Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Geeque,

..ingekuwa vizuri kama ungesoma maelezo ya Dr.Slaa. yeye alihusika na suala hili wakati akiwa katibu wa TEC.

..kwa kifupi mazungumzo kati ya Kanisa na serikali yalianza 1986, halafu hii MOU ilisainiwa miaka ya 90 wakati Lowassa ni waziri ktk Ofisi ya waziri mkuu.

..sasa tangu wakati huo mpaka leo kama Bakwata wangekuwa na nia ya kusaini MOU ya aina yoyote na serikali binafsi naamini wangepewa nafasi hiyo.

..vilevile serikali ya Mkapa walitoa majengo ya Tanesco kuwa Chuo Kikuu cha Waislamu. sasa mali kama zile, na ukizingatia kwamba zilikuwa za Tanesco, hazihamishwi bila mkataba unaotambulika kisheria.

..sidhani kama serikali ikiamua kufanya jambo fulani na Waislamu basi lazima ifanye jambo hilohilo kwa Wakristo. tukiwa na mawazo kama hayo ndiyo mwanzo wa frustration zisizokwisha.
Mie nadhani serikali inavofanya vitu kwa maslahi ya wananchi wake hakuna haja ya kuficha. Mf serikali ilitoa chuo cha benki Amoni Senkela kwa wakristo na pia ikatoa TANESCO kwa waislam. Vivyo ukitaka kuingia mkataba na kundi fulani ili kuwe na fairness lazima makundi mengine yajulishwe. Mf Walitaka uwepo wa mahakama ya kadhi na OIC ilibidi wawaconsult woote na ndio maana imeshindikana. Ingekuwa ni mikataba na kundi moja bila jingine kujua kwa vyovyote vile sasa hivi waislam wangekuwa na OIC na mahakama ya kadhi. Unajua haya mambo yanavyojitokeza yanawaongezea mashaka waislam kuwa huenda malalamiko yao juu ya serikali yanaukweli fulani. Hali hii itaisha tu kama kutakuwa na uwazi. Huwezi kusaidia kundi fulani kupata wataalam, Walimu na fedha wakati kundi lingine halipewi. Wanaweza wakajenga hoja kuwa hata kufanikiwa kwa shule za wakristo kutanokana na msaada wa serikali. Honestly huu ni uchafu mwingine wa Serikali
 
bnhai said:

bnhai,

..hilo la uwazi nakubaliana na wewe 100%.

..nilichojaribu kusema mimi ni kwamba kama Waislamu wanahitaji msaada wa majengo na vifaa basi serikali iwasaidie. kama Wakristo wenyewe wanahitaji utaalamu na siyo majengo basi wasaidiwe utaalamu. and vice versa.

..tusijenge mazingira kama ya ugomvi wa watoto wadogo kwamba serikali ikisaidia majengo kwa taasisi ya Kiislamu, basi Wakristo nao lazima wasaidiwe majengo. mwisho tutadai hata majengo hayo yafanane rangi.
 
Geeque,

..ingekuwa vizuri kama ungesoma maelezo ya Dr.Slaa. yeye alihusika na suala hili wakati akiwa katibu wa TEC.

..kwa kifupi mazungumzo kati ya Kanisa na serikali yalianza 1986, halafu hii MOU ilisainiwa miaka ya 90 wakati Lowassa ni waziri ktk Ofisi ya waziri mkuu.

..sasa tangu wakati huo mpaka leo kama Bakwata wangekuwa na nia ya kusaini MOU ya aina yoyote na serikali binafsi naamini wangepewa nafasi hiyo.

..vilevile serikali ya Mkapa walitoa majengo ya Tanesco kuwa Chuo Kikuu cha Waislamu. sasa mali kama zile, na ukizingatia kwamba zilikuwa za Tanesco, hazihamishwi bila mkataba unaotambulika kisheria.

..sidhani kama serikali ikiamua kufanya jambo fulani na Waislamu basi lazima ifanye jambo hilohilo kwa Wakristo. tukiwa na mawazo kama hayo ndiyo mwanzo wa frustration zisizokwisha.

