Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

kwa hali yeyote wewe ama huelewi kirahisi, au mpotoshaji wa makusudi, au mchonganishi alipwaye, au mchumia tumbo asiyeshiba.
Dr. Slaa kama Mtanzania mwenye kufahamu jambo hili kiundani na ambaye anaipenda nchi yake na mzalendo kwa Taifa lake hawezi kuacha jambo la hatari katika nchi lijisogeze kwenye fikra za watu huku yeye akikaa kimya tu kama walivyo majizi wengine, ameeleza yote anayoyajuwa na kuondoa fikra mgando ndani ya vichwa vya watu, na pia ameondoa kiwingu kilichokuwa kinaletwa na watu ama wasiotakia mema taifa letu au wenye malengo yao ya kutawala kwa kuwagawa watanzania.
Hata hivyo tupeni majibu juu ya nssf na orci mbona kuna minong'ono kuwa kama wewe si Ally, au Juma, au Amina , au Jasmine , au Khadija hupati kazi na kama uliwahi kupata huko nyuma basi hupandi cheo?
Labda yupo Dr. Slaa mwingine kwa upande huu tujalieni kujuwa hilo nalo.
Bismilah toufoq.

Weka data we gasho nini
 
Nimeyapenda maelezo ya Dr.W.Slaa, ila kuna sehemu ameniacha. Sijajua kama aliwahi ulizwa na kufafanua hapo aliponiacha. Mwanzo kulikuwa na Utatu wa TEC, BAKWATA na CCT ukatengeneza umoja ulokuwa unaongea na serikali na wote changamoto zao zilifanana kwa mujibu wa kauli yake. Mie niulize tu, BAKWATA walibakia wapi kwenye hilo basi lililoundwa? Ni hapo tu ndo sijamuelewa.
 
Ilipokuja issue ya maslahi nadhani wao bakwata walikua wameenda kunywa chai basi likawaacha msamvu
 
Nimeyapenda maelezo ya Dr.W.Slaa, ila kuna sehemu ameniacha. Sijajua kama aliwahi ulizwa na kufafanua hapo aliponiacha. Mwanzo kulikuwa na Utatu wa TEC, BAKWATA na CCT ukatengeneza umoja ulokuwa unaongea na serikali na wote changamoto zao zilifanana kwa mujibu wa kauli yake. Mie niulize tu, BAKWATA walibakia wapi kwenye hilo basi lililoundwa? Ni hapo tu ndo sijamuelewa.

Wanawaza elimu ya mbinguni wasijue kuwa bila elimu dunia ni sawa na bure
 
Napata shida sana mtu anapotoa takwimu kwa kugawa wakristo wangapi na waislamu wangapi?Hivi huu udini udini utaisha lini?Ni takwimu za kibaguzi zenye mlengo wa kugawa watu.Kimsingi mtoaji takwimu hana nia njema!
 
Dini hizi zitusaidie kumjua Mungu,kumpenda na kumtumikia ili mwisho tuione pepo ya milele.Maana yake "dini hizi" daraja la kutufikisha huko tu BASI!!Haya mengine ni MANJONJO tu ya duniani.Ukiwa "religionalist" sana kila jambo utaligawa kwenye ukristo na uislamu.Tumepandikizwa mbegu mbaya kuona dini ni jambo kubwa kuliko hata MUNGU mwenyewe!
 
Kwahiyo serikal na tec na cct mliona bora mou muweke nyinyi tu waislamu wasialikwe?..., huon hilo ndo tatzo?
 
Mimi nafikiri tatizo labda ni kwa sababu dini na madhehebu mengine ukiachilia mbali wakristo na madhehebu yao hazikuwekeza sana katika huduma muhimu za kijamii hasa elimu na afya na kujikuta wamejikita zaidi kwenye elimu ahera na kuusahau ustawi wa mwili kiafya na kimaarifa.

Laiti wangekuwa ktk mstari kama huu wa wenzao wakristo, ni wazi sera ya serikali ya Nyerere JK ya utaifishaji ya wakati ule nao isingewaacha, miundombinu yao ya elimu na afya ingechukuliwa tu na serikali kwa manufaa ya watu wote pasipo kujali dini ya mtu.

Mimi pia nimemwelewa Dr Slaa kwa nyongeza ya maelezo yake juu ya MoU. Kimantiki haina tafsiri ya shughuli za kidini moja kwa moja tofauti na waislamu wanavyoitafsiri na kuelewa.

