Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Topical said:
Kwanini vya wakristo vipewe ruzuku? (udini)

Topical,

..kwanini Waislamu nao wamepewa majengo bure waanzishe chuo kikuu? Je huo sio udini?

..kwanini serikali ikajihusisha na suala la kuwasaidia Waislamu waliokwama kwenda Hijja? Je, huo sio udini?

..kwanini serikali inakaa pamoja na Mashekhe kujadiliana kuhusu kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi? Je, huo nao udini?

..kwanini Raisi anawaambia Waislamu waandike MOU yao wampelekee atasaini. Je, huo sio udini?
 
Kwani vyuo vya private, waislamu na hospitali vinatoa huduma kwa watu wa dini gani?

Kwanini vya wakristo vipewe ruzuku? (udini)

Una uhakika kuwa vyuo na hospitali za waislamu hazipewi ruzuku?
 
Hivi vyuo na hizo hospitali zinatoa huduma kwa watu wa dini gani?
Vyuo gani? kinachotazamwa hapa ni serikali kujihusisha na maswala ya dini..Dini zinatakiwa zijiendeshe zenyewe labda kulegezewa sheria tofauti na biashara za watu binafsi..Na hata kama zinapewa msaada na serikali malengo yake zinatakiwa kutoa huduma bure au kiwango kidogo sana ambacho kila mwananchi anaweza kumudu lakini sivyo..Kwa nini serikali inaweka mikataba na taasisi za kidini ikiwa serikali haina dini?, kufikia kuwapa msamaha wa kodi na ruzuku wakati taasisi hizi zinatoza wananchi gharama kubwa kuliko hata za watu binafsi?..

Mwisho ya yote haya inatuonyesha kwamba serikali yetu ina dini na hizi habari za kwamba serikali haina dini ni uzushi na uongo...halafu watu wakisema majibu ati na nyinyi ombeni, alaa limekuwa swala la kuomba kumbe! - Wapagan wataomba wapi na nani atawawakilisha!
 
Mkandara said:
Vyuo gani? kinachotazamwa hapa ni serikali kujihusisha na maswala ya dini..Dini zinatakiwa zijiendeshe zenyewe labda kulegezewa sheria tofauti na biashara za watu binafsi..Na hata kama zinapewa msaada na serikali malengo yake zinatakiwa kutoa huduma bure au kiwango kidogo sana ambacho kila mwananchi anaweza kumudu lakini sivyo..Kwa nini serikali inaweka mikataba na taasisi za kidini, kuwapa msamaha wa kodi na ruzuku wakati taasisi hizi zinazotoza wananchi gharama kubwa kuliko hata za watu binafsi?..

Mkandara,

..kama kuna shirika la dini linatoza gharama kubwa kuliko watu binafsi wakati shirika hilo linapokea ruzuku toka serikalini basi huo tutasema ni ufisadi.
 
Na madrasa zinazojengwa na Aga Khan Development Network nazo "sio za Waislamu ni family business"?

http://www.akdn.org/publications/case_study_zanzibar_education.pdf
Kuna tofauti kubwa baina ya Aghakhan Foundation na AKFED soma vitu uelewe kisha unganisha hoja kulingana. AghaKhan kwa kupitia AKFED walitaka kujiingiza ktk biashara za Utalii na mkataba ukawekwa na Mwinyi ili apate kuingia ktk biashara za Utalii na Mkapa alimwezesha, hivyo mapato ya Utalii hayahusiani na shule kama vile Barricks wanavyojenga shule na zahanati haihusiani na sisi kupinga mkataba wa Barrick.. As a fact, sikubaliani na mkataba wa AKFED..Na AghaKhan Foundation haipewi ruzuku na serikali kuendesha ujenzi wa shule ama zahanati nchini.
 
