sasa hii memorandum naona imejikita zaidi katika provision of elimu na afya, sasa maafa yake kwa uislamu ni nini? kwamba hizo shule na hospitali na za wakristo pekee yake au? maana kama kule peramiho ile hospitali ni ya wote na inatoa huduma kuliko hospitali za serikali, ukienda Njombe utakuta hospitali za walutheri etc, na sasa hivi Pengo alikuwa anajenga shule Rufiji je hizi zote ni juhudi za kuwaonea Waislamu? Bagamoyo kuna shule ya Marion Girl's na kuna watoto wa wakubwa wengi tu wanasomo huko na ni waislamu, je aliye iweka au kuwaruhusu waislamu kusoma huko kafanya kosa? Nakuomba ndugu yangu pale penye kitu kizuri tukiseme kibaya tukiseme, tusije panda hii mbegu ya ubaguzi haito tupeleka kokote.
Kwa Mfano kuna watu wazuri tu na ni waislamu mimi nina waheshimu na kuwapenda kwa matendo yao eg Marehemu Prof Harub, kuna Prof Shivji, na kuna wakristu wabaya wabaya kweli kweli na mimi ninawapinga kwa matendo yao kama Raisi Mstaaafu BWM na wengineyo wenye matendo kama yake.