However, mimi napendekeza kwamba, kama waislamu wanaona kuwa serikali kwa kuchukua (kutaifisha) miundombinu ya huduma za kijamii i.e elimu na afya iliyojengwa kwa nguvu na jasho la waumini wa dini ya kikristo ili iwe ya kitaifa ni tatizo kwao na inawapa picha kwamba nchi hii inaendeshwa kwa mfumokristo, basi serikali iwarejeshee wenye mali hizo (wakristo wa TEC na CCT) mali zao na wakati huo serikali irejeshe majengo yale ya Morogoro na kwingineko mikononi mwa wananchi/serikali iliyowapa waislamu kuanzisha Chuo kikuu chao!.

Najua hili halipo na haliwezekani chini ya CCM na pengine hata kama ni chama chochote kinachoweza kutwaa madaraka ya uongozi wa serikali na dola iwe CHADEMA au CUF au chochote.

Na ni kwa kuwa sbb ziko wazi sana, kwa mfano, katika sekta ya elimu ukiachilia mbali shule za sekondari nyingi, duni na za hovyo za kata sina hakika kama serikali imewahi kujenga shule za maana kama zilivyo Iliboru, Mzumbe, Msalato, Tabora Boys, Tabora Girls na zingine nyingi zilizozagaa nchi nzima ambazo zote zilikuwa za makanisa lakini leo zinaitwa za umma wa wote na dini zote!

Vivyohivyo ktk sekta ya afya. Hospital kama hii ya Muhimbili, Bugando, KCMC na nyingine nyingi Tanzania nzima.

Na ni kwa sababu gani turudi huko, anyway???
 
Nimeyapenda maelezo ya Dr.W.Slaa, ila kuna sehemu ameniacha. Sijajua kama aliwahi ulizwa na kufafanua hapo aliponiacha. Mwanzo kulikuwa na Utatu wa TEC, BAKWATA na CCT ukatengeneza umoja ulokuwa unaongea na serikali na wote changamoto zao zilifanana kwa mujibu wa kauli yake. Mie niulize tu, BAKWATA walibakia wapi kwenye hilo basi lililoundwa? Ni hapo tu ndo sijamuelewa.

nenda nae taratibu; cha'gamoto zilikua ni ardhi iloporwa pamoja na majengo lkn pia hali mbaya ya majengo yaliyokua yamechukuliwa na serikali
Kwa bahat mbaya bakwata hawakua sehem ya changamoto hizo kwa kua hawakua na shule wala hpspital au ardhi walokua wanaidai; So naturally wakawa hawana la kudai na hivyo hawakua na sababu ya kuingia kwenye mazungumzo na serikali
 
Kwa muda mrefu sana nilijaribu sana kujizuia kuingia mada kama hizi kwa sababu kila nitakacho andika kitatafsrika kama hisia badala ya watu kuutazama UKWELI kisha wakapima maelezo yangu juu ya mada kama hizi, lakini maadam mada hii imekuwa ikirudishwa hapa ukumbini imenilazimu niseme yangu na kwa mtazamo wangu mimi binafsi kwa faida ya wale wanaotaka kutazama pande mbili..

Swala la UTAIFISHAJI wa mali za watu ulikuwa ni mpango wa Kitaifa ambao ulitokana na AZIMIO LA ARUSHA na sii tu mali za makanisa zilitaifishwa bali hata mali za watu binafsi kwa malengo makubwa zaidi ya Kisiasa na Kiuchumi kwa sababu tuliweka malengo juu ya Taifa gani tulotaka kulijenga na hivyo siasa za UJAMAA na KUJITEGEMEA uliwalenga Watanzania wenyewe kumiliki njia kuu za Uchumi na utoaji huduma sawa kwa wananchi wote.

Swala la MOU ni swala tata sana na haliwezi kupembuliwa kwa mjadala finyu kwa sababu sheria ya nchi ni moja tu. Iliposemwa KUTAIFISHA mashirka yote yalokuwa mikononi mwa wageni yalitaifishwa. Na Hivyo hivyo inapotokea sheria mpya ya Ubinafsishaji sheria hiyo itatumika kwa misingi ile ile kwa vyombo vyote vya serikali aidha kurudishwa kwa wenyewe ama kuuzwa. Serikali haiwezi kuingia Muafaka na kuunda chombo cha ushirika na kanisa nje ya sheria, maana Memorundum ni maridhiano. MOU ni muafaka baina ya serikali na Kanisa nje ya sheria mama kuunda chombo cha ushirika baina ya serikali na vyombo vya dini.

