Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Hakuna ubaya kuingia makubaliano ili Serikali isaidie uendeshaji wa taasisi zinazotoa huduma kwa jamii nzima ya watanzania bila kujali dini na madhehebu yao. Hebu fikiria hospitali kama KCMC pale Moshi isingekuwa inasaidiwa na Serikali, je watu wa hali ya chini kwa kipato tungeweza kumudu gharama za matibabu?. Binafsi naunga sana mkono makubaliano hayo ili uwepo uwajibikaji wa serikali katika kuchangia gharama hizo kwa watu wake.
 
Sitaki kuamini hili lakini uvumi huu umeeneea sana kiasi cha kwamba umenifanya niwe na shauku kutaka kujua yaliyojiri kwenye kusign hiyo memorandum maana naona kwa taarifa nilizokuwa nazo malalamishi ni kuwa serikali imeipa CCT na TEC nguvu kubwa ajabu na matokeo yake leo watu watu wanaanza kulalama kwa nini serikali haiipi nguvu hizo NGO zingine kama walivopewa na serikali. Na under this memorandum seriali inatoa nafasi za kazi kwa Church candidates kwenye chuo chake cha Teachers Training College

Mfano kuna kipengele kinasema hivi:

Hakuna ubaya hata kidogo kwa serikali kusign hii memorandum lakini nataka kujiuliza je ni sawa serikali kufanya agreements kama hizi na taasisi za kidnini? na Je imefanya gareement kama hii na taasisi za Kisslam au wahindu au ni Kanisa tu ndio walifanya nao? Je hamuoni hapo mambo ya bilateral negotiations wakaachiwa wataalam wa mambo hayo?
Buy The time wankubaliana serikali ilikuwa hoi ktk maendeleo ya nchi......asilimia kubwa ya shule na hospital za rufaa, vituo vya mayatima, vituo vya kutibu vilema, etc vilikuwa chini ya makanisa...ki msingi nchi ilikuwa inatunza na makanisa. Sijui unajiuliza unakoabudu kwanini wamekosa kitu km hii... pengine walikuwa busy kogombania pa kuabudia, busy kutafuta darubini bora ya kutafuta angallau chembe au hata harufu ya watu wa imani yao ktk mapambano ya uhuru. so sasa ni km wewe hapa upo busy kujenga misingi ya kudai kuwa kanisa ndilo linaongoza nchi.by the way kizazi cha kesho kitakuwa kinakulaumu kuwa ulikuwa busy for nothing kwani gap linazidi kukua.wenzenu wanajituma ktk haki na usawa. WELL..USISAHAU WAHIMIZA WENZIO WAKATOE SHUKRANI KWA MAKANISA KWA NILITOYATAJA HAPO JUU.zaidi ya kujificha ktk idea duni kuwa kuna ubaguzi.By the way nasikia BABU naye ana makubaliano na serikali bila maandishi kuhusu usalama wake na kuchukua idara ya AFYA..WHACHI YU SEI?P.:tongue: :smash:
 
maoni yangu..watu tujifunze kujiweka karibu na wenzetu waliofanikiwa ili nasi tujifunze kutoka kwao..kwa mfano WACHAGA wameendelea lakini sisi tunatafuta jinsi ya kuwalaani kwa mafanikio yao..wakatoliki ni wazi kuwa wako mbele sana kulinganisha na sisi waisilam kwa hiyo tunahitaji kuwa wakweli na kujiuliza ni kwanini sisi tunazidi kubaki nyuma siku hadi siku..?..tukishajua hayo hatutakuwa na muda wa kuswali x.7.kwa siku kwani tunahitaji time to catch up...
 
Serikali iepuke Negotiations za namna hii zinatia wasiwasi. Kwa nini iwe Kanisa peke yake? Memorandum ya namna hii ihusishe Dini na madhehebu mengine. Serikali inaongoza wananchi siyo Kanisa. MoU ya Serikali ni kwa manufaa ya nchi siyo Kanisa. Serikali yetu haina Dini ila watu wake wana Dini, wakipewa madaraka ya serikali wasi assume dogma za Dini zao.Kufanya hivyo ni kukaribisha mkanganyiko wa kisiasa, kiitikadi, kifalsafa na kiutawala.Wenye nchi mpo!