Serikali ilikataa kusaini MOU ya waislam,ndio maana MUFTI kwenye mkutano wake wa MYK alisema kuwa nchi hii inamilikiwa na wakristu kila kitu wanapata akiwa na maana ya huu mkataba mchafu wenye ubaguzi,ilipositishwa misamaha ya kodi ambako ndio wakristu wanatanua na misamaha hiyo.walipoambiwa serikali warudishe misamaha walirudisha haraka sana.hivi sasa kila MKRISTU ANASAJILI KANISA LAKE ILI WAKWEPE KODI.

waislam walipeleka MOU wakati wa MKAPA lakini hadi leo hawajjibiwa.
Joka kuu kuna shule nyingi za waislam zimetaifishwa kama Tambaza,ZANAKI,AZANIA,JANGWANI,shule ya msingi mnazi mmoja na lumumba bila kusahau AMANA primary school,MWEMBETOGWA KULE IRINGA.

kwenye kutaifisha waislam ndio wameathirika sana majumba yote ya posta,mnazi mmoja,kisutu,upanga yalikuwa mali ya waislam kila mji majumba mazuri yalikuwa mali za waislam Nyerere akataifisha kwa chuki za udini.

mkapa hakutoa chuo cha Morogoro kwa moyo mweupe,alitoa ili kujisafisha na mauaji ya bila hatia ya mwembechai na Pemba kwa chuki zake kwa waislam,
baada ya kuwaua waislam bila hatia,huku akiwa kajilimbikizia mali nyingi kwa dili zake chafu kuanzia EPA,KIWIRA,KAGERA SUGAR akaona atakuwa hana cha kusema mbele ya watanzania na waislam, kote ananuka akaona atoe chuo kama njia ya kujisafisha.

Slaa kama alikuwa mpenda haki angesema jamani wakati tunaanda hii MOU walikuwepo waislam mbona leo kwenye kusaini hawapo?

walitumiwa waislam mwanzoni ili kumdanganya mzee Mwinyi kuwa dini zote ziko huko mbeleni LOWASSA AKASAINI na jamaa zake wa kanisa.

watu hawa hawa mnalalamika kuwa waislam wasiwe na mahakama ya Kadhi KWA PESA ZA taifa, tukisema tujiunge na OIC ili tutumie pesa za waislam hamtaki.
kwa kweli ndugu zetu hambebeki na mnazidi kutujengea chuki kwa kutuwekea mamikataba kama hii inayowanufaisha nyinyi tu. mnafiki mbunge LAZARO tunaomba kauli yako juu ya MOU ya kanisa na serikali?
 
Ha ha ha ha, kwani umekatazwa kusajili misikiti yako nawe ukwepe kodi? au unataka kusema kuwa serikali imekatazwa waislam kusajili misikiti?!

waislam walipeleka MOU wakati wa MKAPA lakini hadi leo hawajjibiwa.
Joka kuu kuna shule nyingi za waislam zimetaifishwa kama Tambaza,ZANAKI,AZANIA,JANGWANI,shule ya msingi mnazi mmoja na lumumba bila kusahau AMANA primary school,MWEMBETOGWA KULE IRINGA.

Unaengelea Mkapa aliyewapatia waislam chuo cha Tanesco?

Kwa nini wasipeleke MoU yao sasa hivi kwa raisi mwislam na viongozi wa ccm ambao wengi ni waislam ili wakubaliwe. Shule za waislam zilizotaifishwa ni kiduchu ukilinganisha shule za wakristo zilizotaifishwa. Nimekupa proposal moja kuwa shule na hospitali zote zirudi kwenye dini bado unakwepakwepa.

kwenye kutaifisha waislam ndio wameathirika sana majumba yote ya posta,mnazi mmoja,kisutu,upanga yalikuwa mali ya waislam kila mji majumba mazuri yalikuwa mali za waislam Nyerere akataifisha kwa chuki za udini.

