni la dawa jamaa anasema marehemu amekaa wiki tu hapo hospital.


Nimeangalia hilo jedwali nimebaki nashangaa tu.
 
Kwa mwanasiasa kariba ya Dr.Slaa hakutakiwa kabisa kujiingiza katika maswala haya ili kujenga hoja inayounga mapokezi ya mfumo ulojenga Udini ambao mwalimu Nyerere aliukemea mwaka 1995 katika mkutano mkuu wa chama Dodoma. Bora angesema, kushindwa kwa serikali kuendesha vyombo vyote vya ELIMU na AFYA toka wakati wa ubinafsishaji ni matokea ya sera mbovu wa serikali ya CCM katika kuvipa vipaumbele vyanzo vya utoaji huduma kama ELIMU na AFYA kwa sababu binafsi naamini kabisa serikali yetu ina uwezo mkubwa wa kuboresha huduma hizo ikiwa sera na mipango ya kiuchumi na huduma itavipa kipaumbele katika bajeti ya matumizi ya serikali..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…