Vyuo gani? kinachotazamwa hapa ni serikali kujihusisha na maswala ya dini..Dini zinatakiwa zijiendeshe zenyewe labda kulegezewa sheria tofauti na biashara za watu binafsi..Na hata kama zinapewa msaada na serikali malengo yake zinatakiwa kutoa huduma bure au kiwango kidogo sana ambacho kila mwananchi anaweza kumudu lakini sivyo..Kwa nini serikali inaweka mikataba na taasisi za kidini ikiwa serikali haina dini?, kufikia kuwapa msamaha wa kodi na ruzuku wakati taasisi hizi zinatoza wananchi gharama kubwa kuliko hata za watu binafsi?..

Mwisho ya yote haya inatuonyesha kwamba serikali yetu ina dini na hizi habari za kwamba serikali haina dini ni uzushi na uongo...halafu watu wakisema majibu ati na nyinyi ombeni, alaa limekuwa swala la kuomba kumbe! - Wapagan wataomba wapi na nani atawawakilisha!

Mkandara,

Kwa nini Waislamu nao wasiiingie mkataba na serikali ? Afterall, Rais, makamu wa rais, waziri wa fedha wote ni waislamu. Mimi nadhani wakati umefika wa watu kuacha kupiga kelele na kutumia oppurtunity zilizopo. Serikali kutokuwa na dini aimaanishi ya kuwa isishiriki katika kuboresha huduma za jamii. Mimi najua Hospitali nyingi za Misheni zinazotoa huduma sehemu ambako hakuna hospitali za serikali kama Nyangao na Ndanda, sasa unafikiri hospitali hizi zitasurvive vipi bila ya ruzuku? Jua ya kuwa watu wanaoenda kwenye hizi hospitali ni masikini sana.
 
Mkandara,

..kama kuna shirika la dini linatoza gharama kubwa kuliko watu binafsi wakati shirika hilo linapokea ruzuku toka serikalini basi huo tutasema ni ufisadi.
Bila shaka mkuu wangu ni Ufisadi mtupu... shule na zahanati zote za kidini zinazopokea ruzuku hali wakitoza wananchi gharama kubwa ni Ufisadi na naomba sana wakatiwe haraka ikiwezekana.. Na kwa uhakika mkuu wangu swala hili ndio tatizo kubwa liloleta Udini nchini kwa sababu viongozi wa dini wanatazama sasa hivi wanafaidika vipi na misamaha na ruzuku za serikali dhidi ya wengine..
 
..kwanini Waislamu nao wamepewa majengo bure waanzishe chuo kikuu? Je huo sio udini?

"Kwa hili serikali ilikuwa ina fanya cover up ukilinganisha na bil.9 kila mwaka wanayopewa wakristo"
"Pili serikali imetoa majengo ya Mazengo Secondary (my school) kwa wakristo why?
Yaani wakristo wanapendelewa sana aisee halafu waislam wanfanywa kama mazuzu (cover up)
Yana mwisho haya..

..kwanini serikali ikajihusisha na suala la kuwasaidia Waislamu waliokwama kwenda Hijja? Je, huo sio udini?

Kwa hili unasema uwongo mkubwa kila muislam anatakiwa ajitolea nauli ya kwenda hijja, besides hija ni kwa wenyewe uwezo..

Mkuu wa nchi akisaidia ni personal issue siyo goverment arrangement after all how much..danganya toto

..kwanini serikali inakaa pamoja na Mashekhe kujadiliana kuhusu kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi? Je, huo nao udini?

"Hilo ni ndoto mpaka maaskofu wakubali labda baada ya vita...

..kwanini Raisi anawaambia Waislamu waandike MOU yao wampelekee atasaini. Je, huo sio udini

"MoU ilishandikwa wakaikataa kwasababu ya udini na sidhani kama itakujakukubaliwa ..
 
Mkandara,

Kwa nini Waislamu nao wasiiingie mkataba na serikali ? Afterall, Rais, makamu wa rais, waziri wa fedha wote ni waislamu. Mimi nadhani wakati umefika wa watu kuacha kupiga kelele na kutumia oppurtunity zilizopo. Serikali kutokuwa na dini aimaanishi ya kuwa isishiriki katika kuboresha huduma za jamii. Mimi najua Hospitali nyingi za Misheni zinazotoa huduma sehemu ambako hakuna hospitali za serikali kama Nyangao na Ndanda, sasa unafikiri hospitali hizi zitasurvive vipi bila ya ruzuku? Jua ya kuwa watu wanaoenda kwenye hizi hospitali ni masikini sana.
Sasa unacho suggest ni kupingana na katiba. Serikali yetu haina dini kwa nini tubadilishe na kuwa kila dini inaweza kuomba misaada kwa sababu rais. makamu na mawaziri ni waislaam?.. Je wakiiingia Wakristu iwe kwa zamu au sio.

