MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Tukumbuke:
MOU si mkataba wa makanisa yote nchini( madhehebu yote ya kikristo) kwani mengine hayana shule na hospitali kama kanisa la kakobe na Lusekelo ( mzee wa upako). Baadhi ya makanisa ambayo mimi nitaita ya kibabaishaji hayajihusishi na huduma kwa jamii kwa sababu muundo wake ni kama makanisa ya mtu binafsi. Misikiti mingi pia ni ya watu binafsi ( miliki binafsi) haiko kama taasisi ni ngumu sana kujiendesha kitaasisi katika mazingira haya. Mtu aliyejenga msikiti kwa nguvu yake binafsi huwezi kumshurutisha ajenge shule na hospitali au kumwingilia katika mipango yake ya awali kuwa penye msikiti lazima pawe na shule na hospitali.
Kama pesa ya MOU ingekuwa inakwenda makanisani badala ya kuhudumia jamii hata baadhi ya makanisa yangepiga kelele lakini wanaangushwa na kigezo kwamba ni lazima uwe na miundombinu ya shule na hospitali.
Rais Kikwete amesema wanaotaka MOU bado nafasi ipo lakini bila miundombinu..... tutabishana hapa mpaka kesho.