Hata mimi nilitaka kuuliza swali kama hili. Kwani ajabu hapo iko wapi? MoU ni makubaliano kuwa na uelewa wa pamoja kwamba Taasis fulani itatoa huduma fulani katika muktadha fulani na hapa kwa mfano, hizo taasis za "kanisa' zitatoa huduma kufuatana na makubaliano hayo. Serikali nayo imekubali kufanya mambo fulani kama namna ya mashirikiano.Hizo huduma kwani haziwasaidii wenye imani tofauti? Ni lini taasis zenu nyie mnaokereketwa na hii MoU zilikataliwa kusaini MoU na serikali?
Mbona Serikali ina saini MoU n akila taasis inayoshiriki katika kusaidia kufanya kazi au kutoa huduma? Mbona hamuulizi MOU za serikali na UN, Bilaterals kama NORAD, SIDA etc?
Au kwa vile hapa kuna "udini"? Hebu tuache mambo mepesi tujadili issues nzito.Huu udini unakuwa kama ajenda ya siri ya kuleta machafuko hasa ukizingatia wengi wa watanzania bado ni wageni sana wa modalities mbalimbali za namna serikali inavyofaya kazi kushirikiana na taasis zisizo za kiserikali.
Soma vizuri hii MOU ya Kanisa na Serikali ili uielewe vizuri. Hii ni tofauti kabisa na hizo unazosema wewe. Lazima ujue serikali ya TZ NDIYO inayofunds hii MOU na Kanisa.
Kwa mujibu wa Katiba, serikali ilitakiwa isiwe na upendeleo wowote ktk masuala ya dini. Sasa huoni kama Katiba ya nchi imevunjwa?