Kaka unataka ihusishe na dini nyingene kama ipi..hawa wenzetu (wakristu) wanavitu kama mashule,vyuo,mahosipitali ya rufaa,vituo vya watoto yatima,taasisi za mikopo,nk...hivyo ni lazima serikali ikubali yaishe...wenzetu na sisi tumebaki kujenga madrasa wapi wapi..!!!!!!!
 
Hapa kanisa linaformulate education policies....ndio christinization of education system hilo ambalo naona wakristo wamezoea "Kupendelewa"..they cannot stand alone..lazima fedha za umma wote zitumike kuendeleza taasisi za kikristo hii imekaaje?

Sijui unatafsiri vipi neno policies lakini hata nyumbani kwako kunaweza kuwa na policies ukiamua sembuse organ kubwa kama kanisa. Wanapendelewa na serikali kwani jukumu la serikali kutoa elimu na afya walilikabidhi kanisa? Nadhani hii MOU haina tatizo lolote matatizo tunayo Watanzania na udini wetu.

Wanakuja wawekezaji hapa mnawapa misamaha kibao ya kodi ambayo ingeweza kutatua matatizo yaliyopo hamsemi lakini huduma kwa ajili ya Watanzania mnalalama kama nini. Kwali ukoloni bado tunaupenda sana
 
cover.jpg
2-1.jpg
MEMO3.jpg
4.jpg
tano.jpg
sita.jpg
saba.jpg

Sitaki kuamini hili lakini uvumi huu umeeneea sana kiasi cha kwamba umenifanya niwe na shauku kutaka kujua yaliyojiri kwenye kusign hiyo memorandum maana naona kwa taarifa nilizokuwa nazo malalamishi ni kuwa serikali imeipa CCT na TEC nguvu kubwa ajabu na matokeo yake leo watu watu wanaanza kulalama kwa nini serikali haiipi nguvu hizo NGO zingine kama walivopewa na serikali. Na under this memorandum seriali inatoa nafasi za kazi kwa Church candidates kwenye chuo chake cha Teachers Training College

Mfano kuna kipengele kinasema hivi:

Hakuna ubaya hata kidogo kwa serikali kusign hii memorandum lakini nataka kujiuliza je ni sawa serikali kufanya agreements kama hizi na taasisi za kidnini? na Je imefanya gareement kama hii na taasisi za Kisslam au wahindu au ni Kanisa tu ndio walifanya nao? Je hamuoni hapo mambo ya bilateral negotiations wakaachiwa wataalam wa mambo hayo?

Bahati mbaya thread haina initiatives za hao wengine ambazo zilikataliwa na serikali hivyo tunaacha hivyo unless proven otherwise.

Japo thread imeletwa kwa ubaya lakini naungana na wote wanaosema MOU hii ni muhimu. Heading inaonyesha MOU kati ya serikali na "KANISA KATOLIKI" nadhani GT ulikuwa na nia yako fulani lakini bado ukweli utabaki pale pale "Kama serikali inajitosheleza ya nini kubishana si itoe huduma za kijamii tu kivyake bila kujali uwepo wa huduma zinazotolewa na kanisa isipokuwa za kiroho?

Tuangalie kuporomoka kwa elimu na matokeo yasiyoridhisha kwa shule "zisizokuwa za kanisa" nadhani kwa sasa ndiyo inatakiwa kuwa priorities zetu
 
tatizo unaharaka makaratasi umeyageza wewe hizo huduma umenufaikanazo
 
Ni hivi ndugu zanguni, serikali yenyewe imejiona haina uwezo wa kutoa huduma hizo zinazotolewa na taasisi za makanisa. Ingekuwa na uwezo huo kusingekuwa na sababu ya MoU wala kitu kama hicho. Na tena basi marais ambao kwa kiwango kikubwa zaidi wameukubali na kuunga mkono kwa vitendo mchango wa makanisa katika jamii ya watanzania ni Mzee Ruksa (mwislamu) ambaye ndiye aliyerejeshea wakristo taasisi zao zilizotaifishwa na Mwalimu Nyerere (mkristo), na majuzi tumemwona na kumsikia JK (mwislamu mwingine) akitamka hadharani kuwa serikali itaongeza ruzuku kwenye mahospitali ya kanisa. Hawa (Mzee Ruksa na JK) wangekuwa na mawazo ambayo baadhi ya wachangiaji wanaleta hapa ya udini, hali ya utoaji wa huduma za jamii hasa afya ingedorora kwa asilimia kubwa. Tuwe wakweli tu. Na je hao wanaolalamika wamewahi kujenga hospitali zao vijijini kusiko na hospitali ya serikali halafu serikali ikawakatalia ruzuku? Tusiwe na ulalamishi tu usio na tija.
 
