Kwa muda mrefu sana nilijaribu sana kujizuia kuingia mada kama hizi kwa sababu kila nitakacho andika kitatafsrika kama hisia badala ya watu kuutazama UKWELI kisha wakapima maelezo yangu juu ya mada kama hizi, lakini maadam mada hii imekuwa ikirudishwa hapa ukumbini imenilazimu niseme yangu na kwa mtazamo wangu mimi binafsi kwa faida ya wale wanaotaka kutazama pande mbili..
Swala la UTAIFISHAJI wa mali za watu ulikuwa ni mpango wa Kitaifa ambao ulitokana na AZIMIO LA ARUSHA na sii tu mali za makanisa zilitaifishwa bali hata mali za watu binafsi kwa malengo makubwa zaidi ya Kisiasa na Kiuchumi kwa sababu tuliweka malengo juu ya Taifa gani tulotaka kulijenga na hivyo siasa za UJAMAA na KUJITEGEMEA uliwalenga Watanzania wenyewe kumiliki njia kuu za Uchumi na utoaji huduma sawa kwa wananchi wote.
Swala la MOU ni swala tata sana na haliwezi kupembuliwa kwa mjadala finyu kwa sababu sheria ya nchi ni moja tu. Iliposemwa KUTAIFISHA mashirka yote yalokuwa mikononi mwa wageni yalitaifishwa. Na Hivyo hivyo inapotokea sheria mpya ya Ubinafsishaji sheria hiyo itatumika kwa misingi ile ile kwa vyombo vyote vya serikali aidha kurudishwa kwa wenyewe ama kuuzwa. Serikali haiwezi kuingia Muafaka na kuunda chombo cha ushirika na kanisa nje ya sheria, maana Memorundum ni maridhiano. MOU ni muafaka baina ya serikali na Kanisa nje ya sheria mama kuunda chombo cha ushirika baina ya serikali na vyombo vya dini.
Pili, Chini ya misingi tuloiweka wakati ule, serikali yetu ndiyo ilokataza Wahisanii wa Kiislaam walotoka Misri kwa makusudio ya kujenga University ya Kiislaam nchini kutokana na Azimio la kuondoa ama kuzuia vyombo vya kidini kuhodhi, kusimamia na kuendesha utoaji huduma ya ELIMU na AFYA kwa wananchi wake, isipokuwa vyombo hivyo vinaweza kutoa elimu za kiimani za dini na madhehebu kama kama vile Seminaries ili kuwapa wananchi uhuru wa kuabudu na kujielimisha kiimani pasipo serikali kuingilia ibada zao.
Tukiacha wakati ule wa siasa za Ujamaa, hivi majuzi tu baada ya mageuzi ya kiuchumi, serikali imeendelea kupinga wahisani wa kiislaam kutoka nje kama OIC walotaka kuisaidia BAKWATA katika maswala utoaji huduma za ELIMU na AFYA kwa visingizio kwamba OIC iklitaka taifa liwe mwanachama na nchi yetu haiwezi kuwa wanachama wa chombo cha kidini wakati Tanzania ni mwanachama wa YMCA, Red Cross na kadhalika, licha ya kwamba serikali imeingia mufaka na chombo cha kidini kuendesha kwa pamoja shughuli za Elimu na Afya kinyume cha sheria..
Kwa hiyo, Kiongozi wa Chadema mkuu Dr.Slaa anapotumia sababu za serikali kushindwa kuziendesha Shule na vituo vya Afya vilivyokuwa chini ya serikali lakini serikali hiyo hiyo imeweza kuendesha Shule na vituo vyake vya Afya ambavyo havikuwa mali ya makanisa hadi leo hii inanipa wasiwasi mkubwa juu ya siasa gani anazosimamia, yaani anataka tuamini kuwa serikali hii iliweza kuendesha Hospital ya Muhimbili lakini walishindwa kuendesha Hospital ya Bugando!..
Ikumbukwe kuwa ni serikali hii hii ya CCM ilodai tulibinafsisha viwanda na mashirika ya UMMA kwa sababu serikali ilishindwa kuviendeleza lakini la ajabu, Ubinafsishaji wenyewe umerudisha mali hizo kwa WATAWALA walokuwa wameitawala nchi hii KiUCHUMI huku wakitugawa ktk matabaka ya makabila na dini tukasahau kwamba hii ndio asili ya kuweka maazimio yetu ya Kitaifa ili kuvunja misingi hiyo. Leo hii imefikia mahala watu tunajipongeza kurudi ujenzi wa misingi ile ile ya Taifa tegemezi na utengano tukasahau hotuba ya mwisho ya baba wa Taifa Mwl. Nyerere akihutubia mkutano mkuu wa NEC Dodoma mwaka 1995 kabla ya uchaguzi wa rais wa awamu ya 3 (Mkapa) akikemea mambo manne yalojitokeza ndani ya utawala wa Mwinyi kuwa ni RUSHWA, UDINI, UKABILA na UKANDA. Leo tunadiriki kutumia mifano inayopuuza hotuba ile tukijenga hoja zinazotugawa pasipo aibu..
Msema kweli kipenzi cha Mungu, Hotuba ile siku hizi naisikiliza mara nyingi kuliko wakati wowote ule na kutambua nini mwalimu alikuwa akizungumzia na kwamba watu wameazimia kuturudisha nyuma. Maajabu ya kisiasa ilinishangaza sana kiongozi kama Dr.Slaa alokuwa akipiga vita kimfumo - 1. Ufisadi, 2. Taifa hili kuendelea kuwa tegemezi la misaada ya wahisani wa nje, 3. Kiongozi aliyepinga ubinafsishaji holela wa mashirika na viwanda ambavyo vilikuwa vyanzo vyetu vya Ujenzi wa jamii hii ya Kitanzania, leo afike mahala ageuke na kutazama nyuma kuonyesha msimamo kinzani na itikadii yake kisiasa kwa sababu maswala ya elimu na Afya yamehusiana na imani yake ya dini.
Pamoja na yote hayo nimalizie kwa kusema namshukuru Dr.Slaa kwa maelezo yake mazuri sana yanayotoka moyoni mwake akisema ukweli ambao yeye aliujua na kuamini ama kuonyesha ni kiasi gani alihusika na mkataba huo maana kama sikosei nimemsoma mahala akitumia neno SISI tulipoongea na wahisani akiwa upande wa kanisa. Sehemu nyingi kajiweka yeye upande wa Kanisa pengine kwa sababu alikuwa mtumishi wa Mungu ama mwenye mamlaka ndani ya muafaka baina ya washirika akiwakilisha kanisa lake..
January 12, 2013 ni siku ambayo nilifanya maamuzi magumu japo sijui kama yalikuwa maamuzi sahihi...