Ohh crap, kimewazuia nini kujenga mengine? au ndiyo yale yale ya kulia victim kila mwaka?

mkapa hakutoa chuo cha Morogoro kwa moyo mweupe,alitoa ili kujisafisha na mauaji ya bila hatia ya mwembechai na Pemba kwa chuki zake kwa waislam,

iwe ametoa kwa hiyari au kwa lazima bado ukweli unabaki pale pale kuwa yeye alitoa chuo cha watanzania wote kwa waislam.

baada ya kuwaua waislam bila hatia,huku akiwa kajilimbikizia mali nyingi kwa dili zake chafu kuanzia EPA,KIWIRA,KAGERA SUGAR akaona atakuwa hana cha kusema mbele ya watanzania na waislam, kote ananuka akaona atoe chuo kama njia ya kujisafisha.

Okay ... hata kama amewauwa waislam, sasa iweje? unataka kujilipua na mabomu ili ulipize kisasi?

Slaa kama alikuwa mpenda haki angesema jamani wakati tunaanda hii MOU walikuwepo waislam mbona leo kwenye kusaini hawapo?

Kama waislam walizira kama ilivyo kawaida yao ya kuzira yeye angefanya nini? Hii dunia inaenda kasi sana ukisubiria watu wavivu na wenye kulia lia utabaki ukiwa masikini maisha yako yote.

walitumiwa waislam mwanzoni ili kumdanganya mzee Mwinyi kuwa dini zote ziko huko mbeleni LOWASSA AKASAINI na jamaa zake wa kanisa.

Hao waislam wanangoja nini kusaini tena sasa hivi?

watu hawa hawa mnalalamika kuwa waislam wasiwe na mahakama ya Kadhi KWA PESA ZA taifa, tukisema tujiunge na OIC ili tutumie pesa za waislam hamtaki.

Oh oooo ohhh, kutumia pesa za waislam? yaani wengine wakufanyie kazi kisha wewe uje kutumia pesa zao. Akili ya uvivu na utegemezi kama hii ndiyo inakufanya uendelee kuwa masikini huku ukizidi kuwalaumu wenzako kwa hayo matatizo yako.

kwa kweli ndugu zetu hambebeki na mnazidi kutujengea chuki kwa kutuwekea mamikataba kama hii inayowanufaisha nyinyi tu. mnafiki mbunge LAZARO tunaomba kauli yako juu ya MOU ya kanisa na serikali?

Unamtisha nani? au unataka kuanza kulipua majengo yote wa wasio waislam?
 
Wakuu zangu mnapoteza muda wenu bure kwa sababu wengi ya watu hapa ni vigeugeu..
Nitaambatanisha mtazamo wangu ktk maswala yote ya dini ambayo yamekwisha tokea hapa JF hadi sasa hivi.

Swala la MOu halina tofauti kabisa na OIC na mimi Mkandara sioni ubaya wa maswala yote haya kukubalika kwani kila seti inahitaji nutrition hizi kujijenga..tatizo ni usiri uliokuwepo ktk swala la MOu, jambo ambalo binafsi sikuona sababu kabisa ya serikali kulifikisha Bungeni swala la OIC kama ilivyokuwa kwa MOu..Ni swala la kijamii ambalo mara zote ni swala nyeti (Usalama wa Tiafa) huwekwa siri.. Usiri wake hautokani na kuwai mkataba feki, mbaya ama kuna mipango ya kuangusha dini nyingine isipokuwa ni kitu kinachohitajika na seti moja lakini uwazi wake unaweza hatarisha Usalama wa Taifa huru. Hata Marekani kuna maswala ambayo ni rais na makamu wake tu ndio hujulishwa na CIA na waka deal na CIA, maseneta hawajui kinachoendelea...