Katiba inasema wazi kwamba nchi yetu haina dini na kwa kutumia sheria hii ndio maana serikali imekataa swala la Mahakama ya kadhi kwa nini majibu hayo hayo yasitumiwe pale madhehebu ya dini yanapoomba?..Na kama kweli ukiomba utapewa mbona hilo la OIC na mahakama ya kadhi limekataliwa au lazima ombi lenyewe lifanane la wakristu? Je, hao Wapagan nani atawawakilisha?... Huu ni ushenzi ulofanywa na Mwinyi, Mkapa na JK hawa viongozi wote wamekiuka katiba yetu.

Sawa hizo shule na hospital za dini zitoe huduma lakini kwa nini wapewe fedha na serikali as if ni wizara au idara ya serikali?.. wao hukusanya michango ya watu kama JK atatoa yeye toka mfukoni mwake haikatazwi lakini sio kuchota fedha za wananchi kila mwaka kuwezesha kanisa au msikiti kujenga shule hii inajenga Udini - Wao (serikali) wanashindwa nini kujenga shule na hospital maeneo hayo!
 
Bila shaka mkuu wangu ni Ufisadi mtupu... shule na zahanati zote za kidini zinazopokea ruzuku hali wakitoza wananchi gharama kubwa ni Ufisadi na naomba sana wakatiwe haraka ikiwezekana.. Na kwa uhakika mkuu wangu swala hili ndio tatizo kubwa liloleta Udini nchini kwa sababu viongozi wa dini wanatazama sasa hivi wanafaidika vipi na misamaha na ruzuku za serikali dhidi ya wengine..

Nenda muheza DDH linginisha diagnosis fee na fee ya kumwona doctor, na hospitali ya serikali ujue uwizi wa kanisa pamoja na ruzuku..

You know what? ruzuku tunayopeleka DDH-muheza inatosha kujenga hospitali nzuri ya serikali ya hadhi ya wilaya..

Kwanini hawafanyi hivyo ...udini udini udini ukristo..
 
Topical said:
Pili serikali imetoa majengo ya Mazengo Secondary (my school) kwa wakristo why

Topical,

..unanishangaza!!

..yaani umesoma Mazengo Sec, halafu hufahamu kwamba ilikuwa shule ya Kanisa kabla Nyerere hajaitaifisha?!!

..sasa basi kuwa na shukurani kidogo kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwasababu bila uamuzi wake wa kutaifisha iliyokuwa Alliance sec, wewe usingepata nafasi ya kusoma Mazengo Sec.

..Mazengo imerudishwa kwa wamiliki wake wa awali, Kanisa la Anglican.
 
Mkuu acha utani ..

Kwanini serikali kama siyo ya kidini isirudishe shule za kiislamu hata moja? kwanini za wakristo tu zirudishwe?
 
Mkandara,

..tumeona kwamba mwanzo kulikuwa na MOU kati ya serikali na Agha Khan, ambao ni Ismailia.

..halafu ikaja MOU kati ya serikali na makanisa ya Kikristo, namely Anglican,Catholic,Lutheran.

..mwisho, Muslim Trust Fund nao wakapewa majengo kwa ajili ya chuo kikuu, hapoo napo lazima kulikuwa na mkataba/mou.

..sasa katika mtiririko huo, serikali ina dini gani? Je, ni Ismailia, Kristo, au Islam???

