Habari za asubuhi wandugu,
Nilivoona heading nimeshawishika kuufungua uzi huu ili nionekilichomo na kuchangia pale ikibidi. Nimeona, kama ambavyo wenzangu mmeona, kilichomo ndani ya MoU ambayo kimsingi imewekwa katika mlengo ambao haupo kwenye mizania. Wengi wamemfahamisha mleta mada kuwa angekua amefanya justice kama document yote ingeletwa humu.
Mawazo yangu juu ya hili ni kama ifuatavyo;
MoU ilisainiwa 1992, commander in chief wa wakati huo alikua Ali Hassan Mwinyi. Wote mnafahamu imani yake na ukweli kwamba nchi haina dini. Nimeanza hivi ilikuonesha kuwa hata mkuu wa nchi alijiridhisha mantiki ya ombi la TEC na CCT kuwa hapakuwa na nia ovu katika kuomba mashirikiano haya. Kwanza aina ya huduma ni za kijamii hususan elimu na afya (consumption of social services the principle of non-exclusivity holds). Maana yake ni kwamba hamna namna ya kumzuia mtu ku-access huduma ya kijamii kwa msingi mwingine wowote ule nje ya utu na haki ya mtu kuishi.
Naomba nimuulize mleta mada hivi katika taasisi za afya madhalani, kanisa liliomba waiver ya kodi na kusaidiwa wataalam na mishahara ikibidi. Kwa kuwa huduma zinatolewa kwa misingi ya utu na haki ya kuishi, si kwa imani zao, naona MoU haikua na tatizo ikiwa unalitazama jambo hili objectively. Ninavyofaham kuna combination ya waajiriwa wa taasisi husika na waajiriwa wa Wizara ya Afya. Ivi kunaushahidi wowote kuwa ajira chini ya Wizara ya Afya zipo ktk misingi ya kidini? hapana binafsi siamini na sina ushahidi. Ukienda Bugando, KCMC, Mbeya Referal Hospital nk hutakuta watumishi wa imani moja lakini hizi taasisi ni za madhehebu ya kidini hii inaonyesha kuwa hizi fikra mfu na incitement zinazojaribu kujengwa ni watu wenye akili ndogo tu ndo wanaweza kuafiki hoja ambazo hazina mashiko. Pia fanyeni utafiti kwny registers za haya mahospitali wagonjwa wanaotibiwa kama majina yao ni ya dini fulani pekee ama vinginevyo! Na kama utafiti utadhihirisha beyond reasonable doubt kwamba huduma zinatolea kibaguzi then hoja itakua na mashika. Utafiti huu hauhitaji PhD hata asiye jua kusoma na kuandika ila akawa anajua majina ya dini zetu atakuja na genuine findings katika hili.
Pia najiuliza ivi watu wa imani zingine hawakuwepo na kama walikuwepo hawakusikia hata tetesi ya kilichokuwa kinaendelea ktk maombi ya CCT + TEC kuhusu MoU? Je, mtazamo wa watu wa imani zingine bila kusahau wapagani walilionaje jambo hili kwa wakati huo? Je, ni kweli kwamba MoU iliratibiwa chini ya Carpet? Je, tangu wakati huo wanufaika ni kundi fulani la kiimani? Je, mtu wa imani nyingine ukienda kutibiwa treatment ni tofauti? Ukiwa katika taasisi hizo unalazimishwa kufuata imani ya kikristo? Nadhani ukifanya uchambuzi wa dodoso langu utakuja kugundua kuwa mada hizi zinaanzishwa si kwa nia njema. Maana unavoleta mada jaribu kufanya japo utafiti mdogo ili hoja iwe na uzito zaidi.
Mimi ni mkristo, siandiki haya kwa kuzingatia imani yangu ila najaribu kutazama objectively. Nimesoma shule iliyokuwa na mchanganyiko wa imani tumesoma vizuri, tulikua na group discussions based on our programs na sio imani, nimarafiki zangu wa karibu kabisa ila ni waimani tofauti na yangu lakini ni marafiki si wakinafiki. Nashangaa leo kila jambo tunataka kulipa mlengo aidha wa ukristo ama uislam. Napenda niwakumbushe Watanzania wenzangu kuna jambo tunalisahau kuwa nchi hii hakuna imani mbili pekee, ukristo na uislam. Kwa mfano mimi ni mkristo kwa kuwa nimezaliwa ktk imani/familia hiyo, wewe ni muislam kwa kuwa umezaliwa ktk familia/imani ya kiislam. Wengine wanamajina ya kikristo lakini si waumini wa ukristo ama ya kiislam lakini sio waumini wa uislam. Tunawaweka wapi watu hawa ktk mijadala yetu. Na wanahaki ya kuishi, kuheshimiwa, kuto bughudhiwa wala kudharauliwa kwa kuwa hawana ufuasi wa wa dini tunazozijua.
Kwa mfano, tunawaganga wa jadi (kienyeji) wenye majina yanayoshabihiyana na imani zetu lkn shughuli zao ni tofauti na mafundisho ya imani zetu. Ikumbukwe mganga wa jadi amesajiliwa na mamlaka za nchi hii. Hawa tunawaweka wapi kwenye huu ujinga tunaoukuza bila sababu. Utulivu wa nchi hii unatakiwa uwe chachu ya maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla na si vinginevyo. Naamini lengo la dini ni kudumisha amani na upendo na si vinginevyo. Sitaki kuamini kama dini zinamaanisha chuki, uadui, fujo na aina nyingine za fujo. Tumekua wandugu tudumishe udugu wetu. Na kwa wale waliochoka utulivu wakae kimya kwa faida ya tuliowengi!
GT,
Mkuu ndio hapo naposema kila siku watu wanakataa OIC bila kujua wala kufikiria kwa sababu tu kuna jina la Uislaam lakini ni serikali hiyo hiyo imeweka mikataba kibao na Taasisi za Kikristu kwa kutumia jina la Vatican ambayo ni Taasisi ya kidini vile vile.
Fundi Mchundo,
Mkuu unakataa hili kwa sababu kiingereza kilichotumika ni kibovu au?..Hivi katika akili yako unafikiri watu hawafdahamu mikataba ambayo serikali imekwisha ingia na taasisi za kidini?..Au kwa sababu hazitangazwi isipokuwa inapofikia za Kiislaam basi kila mtu hupiga kelele hata mwenye kulala huamka..Mkuu hatusemi tuu na mjue kwamba Waislaam ni watulivu sana kiasi kwamba ingekuwa maswala mengi yametokea upande wa pili sidhani kama nchi ingekalika..