Pili, Chini ya misingi tuloiweka wakati ule, serikali yetu ndiyo ilokataza Wahisanii wa Kiislaam walotoka Misri kwa makusudio ya kujenga University ya Kiislaam nchini kutokana na Azimio la kuondoa ama kuzuia vyombo vya kidini kuhodhi, kusimamia na kuendesha utoaji huduma ya ELIMU na AFYA kwa wananchi wake, isipokuwa vyombo hivyo vinaweza kutoa elimu za kiimani za dini na madhehebu kama kama vile Seminaries ili kuwapa wananchi uhuru wa kuabudu na kujielimisha kiimani pasipo serikali kuingilia ibada zao.

Tukiacha wakati ule wa siasa za Ujamaa, hivi majuzi tu baada ya mageuzi ya kiuchumi, serikali imeendelea kupinga wahisani wa kiislaam kutoka nje kama OIC walotaka kuisaidia BAKWATA katika maswala utoaji huduma za ELIMU na AFYA kwa visingizio kwamba OIC iklitaka taifa liwe mwanachama na nchi yetu haiwezi kuwa wanachama wa chombo cha kidini wakati Tanzania ni mwanachama wa YMCA, Red Cross na kadhalika, licha ya kwamba serikali imeingia mufaka na chombo cha kidini kuendesha kwa pamoja shughuli za Elimu na Afya kinyume cha sheria..

Kwa hiyo, Kiongozi wa Chadema mkuu Dr.Slaa anapotumia sababu za serikali kushindwa kuziendesha Shule na vituo vya Afya vilivyokuwa chini ya serikali lakini serikali hiyo hiyo imeweza kuendesha Shule na vituo vyake vya Afya ambavyo havikuwa mali ya makanisa hadi leo hii inanipa wasiwasi mkubwa juu ya siasa gani anazosimamia, yaani anataka tuamini kuwa serikali hii iliweza kuendesha Hospital ya Muhimbili lakini walishindwa kuendesha Hospital ya Bugando!..

Ikumbukwe kuwa ni serikali hii hii ya CCM ilodai tulibinafsisha viwanda na mashirika ya UMMA kwa sababu serikali ilishindwa kuviendeleza lakini la ajabu, Ubinafsishaji wenyewe umerudisha mali hizo kwa WATAWALA walokuwa wameitawala nchi hii KiUCHUMI huku wakitugawa ktk matabaka ya makabila na dini tukasahau kwamba hii ndio asili ya kuweka maazimio yetu ya Kitaifa ili kuvunja misingi hiyo. Leo hii imefikia mahala watu tunajipongeza kurudi ujenzi wa misingi ile ile ya Taifa tegemezi na utengano tukasahau hotuba ya mwisho ya baba wa Taifa Mwl. Nyerere akihutubia mkutano mkuu wa NEC Dodoma mwaka 1995 kabla ya uchaguzi wa rais wa awamu ya 3 (Mkapa) akikemea mambo manne yalojitokeza ndani ya utawala wa Mwinyi kuwa ni RUSHWA, UDINI, UKABILA na UKANDA. Leo tunadiriki kutumia mifano inayopuuza hotuba ile tukijenga hoja zinazotugawa pasipo aibu..

Msema kweli kipenzi cha Mungu, Hotuba ile siku hizi naisikiliza mara nyingi kuliko wakati wowote ule na kutambua nini mwalimu alikuwa akizungumzia na kwamba watu wameazimia kuturudisha nyuma. Maajabu ya kisiasa ilinishangaza sana kiongozi kama Dr.Slaa alokuwa akipiga vita kimfumo - 1. Ufisadi, 2. Taifa hili kuendelea kuwa tegemezi la misaada ya wahisani wa nje, 3. Kiongozi aliyepinga ubinafsishaji holela wa mashirika na viwanda ambavyo vilikuwa vyanzo vyetu vya Ujenzi wa jamii hii ya Kitanzania, leo afike mahala ageuke na kutazama nyuma kuonyesha msimamo kinzani na itikadii yake kisiasa kwa sababu maswala ya elimu na Afya yamehusiana na imani yake ya dini.