Hebu tupatieni basi gharama za MoU ya Aga Khan and Serikali. Halafu gharama za Chuo cha Morogoro. Halafu tulinganishe na Tshs Trilioni 2 mnazoiba serikalini tuyazungumze kwa ufasaha. Maswali ya msingi hamjibu. Bilioni 91 za nini? Je mbona private hospitals and schools survives bila ya misaada ya serikali? Mbona tunalipia gharama za matibabu na shule kwa bei mbaya ijapokuwa tunawapa Bilioni 91 kila mwaka? What is financial performance of each and every institution ya kanisa tuzifanyie tathmini kujiridhisha maana tunawapa hela zetu? Hamjibu maswali ya msingi badala yake mnajitahidi kupoteza lengo la thread hii. Watu wagumu kuelewa nyie ndio sababu narudi UFISADI NCHI HII HAUTAISHA KAMWE kwani unaanzia huko huko makanisani mwenu!!!!
 
Mkandara,

..tumeona kwamba mwanzo kulikuwa na MOU kati ya serikali na Agha Khan, ambao ni Ismailia.

..halafu ikaja MOU kati ya serikali na makanisa ya Kikristo, namely Anglican,Catholic,Lutheran.

..mwisho, Muslim Trust Fund nao wakapewa majengo kwa ajili ya chuo kikuu, hapoo napo lazima kulikuwa na mkataba/mou.

..sasa katika mtiririko huo, serikali ina dini gani? Je, ni Ismailia, Kristo, au Islam???
Ningependa kwanza kutofautisha MoU na Accord of Cooperation kwa sababu makubaliano yake ni tofauti kabisa. Kisha mali za Aghakhan ni mali zake yeye tofauti na kanisa ambapo mali sii ya Pope na serikali bado inaweza kutaifisha mali za Aghakhan..He makes the call..

Pili, serikali inaposema haina dini ina maana haiwezi kujihusisha na maswala ya dini isipokuwa inawawezesha kisera kufanya ibada zao. Unapoanza kuwapa Aghakhan, kanisa au Muslam fund toka serikalini ndiko kunakojenga Udini kwa sababu nina hakika hapa wapo watu wengi wana question kwa nini Muslim Trust fund wamepewa majengo yale na hawapendezewi, hivyo kesho watataka kuona dhehebu au dini zao pia wakipewa majengo kama hayo.. Ni kile kile mnachokikataa kuhusiana na mahakama ya kadhi mkisema kama waislaam wakipewa Je, Wakristu nao waombe? kisha watafuata baniani, na madhebu mengineyo jambo ambalo liaondoa nguvu ya sheria na katiba yetu..

Mimi sipo hapa kupendekeza Waislaam nao wapewe hiki ama kile laa hasha!, napinga vyombo vyote vya dini kupewa ruzuku, kodi za wananachi wakati taasisi hizi zinakusanya mabillioni ya fedha toka kwa wafadhili ili kutoa huduma hizi bure. Napinga hadi NGOs zilizopo nchini ambazo zinapokea mabillioni ya michango ya watu kusaidia watoto wa Afrika lakini asilimia 80 ya pato huishia ktk mishahara na matumizi ya NGOs hawa pia hawatakiwi kupewa afueni ya kodi isipokuwa kwa masharti..mbona Aghakhan anaendesha shughuli zake bila kupewa ruzuku na anaweza kukusanaya fedha na kupanga shughuli zake kwa kutegemea michango na mapato ya shughuli zake. wengine wanashindwa kipi?

Serikali inatakiwa itambue na kuwawezesha madhehebu yote ya dini (Kisera) kuweza kuendesha shughuli zao ktk ujenzi wa imani za wananchi na sii kuwa sehemu ya matumizi ya serikali ama wajibu wa serikali kuwapa vitu hivi. Kama kuna majengo City plan lazima itatenga maeneo kwa ajili ya misikiti na makanisa, shule na zahanati hii ndio kazi pekee wanayotakiwa kuifanya lakini sio kugawa ardhi bila hata kupimwa tena nyingine wananyang'anywa watu ili kusimamisha kanisa au msikiti..

Serikali ina dini gani? well itategemea na kiongozi aliyepo madarakani yeye atapendelea kipi ili apate kuchaguliwa tena na kupata support ya wananchi wa dhehebu hilo.
 
