Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Kwenye ili Dr.Slaa yupo pamoja na mfumo lakini kwenye siasa anakuwa mkali kweli kuishambulia CCM na kulaani mfumo wake.
 

Mkuu pamoja na uchambuzi mrefu lakini umeshindwa kuficha kitu kimoja - ndani ya nafsi yako una shida kubwa zaidi na "Dr. Slaa" kuliko na "MoU"!
 
Kwenye ili Dr.Slaa yupo pamoja na mfumo lakini kwenye siasa anakuwa mkali kweli kuishambulia CCM na kulaani mfumo wake.

Asiseme anachokijua??

Mimi ni mwislamu namshukuru sana Dr. Slaa kwa kuwa amenifumbua macho, nimepata pa kuanzia..... Hilo jedwali kama ni kweli limenitisha.
 
Mkuu pamoja na uchambuzi mrefu lakini umeshindwa kuficha kitu kimoja - ndani ya nafsi yako una shida kubwa zaidi na "Dr. Slaa" kuliko na "MoU"!
Unayasema haya kwa sababu wewe ni mfuasi wa CDM pengine hunijui vizuri maana Dr.Slaa alikuwa tegemeo letu sote mwaka 2010. Haya yote sikuyajua na pengine nikwambie ndio kuwa MOU ndio sababu kubwa ilonifanya nisimpende rais Mwinyi acha mbali hotuba ya Nyerere ya mwaka 1995.

Ile hotuba, Nyerere alimchana chana bila kuuma maneno rais Mwinyi ikiwa utaisikiiza kwa makini sana na binafsi yangu yanibidi nikiri kuwa hotuba ile ni sabuni ya roho yangu maana imetueleza kinagaubaga ya kuwa maadui wetu sasa sio tena watatu bali ni saba na wote wanatokana na Umaskini!.Nyerere hakumchukia Mwinyi bali alichukia maamuzi yake na taifa alokusudia kulijenga.

Sina sababu ya kuwa na shida na Dr.Slaa isipokuwa kajiponza mwenyewe kisiasa na sikutegemea kabisa kwamba Dr.Slaa alikuwa akiunga mkono maamuzi yalotolewa kuunda muafaka wa MOU.
 
Wawili wapo katika JIHAD bado wengine na baba yao Mohamed Said atawasili muda si mrefu.

Hapa upumbavu na ujinga wa kidin teyari umeanza kufanya uzushi na meengi yakinafiki kuelekea uchaguzi mkuu October 2015.

Ukiwauliza tangu KIKWETE AWAITE WOOTE TENA WADIN ZOOTE KUPELEKA MOU ZAO HAWANA MAJIBU Maana hakuna aliyepeleka - unafiki Tu.

Nidhahili mtaji wa mnafiki nimajungu na uzushi akiaambiwa fanya hawezi.
 

Mkuu naomba niweke kwanza bayana kwamba mimi sio mfuasi wa chadema japo naunga mkono baadhi ya harakati zao (sio zote tafadhali!!!). Pili naomba nikukumbushe kuwa wakati mjadala kuhusu "MoU" ulivyokuwa umepamba moto sana kwenye mitandao ya kijamii na kukawa na upotoshaji mwingi kutokana na ukweli kwamba wengi walikuwa wanajadili bila kujua "MoU" ni nini hasa, ndipo Dr. Slaa alijitokeza hadharani akakiri kuwa wakati "MoU" ilifikiwa yeye alikuwa ni Katibu Mkuu (na hivyo Mtendaji Mkuu) wa TEC. Hapo ndipo alipojaribu kuuweka ukweli hadharani kama alivyoufahamu yeye kwani serikali ilikuwa kimya wakati mitaani watu wanatiana ngeu kwa kutokuwa na ufahamu!
Kilichonigusa binafsi kwenye uchambuzi wako ni jinsi ulivyoelekeza nguvu nyingi kumshambulia "Dr. Slaa" kama mtu binafsi na ukaacha pembeni "Taasisi" za maamuzi zilizoafikiana katika hiyo "MoU" i.e Serikali, TEC, CCT, BAKWATA!
 
Naelewa sana mkuu wangu lakini bado hunipati ya kwamba Dr.Slaa kama mgombea Urais hakutakiwa kuyasema haya kabisa kwa kuunga mkono muafaka ulovunja utawala bora na miiko na maadili ya viongozi ambayo yamepelekea leo tuna Udini nchini. Nilijua Dr.Slaa atakuwa kaona mbali zaidi kisiasa athari za MOU kwa sababu watu hawalalamikii MOU kama MOU bali uvunjaji wa misingi ya maazimio ya taifa tulokusudia kulijenga, na MOU ndio chimbuko hasa la Udini nchini..

Yeye kama alikuwa kiongozi na mwakilishi wa TEC wakati ule alikuwa na interest tofauti na kwa watu tofauti lakini pindi alipoingia SIASA lazima maswala kama hayo ayatazame upya na Kisiasa na kwa mapana zaidi (mfano mzuri Nyerere). Kifupi hakuna aloongea hapo ambalo sisi hatukulijua, yote haya tuliyazungumzia humu JF sana tu tena kwa miaka, tofauti iliyopo hapa ni ushiriki wa Dr.Slaa na nini mtazamo wake kama kiongozi wa siasa na kidini anaonyesha anashindwa ku separate serikali na dini.. Na ndio maana nimempongeza kwa ujasiri mkubwa aloufanya lakini kisiasa kajimaliza. Hakutakiwa kabisa kuandika/kuyasema yote hayo..
 