Pamoja na yote hayo nimalizie kwa kusema namshukuru Dr.Slaa kwa maelezo yake mazuri sana yanayotoka moyoni mwake akisema ukweli ambao yeye aliujua na kuamini ama kuonyesha ni kiasi gani alihusika na mkataba huo maana kama sikosei nimemsoma mahala akitumia neno SISI tulipoongea na wahisani akiwa upande wa kanisa. Sehemu nyingi kajiweka yeye upande wa Kanisa pengine kwa sababu alikuwa mtumishi wa Mungu ama mwenye mamlaka ndani ya muafaka baina ya washirika akiwakilisha kanisa lake..

January 12, 2013 ni siku ambayo nilifanya maamuzi magumu japo sijui kama yalikuwa maamuzi sahihi...
 
cover.jpg


quote_icon.png
By Dr.W.Slaa


Wana JF,

Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika
. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

1)
Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School (Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2)
Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi Dr. Slaa, ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili :
a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii,
b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria.

Hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) . Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo. Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.
Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando).

Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo.
Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa. Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa. Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.
___________________________________________________

MAJIBU KWA DR SLAAA:


Issue hapa inatokana na Dhana ya Serikali kutokuwa na Dini au Serikali ya Kisekula Dhana hiyo ni maarufu Tanzania. Mara nyingi katika masuala yahusuyo dini, viongozi wa serikali husikika wakisema «serikali haina dini, ila wananchi wake wana dini zao ». Hoja ya usekula wa serikali ni ya kihistoria. Ilijengwa kiasi cha miaka miambili iliyopita ikitaka serikali ijiepushe na shughuli za kidini hususan katika masuala ya elimu, mafundisho ya maadili na na ibada.Japokuwa Tanzania imekuwa ikidai kwamba serikali yake ni ya kisekula, hali halisi haioneshi hivyo. Pamoja na madai hayo, serikali ya Tanzania imewahi kuingia katika msuguano na Waislamu na baadhi ya wasiokuwa waislamu pale Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipotaka kuanzisha somo la dini au maadili ya nchi. Kadhia hii ni maarufu kwa jina la “dini mseto”. serikali ya kisekula haiwezi ikaja na mipango ya kusomesha dini kwa jina lolote lile liwe la maadili au vyovyote vile.

Mifano mingine inayotia wasiwasi usekula wa serikali ya Tanzania ni hii ifuatayo:

1. Wimbo wa Taifa – unaomba mungu aibariki nchi

2. Dua ya Bungeni – ina muomba mungu

3. Kuapishwa kwa wanaochukua nafasi za uongozi.
Japo wanaoapa huapa kwa dini zao, aneapishasi kiongozi wa dini husika bali wa serikali au wabunge.

Utaratibu huo hauendani na madai kuwa nchi au serikali ya Tanzania haina dini, bali wananchi wake ndiyo wenye dini. Swali ni je, tunapomtaja Mungu katika wimbo wa taifa au katika dua ya bungeni, na kadhalika, tunamkusudia mungu yupi? Mungu wa Waislamu? Wa Wakristo? Wa dini za asili? Je, kuna mungu wa kitaifa? Mungu huyo wa kitaifa ni yupi na ni wa dini gani?Je, katika hali hiyo, ni kweli serikali haina dini? Katika mazingira ya Waislamu kuandamwa na kukandamizwa na mila ya Mfumokristo, mfumo ambao unajidhihirisha zaidi katika vitendo vya kibaguzi vinavyofanyiwa Waislamu na sehemu kubwa ya watendaji serikalini na katika taasisi mbalimbali, kwa nini mwananchi Muislamu asiamini kuwa serikali hii si ya kisekula bali ni ya kidini; na dini yenyewe ni Mfumokristo.

Kufuatia makubaliano hayo katika ya serikali na makanisa mabilioni ya fedha za walipa kodi yamekuwa yakitolewa kila mwaka kwa taasisi mbalimbali za makanisa zinazotoa huduma za afya nchini. Kwa mfano jedwali lifuatalo linaonesha baadhi ya fedha za umma zilizotolewa mwaka 2009 na 2010 na serikali kwa taasisi mbalimbali za makanisa zinazotoa huduma za afya nchini ikilinganishwa na kiasi cha fedha zinazopelekwa kwa taasisi za afya zinazomilikiwa na serikali.