Ningependa kwanza kutofautisha MoU na Accord of Cooperation kwa sababu makubaliano yake ni tofauti kabisa. Kisha mali za Aghakhan ni mali zake yeye tofauti na kanisa ambapo mali sii ya Pope na serikali bado inaweza kutaifisha mali za Aghakhan..He makes the call..

Pili, serikali inaposema haina dini ina maana haiwezi kujihusisha na maswala ya dini isipokuwa inawawezesha kisera kufanya ibada zao. Unapoanza kuwapa Aghakhan, kanisa au Islam fund toka serikalini ndiko kunakojenga Udini kwa sababu nina hakika hapa wapo watu wana question kwa nini Muslim Tryst fund wamepewa majengo yale na hawapendezewi, hivyo kesho wattaka kuona dhehebu au dini yake wakipewa pia majengo hayo.. Ni kile kile mnachokikataa kuhusiana na mahakama ya kadhi mkisema kama waislaam wakipewa Je, Wakristu nao waombe? kisha watafuata baniani, na madhebu mengineyo jambo ambalo liaondoa nguvu ya sheria na katiba yetu..

Mimi sipo hapa kupendekeza Waislaam nao wapewe hiki ama kile laa hasha!, napinga vyombo vyote vya dini kupewa ruzuku, kodi za wananachi wakati taasisi hizi zinakusanya mabillioni ya fedha toka kwa wafadhili ili kutoa huduma hizi bure. Napinga hadi NGOs zilizopo nchini ambazo zinapokea mabillioni ya michango ya watu kusaidia watoto wa Afrika lakini asilimia 80 ya pato huishia ktk mishahara na matumizi ya NGOs hawa pia hawatakiwi kupewa afueni ya kodi isipokuwa kwa masharti..

Serikali inatakiwa itambue na kuwawezesha madhehebu ya dini kuweza kuendesha shughuli zao ktk ujenzi wa imani za wananchi na sii kuwa sehemu ya matumizi ya serikali ama wajibu wa serikali kuwapa vitu hivi. Kama kuna majengo City plan lazima itatenga maeneo kwa ajili ya misikiti na makanisa, shule na zahanati hii ndio kazi pekee wanayotakiwa kuifanya lakini sio kugawa ardhi bila hata kupimwa tena nyingine wananyang'anywa watu ili kusimamisha kanisa au msikiti..

Huu pia ni msimamo wangu...

Hakuna haja ya hela ya serikali (hat shilingi) kwenda kanisani au msikitini period..

Serikali inaweza kutumia ruzuku ilizotoa kwenda kanisani (Bil.9) kuboresha shule zake za kata na hata dispensary zake..

Kanisa waendeshe miradi yao pekee..mbona waislamu tunaendesha shule na hospitali zetu bila ruzuku

Wakristo wanaendekeza sana udini kwenye hili utashangaa sana..

Tukisema wakristo wana udini udini udini hundred times waislamu watu watabisha..
 
Unajua Mkandara,

Mie ni mfuasi wa kiliberali yaani naamini katika siasa za usawa na haki. Sipendelei jamii moja iwe juu ya nyengine. Watanzania wanaona sawa serikali ipendelee Makanisa lakini Waislamu wakipewa kitu inakuwa nongwa. Taasisi zikiongozwa na mwislamu zinaonekana zina udini lakini zikiongozwa na mkristo ziko makini. Watu wakikosa kazi katika taasisi fulani wanadai wamebaguliwa (mfano Bakhressa). Jamani sisi ni watanzania na tunatakiwa tuwe watanzania kwanza halafu dini zetu.

