Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi, gotta problem with that?
Huo ndiyo ukweli
Hata mimi nilitaka kuuliza swali kama hili. Kwani ajabu hapo iko wapi? MoU ni makubaliano kuwa na uelewa wa pamoja kwamba Taasis fulani itatoa huduma fulani katika muktadha fulani na hapa kwa mfano, hizo taasis za "kanisa' zitatoa huduma kufuatana na makubaliano hayo. Serikali nayo imekubali kufanya mambo fulani kama namna ya mashirikiano.Hizo huduma kwani haziwasaidii wenye imani tofauti? Ni lini taasis zenu nyie mnaokereketwa na hii MoU zilikataliwa kusaini MoU na serikali?
Mbona Serikali ina saini MoU n akila taasis inayoshiriki katika kusaidia kufanya kazi au kutoa huduma? Mbona hamuulizi MOU za serikali na UN, Bilaterals kama NORAD, SIDA etc?
Au kwa vile hapa kuna "udini"? Hebu tuache mambo mepesi tujadili issues nzito.Huu udini unakuwa kama ajenda ya siri ya kuleta machafuko hasa ukizingatia wengi wa watanzania bado ni wageni sana wa modalities mbalimbali za namna serikali inavyofaya kazi kushirikiana na taasis zisizo za kiserikali.
Tatizo ni kwanini Serikali imeingia makubaliano na Kanisa; kwa maoni ya watu inaonesha kuwa Serikali inapendelea makanisa. Kwa baadhi ya watu haijalishi kama mambo ya MoU ni ya kawaida au haijalishi kama serikali inafanya hivyo kwa taasisi nyingine hata ziwe za Kihindu au Kiislamu au mashirika mengine yasiyo ya kiserikali. Haijalishi. Tatizo ni kuwa kanisa limeingai makubaliano hayo. Na utaona kuwa watu hawataki kuangalia kabisa kuwa ilipofanyika Rais alikuwa ni Muislamu - hata hilo halijalishi.
Kuna msemo kwamba ni kujaribu kutengeneza kimbunga kwenye kikombe cha chai!
Vitu viwili tofauti umezungumza. Bilateral agreement ni tofauti kabisa na hii memorandum of understanding ilivyosaigniwa. Hii inazungumzia Serikali ya TZ kuipatia funds Kanisa ktk uendeshaji wake.
Ktk Katiba ya TZ, serikali inatakiwa isiwe ina upendeleo wowote na dini yoyote au taasisi yoyote ya kidini. Sasa huoni kama hii memorandum inavunja katiba ya nchi?
The Aga Khan Development Network (AKDN) and its institutional predecessors have had a presence in Tanzania and Zanzibar for more than a century, starting with the establishment of the first Aga Khan Girls School in Zanzibar in 1905. In recognition of AKDN's commitment to the country, an Agreement of Co-operation was signed with the Government of the United Republic of Tanzania in 1991. The Agreement was subsequently revised and endorsed in 2001, and today enables AKDN to contribute significantly to Tanzania's development agenda.
Kama tunakuwa na rais wa nchi (sio TFF) ambaye waziri wake au mtu aliyemteua anaridhia mkataba unaopelekea mabilioni ya fedha za umma zielekezwe kwenye taasisi 'zisizostahili' kupata fedha hizo, tena bila ridhaa ya rais, basi hapo tatizo ni rais na sio waziri au mtu mwingine yeyote. Kama Rais Mwinyi asingeafiki, alikuwa na mamlaka ya kuuvunja mkataba na kumwajibisha aliyesaini, lakini hakufanya hivyo. Vile vile, hata marais waliofuatia na watakaokuja wana mamlaka ya kikatiba ya kuvunja hiyo MoU kama wanaona ilikuwa ni kosa kwa serikali kufanya hivyo, la sivyo wao ndo wanastahili lawama.
Hata mtu anayeilalamikia hiyo MoU kichinichini ana matatizo maana mahakama zipo,nenda mahakamani kama raia wa TZ na upinge hiyo MoU-mbona Mtikila ameweza kwenye suala la mgombea binafsi? Rais wetu pia ni msikivu, peleka kilio chako kwake, kama kuna mantiki utasikilizwa.
Je ni haki ya serikali kufanya hivi kisheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi? Hapa naona Serikali imevunja katiba ya nchi.
Usikimbilie kutumia nguvu kubwa sana kwa kitu kidogo. Hamna sheria iliyokiukwa hapo.
Katika haijavunjwa..labda uonyeshe kifungu kipi cha Katiba.
MM hujaeleweka hapa, kanisa linapendelea kanisa?
Napata shida kuelewa mantiki ya watu wanaolalamikia MoU hii. Mbona hawalalamiki huduma zitolewazo na taasisi hizo kama hospitals?
Vitu viwili tofauti umezungumza. Bilateral agreement ni tofauti kabisa na hii memorandum of understanding ilivyosaigniwa. Hii inazungumzia Serikali ya TZ kuipatia funds Kanisa ktk uendeshaji wake.
Ktk Katiba ya TZ, serikali inatakiwa isiwe ina upendeleo wowote na dini yoyote au taasisi yoyote ya kidini. Sasa huoni kama hii memorandum inavunja katiba ya nchi?
Kanisa ni taasis ya kidini, ambayo itapewa funds kiundeshaji na serikali ya TZ. Sasa Katiba ya nchi inasema serikali isiwe na upendeleo na taasisi yoyote ya kidini. Sasa huoni kama Katiba ya nchi imevunjwa hapo?
Hizo agreement ulizokuwa unasema ni Aga Khan. Aga Khan haitegemei funds kutoka serikali ya TZ ktk uendeshaji wake.