Data za WIZARA YA AFYA zinaonesha kuwa hospitali na taasisi nyingine za afya zaidi ya 80 zinazomilikiwa na Makanisa zinaendeshwa kwa kutumia fedha za serikali. Aidha utafiti wetu umeonesha kuwa serikali imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kila mwaka kuendesha hospitali na taasisi za afya zinazomilikiwa na Makanisa.

Kwa mfano Jedwali lifuatalo linaonesha fedha za serikali zilizotumiwa na hospitali na taasisi za afya zinazomilikiwa na Makanisa ikilinganishwa na matumizi katika hospitali za serikali mwaka 2009 na 2010.
attachment.php

attachment.php


attachment.php

Jedwali hilo hapo juu linaonesha fedha zilitolewa na serikali kwa hospitali na taasisi nyingine za huduma ya afya zinazomilikiwa na makanisa na zile zinazomilikiwa na serikali kwa ajili ya kulipa mishahara wafanyakazi na gharama za uendeshaji.

Men lie, women lie, numbers dont lie....

attachment.php

attachment.php

attachment.php

chanzo: wizara ya Elimu

Wakati fulani Benjamini W. Mkapa alipounda Parorle aliona sawa lakini baada ya muda mfupi kabla hajaiapisha ili ianze kazi akagundua au alishauriwa kwamba haiko sawa kwa sababu haina Uwiano, ikabidi aifumue na kuipanga upya, kama utawala uko vizuri na unatendea mema Wananchi wake hutasikia chokochoko lakini pale unapotenda kinyume na matarajio yao lazima manung'unuko yatasikika na chokochoko zitaanza.

Ukiona hayo yanaanza kujitokeza elewa kuna shida anza kushughulikia kwa taratibu na kwa hadhari kubwa kwani hali hugeuka na kua mbaya pale ambapo Upande wa wale wanaona kwamba wanakandamizwa Watabezwa na kudharauliwa.

kugawa Keki ya Taifa kwa upendeleo hakuwezi kuiacha nchi salama, kuacha Watu wengine waishi maisha ya juu kwa UFISADI wa kuiba mali ya Umma huku wananchi wakishindwa kupata Dawa kwenye hospitali za UMMA hatutabaki salama kinachotakiwa ni UADILIFU na kufanya UPEMBUZI YAKINIFU Je? mpaka sasa baada ya miaka yote hii MoU bado inatakiwa iendelee au Wakati sasa umefika wa Serikali kujenga Miundo mbinu yake ya AFYA na ELIMU kwa ajili ya wananchi wake na kuacha kutegemea Taasisi za Dini.
 
Juzi kuna Muhasibu wa KCMC alimuandikia barua rais Kikwete kuwa wasitishe kutoa ruzuku KCMC Hospital watu wanagawana tu hizo pesa za ruzuku!!!.

Kuna jamaa wiki iliyopita analalamika Bugando Hospital wamegoma kumpa maiti ya kaka yake mpaka alipe milioni moja deni la dawa jamaa anasema marehemu amekaa wiki tu hapo hospital.


Nimeangalia hilo jedwali nimebaki nashangaa tu.
 
Juzi kuna Muhasibu wa KCMC alimuandikia barua rais Kikwete kuwa wasitishe kutoa ruzuku KCMC Hospital watu wanagawana tu hizo pesa za ruzuku!!!.

Kuna jamaa wiki iliyopita analalamika Bugando Hospital wamegoma kumpa maiti ya kaka yake mpaka alipe milioni moja deni la dawa jamaa anasema marehemu amekaa wiki tu hapo hospital.


Nimeangalia hilo jedwali nimebaki nashangaa tu.
Kwa mwanasiasa kariba ya Dr.Slaa hakutakiwa kabisa kujiingiza katika maswala haya ili kujenga hoja inayounga mapokezi ya mfumo ulojenga Udini ambao mwalimu Nyerere aliukemea mwaka 1995 katika mkutano mkuu wa chama Dodoma. Bora angesema, kushindwa kwa serikali kuendesha vyombo vyote vya ELIMU na AFYA toka wakati wa ubinafsishaji ni matokea ya sera mbovu wa serikali ya CCM katika kuvipa vipaumbele vyanzo vya utoaji huduma kama ELIMU na AFYA kwa sababu binafsi naamini kabisa serikali yetu ina uwezo mkubwa wa kuboresha huduma hizo ikiwa sera na mipango ya kiuchumi na huduma itavipa kipaumbele katika bajeti ya matumizi ya serikali..
 
Back
Top Bottom