Pili, swala la mahakama ya kadhi na waraka wa kanisa ni vitu ambavyo naviona vimekosewa kwa taratibu zinazochukuliwa hivyo zote ni bogus.. Napinga mahakama ya kadhi kama navyopinga waraka wa kanisa.. Kama mnaona mahakama ya kadhi ikianzishwa Wakristu nao watataka mahakama yao, iweje iwe vigumu kwenu kuona kwamba waraka wa kanisa ukipokelewa basi, Waislaam na Mapagan nao watataka waraka wao usikilizwe ktk maswala hayo hayo ama mengine.. Hivyo kupoteza kabisa dira ya nchi yetu..
Wakuu zangu najua wengi wenu mkianza kujiuliza ktk maswal hayo hapo juu mtapata majibu tofauti kabisa pamoja na kwamba yanafanana sana tu.. Wapo wanaonga mkono OIC lakini hawaungi mkono MoU na kinyume chake.. wapo wanaunga mkono waraka wa kanisa lakini hawakubaliani na mahakama ya kadhi kwa sababu zinazojifunga zenyewe..
 
Kama unazo facts jibu hoja za msela point by point sasa acha kurahirahi..
David Solomon
Nikujibu nini zaidi?
ikiwa MOU mmeifanya kinyemela lakini OIC ijadiliwe bungeni haki na usawa uko wapi?Bwana Slaa anajua kila kitu lakini alinyamaza kimya kama mwana haki angesema kwenye MOU hakuwa uwakilishi wa Bakwata.
 
Bua ha ha ha..

Nimeshakuwa David Solomon sasa..he he he. Mimi naitwa Abdulhalim bana mdogo.

Naona mada imekuwia ugumu, na hivi ndivyo ilivyotegemewa..watu mnaotanguliza udini na chuki, busara na elimu huwakimbia..

Wakatabahu.
 
Wana JF hili linawezekana kuwa ni swali la kijinga, na mara nyingi watu wanao-raise issue hii ya wakristo kupendelewa na serikali au waislamu kupendelewa na serikali ni watu walio mufilisi kimawazo. Na ambao wameshindwa kuona matatizo halisi na ya msingi yanayowakabili watanzania, au ambao hawajui nini kifanyike ili watanzania wote waishi maisha bora.
Au wanaowatumia waislamu kufikia malengo yao ya kibiashara na kisiasa, ambao wanajua kabisa wanayosema hayawezi kuwasaidia waislamu.
Naamini kuwa kwenye jamii ya watanzania, kama mwislamu akiwa na maisha mabaya mkristo hawezi kuwa na maisha mazuri, na mkristo akiwa na maisha mabaya hata mwislamu hawezi kuwa na maisha mazuri.

Nakumbuka kuna siku nilikuwa natazama kipindi kimoja channel Ten, wageni walikuwa Professor Safari na Ali Mafruki (sina hakika na jina). Walisema kuna conspiracy ya kuifanya Tanzania iwe nchi ya kikristo, ndio maana wanaopata elimu zaidi ni wakristo, watu wenye nyadhifa nyeti serikalini ni wakristo, magerezani wakristo ni wachache kuliko waislamu, na waislamu wanawekwa magerezani kwa makusudi ili kuwapunguza mitaani, hospitali zote za serikali ni za kikristo, vyuo na hasa mlimani wanapendelewa wakristo, na hata sheria tunazofuata Tanzania ni za kikristo, kisa zimetoka Uingereza ambayo ni nchi ya kikristo.

Sijui hali hii inaelezwa vipi kwa Zanzibar ambao asilimia zaidi ya 95 ni waislamu, huenda kwa mantiki ya hao wenye “conspiracy ya wakristo” waislamu wa Unguja wana maisha bora kuliko wa bara.

Kuna arguments nyingi sana ambazo zinachekesha sana ambazo siwezi kuziweka hapa, nyingine naona kama zinawadhalilisha waislamu na hata hao wakristo wenyewe.

Nimewahi kusikia na wengine waliitisha hata mkutano wa waislamu ili kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha nchi haichukuliwi na wakristo, nasikia wameweka na mkakati pia ambao sasa unatekelezwa kisirisiri.