"Game Theory" sijui uelewa wako ni kiasi gani.Kwa ufupi hakuna tatatizo lolote na MOU hiyo.Ili taasisi mbili ziweze kufanya kazi lazima yawepo
makubaliano.Hiyo ndo "MOU".Maudhui ya habari unayoleta ijadiliwe inajenga picha ya udini ilhali sio kweli.
Nimefanya kwenye NGO huu mwaka wa 9 sasa.Kwa tarifa yako mashirika ya kidini kama Catholic Relief Services (www.crs.org) yanapotoa huduma hayaangalii walengwa ni wakristo,waislam au wapagani.Nia yao ni kutoa huduma tu.Cha kushangaza zaidi hata ajira hawabagui.Wapo
waislam wanafanya kazi CRS.Hawa CRS wako chini ya Baraza la Maaskofu Wakatoliki Marekani.Lakini pia wana MOU na serikali ya Marekani
kupitia PEPFAR kufanya kazi hapa Tanzania.

Nakushauri ndugu yangu uachane na mawazo ya udini.We chapa kazi ujenge nchi yako na sio kushabikia dini.Watu makini hawashabikii mimi dini au kabila fulani.Shabikia unaifanyia nini nchi yako na familia yako.
Naomba kuwakilisha
 
MoU sio legally binding instrument.Ni jambo linaloendana tu na honest.Hapo hakuna la mjadala
 
Mimi napata shida na watu wanaosema kuna udini kwenye hii MoU. Kwanza kabasa tulitakiwa kushukuru hawa ndugu zetu kwa kutumia ujuzi na moyo walionao ili kuokoa wa-Tanzania kwa miaka yote hii, hii ni kwa sababu hizi hospitali hazipokei Wa-Kristo peke yake. Si ajabu hata Imamu, Shekhe ama Ustaadhi alizaliwa kwenye hospitali ya misheni ama kusoma kwenye shule hizi, anayepinga hili ana matatizo.

Swali la kujiuliza, tungeingia kwenye u-Dini, Majengo ya kilichokuwa Chuo ch Tanesco Morogoro yasingepewa Taasisi ya Ki Islam, je ulishasikia Performance ya Morogoro Islamic University? kama kina perform tafadhali leta hoja. Swala ni taasisi inasaidia nini katika jamii.

Tukitoa hizi Hospitali na Shule za Misheni, Tanzania itazimika. Hapa issue ya OIC inaingiaje?

Tchao
 
To strengthen their social services sector, the two Church bodies that is the Protestants under the Christian Council of Tanzania (CCT) and the Catholics under the Tanzania Episcopal Conference (TEC), in 1992 assisted by the German partner Churches negotiated a "Memorandum of Understanding" with the Tanzania government. In this memorandum the government recognized the important role played by the Churches in the social services sector of the country, pledged to help the Churches by sharing with them grants from foreign government and promised never to nationalize the church institutions again. The "Memorandum of Understanding" authorized the forming of the "Christian Social Services Commission"(CSSC). TEC and CCT are each represented by the General Secretary and four bishops. The Commission has two executive organs, the Christian Medical Board of Tanzania (CMBT) and the Christian Education Board of Tanzania (CEBT) for health and education respectively. This commission formulates common policies for the Education and medical Services of the Churches and negotiates with the Tanzania government in the name of the churches. The two executive organs run common programs. The churches together run more than 50% of the Medical Services and secondary schools in the country.
 
MoU yako hii hapa:

watu walisema ni uvumi tuu haipo , na wakataka ushahidi sasa wenye kubisha wakashindwa la kubisha

https://www.jamiiforums.com/jamii-i...rikali-na-kanisa-katoliki-19.html#post2275059
 
Former President, Alli Hassan Mwinyi is in a better position to answer your question. Likewise, Benjamin Mkapa can tell us what really happened to the TANESCO College in Morogoro.

Edward Lowassa ndiye aliyesign hii Memorandum of Understanding kati ya Kanisa na serikali
 
Edward Lowassa ndiye aliyesign hii Memorandum of Understanding kati ya Kanisa na serikali

Ni kweli Edward Lowassa alisign MoU. Pia ni kweli Lowassa alikuwa rais wa Tanzania 1992. Lowassa alishika wadhifa huo kuanzia mwaka 1985 mpaka 1995!
 
Back
Top Bottom