Tunautaka uzalendo na utaifa lakini huku udini unatumaliza. Memorandum taasisi za kidini zinapewa Bilioni 91 lakini taasisi zengine hazipewi! Mnalinganisha organisation ya mtu binafsi wakati serikalini kuna upendeleo unaonekana wa wazi kabisa. Tutaendelea kweli??? Binafsi yangu ningelipendelea this business ya MoU baina ya serikali and taasisi za kidini to come to an end. First of all kwasababu inachochea vuguvugu na pia it is unfair. Failures of the government to fail to provide medical services does not justify favoritism to certain institutions. Vile vile kama serikali yetu ni makini pesa zilizopelekwa huko zirudishwe maana ndani ya zile pesa zimo pesa za watu ambao either hawafaidiki na huduma hizo au hawana kabisa uhusiano nao mfano waislamu. Tuishi katika jamii ya uwazi, ukweli bila ya upendeleo fulani. Tukiweza kufika hapo tutapiga hatua kubwa sio hivi sasa.
 
Wakristo wamezoea kupendelewa na serikali zote..hawawezi ku-survive bila msaada wa serikali period..

Kabal ya uhuru serikali ya kikoloni ilikuwa inajenga makanisa na kusomesha wakristo..understandable though..kwasababu ni wakoloni

Baada ya uhuru wanapendelewa through kuna mtu amenidokeza serikali kuwa wakati wa nyerere walikuwa wanachotea bila MoU na Maaskofu walizoea hivyo..sasa ilipofika zamu ya Mzee mwinyi walipokuja kuchukua mzee akashangaa..akawashauri waweke utaratibu..ndio ikazaliwa MoU uwizi mtupu..

Mbona sisi waislamu tunaendesha shule zetu na hospitali bila ruzuku na zinatoa huduma kwa wananchi wote??
 
Jamani JK si alisema SIKU IDD pale msikiti wa marehemu Gaddafi Dodoma. Kukibwa dini zingine zijpange. Waanzishe mashule na mahospitali ili watoe huduma, BAKWATA kama bakwata ni taasisi ndogo sana. Msikiti au mkoa uwe na hospitali au huko vijijini ambako wanamatatizo ya huduma ya afya. Sisi kama watz wacha mungu tukatoe huduma huko bila kubagua. Ila siku moja samahani kama nitakuwa nimekosea. Shehe alikuwa anatoa mhadhara kwenye TV moja iko Mwanza kwenye Barmedas Cable namnukuu Waislamu tujenge hospitali zetu na sisi ili tukatibiwe kiislamu maana yake waislamu wakienda kutibiwa kwenye hospitali za Kikristo wanadhalilishwa na Wakiristo. Mama wa akiislamu akienda kujifungua na akamkuta Dr Mkiridto akamuchoma kidole ili kuangalia kama njia itaweza kupitisha mtoto huko ni kumdhalilisha Mwislamu.

Mimi binafsi nilibaki mdomo wazi kama Dk 5, Nikajiuliza je hakuna wakiristo wanaojifungulia Regency, TMJ, Agakhan mbona madaktari wenge Waislamu. Je haya wanayohubiri waislamu kwenye TV na mihadhara pale manseze wangehubiri kujenga vituo vya afya na mashule ingesaidia sana kuliko kutoa maneno mabaya kwa wakiristo hayatawasaidia bali wanazidi kujiua kisaikolojia.
 
Huu pia ni msimamo wangu...

Hakuna haja ya hela ya serikali (hat shilingi) kwenda kanisani au msikitini period..

Serikali inaweza kutumia ruzuku ilizotoa kwenda kanisani (Bil.9) kuboresha shule zake za kata na hata dispensary zake..

Kanisa waendeshe miradi yao pekee..mbona waislamu tunaendesha shule na hospitali zetu bila ruzuku

Wakristo wanaendekeza sana udini kwenye hili utashangaa sana..

Tukisema wakristo wana udini udini udini hundred times waislamu watu watabisha..
Na hii ndio sababu kanisa na misikiti wamekuwa sehemu kubwa sana ya uchaguzi wa mwaka 2005, kwa sababu kila mmoja wao alikuwa aki lobby ili kumpata kiongozi ambaye atakuwa upande wake, Na JK aliweza kucheza karata kama zilivyolazwa.. Wananchi wote tukasahauliwa isipokuwa tukajigawa kwa imani zetu za dini..Hii ni athari ya kuua Azimio la Arusha kuhusiana na utaifishaji.
 
Back
Top Bottom