Mkuu naomba kupingana/tofautiana nawe kwenye mtizamo kwamba "MoU" ndio chimbuko la "Udini"! Serikali ndio chimbuko hasa la "Udini" kwa kukaa kimya pale jamii ya Wa-Islam ilipoibua maswali yaliyotaka kujua ukweli na makando kando yote ya "MoU"! Na serikali ilakaa kimya kama "political strategy" pale walipoona kuwa kuwagawa wa-Tanzania katika misingi ya u-Dini & u-Kabila kutakuwa na manufaa kwao bila kujali athari itakayotokea ki-Taifa kutokana na mpasuko huo! Serikali ingekuwa na weledi na kuweka bayana makando kando yote ya "MoU" hadharani, wala kusingalikuwa na malalamiko toka jamii ya wa-Islam!
 
Asiseme anachokijua??

Mimi ni mwislamu namshukuru sana Dr. Slaa kwa kuwa amenifumbua macho, nimepata pa kuanzia..... Hilo jedwali kama ni kweli limenitisha.
Kama wewe ni muislam mimi inanihusu nini kuna mtu kakuuliza dini yako?
 
Dr.Slaa bora ungekaa kimya tu kwenye haya masuala ya MOU.
 
Akiishi kwa mfumo wa HAYAWANI hata ukimvika vazi jeupe peee bado atalichafua tu.

Shukrani hatuzitegemei kutoka upande B maana kila wakifanyacho upande A wakifai kwao hata kama kina MANUFAA KWA JAMII NZIMA.
 

Akufukuzae Hakwambii Toka, Sasa Mikutano Yenyewe Inafanyikia Kanisani Wewe Ulitarajia Nn Kwa BAKWATA Hapo. Huyu Dr Mi Naona Kama Amesikiliza CD Za Ilunga Hasani Kapungu (Allah Amuweke Mahali Panapostahili) Akatafakariii Ndo Akaona Afunguke, Kwani Naona Ni Kama Amethibisha Yale Alokuwa Akiyasema Mwl Ilunga, Ama Kweli Neema Ikikutoka Ndio Utajua Thamani Yake.
 

BAKWATA Haikuhusishwa Fully, Rudia Maelezo Ya Dr Vzuri Uelewe!
 

nikionacho mimi hizo ni lawama zisizo na msingi somesheni watoto shule na si kucheza vigodoro halafu utegemee mtoto wako atakuwa mkaguzi wa shule au mkurugenzi wa taasisi fulani ni ngumu. mkapa kawapa chuo morogoro mmeshindwa kukiendesha hata kupaka rangi tu majengo mmeshindwa mnakuja kulalama lalama someni acheni lawama.
 
Sasa wewe msomi gani hata kuandika kiswahili shida hujui hata matumizi ya herufi kubwa na ndogo unaandika kama mtoto wa kindergarten.

Teh teh teh teh
 
Kwenye ili Dr.Slaa yupo pamoja na mfumo lakini kwenye siasa anakuwa mkali kweli kuishambulia CCM na kulaani mfumo wake.
sioni hoja yeyote katika haya unayoyasema, Dr. Slaa ametusaidia kutupa historia sahihi ya jambo hili kwa vile wakati linatokea yeye alikuwa kiongozi wa dini, sasa si kiongozi wa dini ni mwanasiasa mwenye mtizamo wake, wewe unajaribu kuonyesha kama vile Dr. Slaa ni kigeugeu kwa malengo ya kisiasa badala ya ukweli wa mambo, ni vema kuitendea haki hoja hii kwa kuiacha ijikite kwenye mantiki yake kuliko kuiteka nyara na kuisiasisha kwa misingi ya kujijengea uhalali wako wa kisisa na genge lako, jikite kwenye haki zaidi badala ya ghilba.
 
NGOLOMBWE hapo juu kuna majedwali yanayojieleza sasa tupe yako ya NSSF.Tuzungumzie facts sio minong'ono
ukitaka data nenda mwenyewe pale nssf kajionee tu, au fanya utafiti mdogo tu tafuta vijana kumi wa dini hizo mbili walioajiriwa pale na uwaulize dini zao na mwaka walioajiriwa utashangaa sana na matokeo ya kautafiti hako kadogo, lakini pia ninashangaa sana ninyi mnapolalamikia madhehebu ya kikristo kuomba tena shule walizojenga kwa sadaka na misaada ya wakristo wenzao wa nje, wakati idadivya watu wanaotibiwa hospitalvza kikristo wengi ni waislam, mfano nzuri hospital ya Mbesa missioni, 85% ya wagonjwa ni waislam na zaidi ya 65% ya waajiriwa ni waislam, sasa sijui mnataka kitu gani!! au mngependa mpewe shule zote na hospital zote za wakristo ziwe zenu? kama chuo kile tu cha morogoro kinawatoa kamasi mtaweza hayo mengine? hizi hoja za kitoto hazina maana kabisa hapa nchini kwetu, acheni kulalamika badala yake fanyeni kazi kwa bidii kujijenga kielimu na kiuchumi muinue jamii ya kiislam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…