Huduma za jamii ni kazi ya serikali, kwa hiyo mashirika ya dini yanafanya hivyo kwa hisani tu. kwa maneno mengine serikali ilitakiwa kufanya hayo yote, lakini tuyashukuru hayo mashirika kwa kuisaidia serikali. na nina uhakika mashirika ya dini zote yananufaika na fedha za serikali, ingawa yanatofautiana viwango kulingana na yalivyojiwekeza.
Ushauri: Tumieni haya mashirika kujiendeleza hasa kielimu, kwasababu miaka ijayo mambo yatakuwa mabaya zaidi. mimi watoto wangu nawapeleka shule yoyote iliyo bora bila kujari ni ya kiislamu au kikristo ilimradi inafuata maadili na kutoa elimu bora. Chonde chonde ndugu zangu badala ya kuendeleza malumbano ni vizuri ukatumia fulsa zilizopo ili baadae usiendelee kuwa mlalamikaji. Sisi ni ndugu ukristo na uislamu umeletwa ukatukuta, sasa iweje uwe bora zaidi ya udugu wetu? kama dini zinatugombanisha basi hizi dini hazina maana.