Kwa vile rais na pm kipindi hiki ni muislam mwenzetu, tumieni fursa hii muwashinikize watumie mamlaka yao kufuta hiyo MoU. Ninachojua pale Bugando na kcmc serikali imeweka watumishi wake, imewekeza vifaatiba na madawa. Serikali iondoe kila kilicho chalke. Then hawa watu wa makanisa watakachofanya ni ku-scale down huduma wanazotoa, zilingane na uwezo wao. Swali je serikali sasa hivi iko tayari kutoa huduma za kibingwa zinazotolewa na hospitali hizi za makanisa? Kama iko tayari, well and good.
Ndugu zangu waislam (baadhi), msifikiri kwamba hudama/maendeleo yanayofanywa na sisi wakristo pesa zinatoka serikalini. Sisi kwa mfano parokiani kwetu sadaka kila jumapili tunatoa kati ya 4m mpaka 5m. Tumeweza kwa kipindi kujenga kanisa zuri, nyumba ya Mapadre, na sasa tuko kwny mchakato wa kujenga ukumbi, zahanati na shule ya chekechea. Parokia zingine wana miradi ya kilimo ufugaji kuku, ng'ombe, mbuzikatoliki etc. Miradi yote hii inaingiza pesa inayosadia kufanya maendeleo zaidi.
Pia mnapotoshana kwamba wakristo wanapitisha mizigi bandarini bila kulipa ushuru. Hili mbona liko wazi? Je bandari inasimamiwa na makanisa? Tra inasimamiwa na makanisa?. Kama kuna msamaha wa kodi kwaajili ya mizigo ya mashirika ya dini, hiyo ni kwa dini zote. Agizeni na nyie mizigo, pitieni utaratibu wa kawaida kupata msamaha wa kodi, muendelee na mambo yenu.
Sasa hili swala la bandari linataka kutugawa. Mimi naona uelewa ni mdogo kwa baadhi yetu.
Mimi kwakweli sina shida na muwekezaji yeyote, ilimradi uwekezaji huo uwe kwa maslahi mapana ya taifa letu kwa sasa na vizazi vyetu hapo baadae. Mkataba huu wa Dpw, ambao 1) hauna ukomo, 2) unampa muwekezaji bandari zote za bahari na maziwa yote, pamoja na miundombinu ya usafiri na anga 3) una masharti kwamba hauwezi kuvunjwa ktk mazingira yoyote, 4) haubainishi mgawano wa mapato; mkataba huu ni wa ovyo kabisa. Ni mwehu atakaye toa rasilimali zake kwa namna hii.
Pia tuangalie namna muwekezaji alivyo patikana. 1) Waziri Mbarawa: Tulishindanisha makampuni 8 toka nchi tofauti, then tukamchagu Dpw. Huu ni uwongo- tenda ilitangazwa lini na wapi, tenda ilfunguliwa lini na wapi? 2) Pm Majaliwa: Rais alipoenda Dubai (kwenye expo2022?), tukampata Dpw. Unaweza kuona viongozi hawa wanavyotofautiana.
Nguvu kubwa inayotumika kumpinga, sawa na kumtetea muwekezaji huyu. Kwa vile suala hili tayari limetugawa, kwanini tusiachane na Dpw tukatafuta muwekezaji mwingine? Wawekezaji wenye sifa wako wengi. Ila kuna harufu ya rushwa hapa ambayo imeshaliwa, itarudishwaje?