Hapa mkuu wangu tuko pamoja sana kwa sababu swali hili linatakiwa kuchunguzwa kwma tulivyofanya Richmond na ilipelekea kujiuzulu kwa Lowassa na ikiwa na maana pande zote mbili zilizoshiriki zinahusika na mpango huu.
Kuhusu Mwinyi hakika naelewa vizuri sana kwamba anafahamu alichokifanya na hakujali kama Nyerere ambaye alikuwa mkristu na bado alitaifisha shule za kikristu tofauti zao ni for whose interest!..Tofauti na waislaam wengine mimi Mwinyi simpendi na simpendi na sintampenda kwa lolote la uongozi zaidi ya kumpa heshima zake kama rais wangu wa pili..
Kinachonishangaza sana ni mapenzi ya Wadanganyika. hHuko nyuma nimetoa mfano mdogo sana kwamba huwezi kumpenda Nyerere ukamchukia Ghadaff na wala huwezi kumpenda Ghadaff ukamchukia Nyerere kwa sababu hawa wote walikuwa na sifa moja kubwa ya uongozi na mapungufu yao yanafanana sana tu. Na kama mtu anataka kujua ana Udini ndani yake basi lazima atakuwa na mtazamo tofauti kwa watu hawa na nakuhakikishia dini yake lazima iwe sawa na yule alompenda akamchukia mwingine...
Mfumokristu umerudishwa na Mwinyi sio Nyerere, na tunaweza kesha hapa kubishana kwa sababu tutarudi ktk fikra zile zile za udini maanake hakuna Muislaam anayetaka kumlaumu Mwinyi ambaye alipiga Vita Balukta kwa nguvu zote akitetea Bakwata chombo wanachokitumia sana ktk kuwapoza waislaam kisiasa. Kayafanya mengi mabaya kwa Jumuiya ya wiaslaam na Watanzania kuliko kiongozi yeyote..Waislaam kwa Wakristu wote are into denial hawataki kuamini kwamba CCM ndiye mtunzi wa mfumo na uendeshaji wa siasa za Tanzania. Kama wanaweza ku ammend Katiba, sheria, kuweka mikataba na miafaka kwa matakwa yao. Tazama nguvu ya rais, bunge lao hawajawahi kuwa na chini ya 2/3 ya uwakilishi lakini bado utaona mapenzi ya watu yapo kwa CCM, chombo kinachoendelea kuwadhalilisha mwaka hadi mwaka..
Lakini tusipoteze matumaini mwaka 2015 inawezekana kuwa mwaka ambao utaleta mabadiliko kwa sababu wananchi wamechoka na Ufisadi wa chama hiki. Hayo matumizi ya TCRA na huko Mtwara ni sehemu ndogo sana ya ubadhilifu unaofanyika nchini, kifupi nikwambie la kunuka halina ubani - serikali, bunge, mahakama (mihimili yetu) inanuka! mashirika yote ya Umma ni Ufisadi kwa kwenda mbele na viongozi wote ni matajiri wa kutisha. Ubepari unakwenda sambamba na Ufisadi kama vile biashara na faida!
Hivyo, sisi maskini kukubali Ubepari ina maana tumekubali Ufisadi na sasa taratibu dawa inaanza kuingia ktk mishipa ya damu zetu. Hakika Nyerere akirudi leo, atacheka sana na kutwambia Yakowapi? niliwaambia hamkutaka kunisikia! na nadhani kujuzulu kwake kulitokana na kutokubali kubatizwa kama bepari maana aliwahi kusema hawezi kugeuka kutazama nyuma akageuka jiwe!..Na baada ya hapo - He did what he did just to prove us wrong ktk sisi kuchagua Ubepari, bahati mbaya hataweza kushuhudia haya..