Swali langu ni kuwa. JE ni kweli kuna conspiracy yoyote ya kuwadunisha waislamu hapa Tanzania? Is it really or perceived? Ni kweli kuna conspiracy ya kuwadumisha wakristo? Na sisi tusio wakristo na waislamu tuko wapi kwenye hizi conspiracy?
 
Hivyo hujui kuwa hata humu jamvini ilishaletwa MoU kati ya serikali na wakristo?Au huna macho hata masikio huna!Hilo jambo lilishasemwa mara nyingi zilizopita na sasa halina tena hamu humu jamvini,tafadhali futa mada yako na kama huna cha kuandika ni bora ukanyamaza kama Kingunge.
 
Na serikali ilipotwaa taasisi za kanisa kama vile mahospitali na mashule ilikuwa ikiwapendelea wakristu si ndio?
 
sasa uwezo wetu wakufikiri unayeyuka....tunapoteza nuru ya kuona hata umbali wa mita kumi......matatizo mengi ya Waislamu wenzangu ni kudhani kua adui yetu mkubwa ni kushine kwa makanisa ya Kikristo na Wakristo wenyewe, adui yetu ni Historia ya usaambaaji wa Uislamu na waislamu wenyewe,
unadhani fursa za kusoma Tanzania zinauliza wewe ni dini gani...lakini waislamu wenyewe wasomi hawachukui hatua za msingi kurekebisha hali, unadhani tunaonewa....kwa taarifa Ukombozi pekee wakututoa kwenye matatizo haya ni elimu wala sio upuuzi unaojadiliwa kua kanisa ndo limetufikisha hapa, Tuwape Elimu stahiki watoto wetu badala yakupambana na uvaaji wa Hijab.
nimesikiliza redio yetu ya dini juzi....wanasema kua kuna kamati imeundwa na itatembea nchi nzima kuhimiza watoto Wakiislamu wavae Hijab....na sio kuwaambia wakasome.
Angalia seminari zetu za kidini...Jabal Hilla Morogoro, Al harramain...huwezi kulinganisha kwa ubora na Lutherans Junior Seminaries yoyote au seminari yoyote ya Kikatoliki.
Tuacheni maneno maneno...utawapata wapi kwenye ajira wakati tumekimbia madarasa? hawa akina Lipumba ,Safari na wengine wamefanya nini kuinua ustawi wa Waislamu kivitendo.
Tumefikishwa hapa na sababu za historia yetu tusidanganyike.
 
Hivyo hujui kuwa hata humu jamvini ilishaletwa MoU kati ya serikali na wakristo?Au huna macho hata masikio huna!Hilo jambo lilishasemwa mara nyingi zilizopita na sasa halina tena hamu humu jamvini,tafadhali futa mada yako na kama huna cha kuandika ni bora ukanyamaza kama Kingunge.

Mkuu kama umesoma sehemu ya mwanzo ya maelezo yangu nimesema hili ni jambo la kijinga, hata tunaposikia kuwa kuna MOU kati ya wakristo na serikali i wonder nani Tanzania mwenye mamlaka ya kuwakilisha madhehebu ya yote ya wakristo, walokole, wakatoliki, wasabato, waanglikana, walutheri, mashahidi wa yehova nk na tunapoelekea 2010 kuna watu wanaweza kujaribu kutumia jambo hili ambalo wenye akili hapa JF clearly wanaona na wanaita low level of thinking kuwarubuni watanzania wengine wasio na elimu.
Lakini pamoja na ujinga wake usi-underestimate influence inayoweza kusababisha kwenye uchaguzi wa 2010.
 
Na hayo ndo hasa Wasomi uchwara Wakiislamu wanayotafuta, hatumjui mchawi wa uduni wa maisha miongoni mwetu, kweli inakera.
Ipo siku tunajua ukweli.....TUSIDANGANYIKE ADUI YETU NI SISI WENYEWE KUCHUKUA HATUA, juzi hapa nimeona post ya ndugu yangu wakiislamu anaomba msaada wa tende...kweli, sisi tunataka kujikomboa? matunda unaomba msaada.
 
Back
Top Bottom