Mjumbe aliyeandika mada yenye "MAJIBU KWA DR SLAA" ingefaa atueleze yafuatyo:
a) Amebainisha utafiti wake unaoonesha asilimia ngapi ya fedha inatolewa na serikali kwenda kwenye hospitali za kanisa na zile za serikali. Mbona anaongozwa na taasubi (biasness): ni kwa nini hajadadavua hospitali zinazomilikiwa na kanisa zinapata asilimia ngapi? Hapo ametaja Waislamu. Je kuna hospitali yenye jina hilo Waislam? Iko wapi? Nami niende nikatibiwe?
B)Ainishe hizo hospitali zilijengwa kwa hela za kanisa au serikali? Ukisoma kwenye hiyo MOU huoni kwamba wewe ni mzushi na mnafiki - unasema uongo?
C) Hospitali hizo haziajiri madaktari na manesi waislamu?
d) Je hospitali hizo za kanisa haziajiri wafanyakazi wengine ambao ni Waislamu?
e) Kama kweli utafiti wake hauna walakini - ni kwa nini hajatuorodheshea hospitali zinazomilikiwa na msikiti ili tuzijue?
f) Mbona anatafiti ofisi ndogondogo tu na kuainisha kuna Wakristo wangapi katika sekta hiyo ya ukaguzi (elimu). Mbona hafanyi utafiti na kutuorodheshea ngazi za juu za nchi hii zimeshikwa na nani? Kwa nini hajatuambia mkuu wa majeshi, mkuu wa kila kitu (kama kweli wewe ni mtafiti na sio mzushi) kwa nini hubainisha idadi ya waislamu walioshika nyadhifa za juu serikalini bali una hangaika na vitu vidogodogo?
Toa takwimu katika sekta zote za nchi hii utuoneshe asilimia ngapi ya wasilamu na Wakristo wameshika nyadhifa hizo.
NAKUSIKITIKIA SANA KWA KUWA UNAJIITA MTAFITI LAKINI WEWE SI MTAFITI - BALI NI MJENGA FITINA!
1. Ngoja nianze na hili la CAUSE and EFFECT - walioneza Uislamu walikazania zaidi kueneza dini ya Kiislamu kwa kuwafundisha watu wawe Waislamu na kujenga nyumba za ibada tu.
2. Wamisionari wao walieneza dini yao (Ukristo), kujenga makanisa, shule, hospitali na huduma zingine za jamii.
3. Baada ya sehemu zote mbili kupata wafuasi wazawa kila kundi liliendeleza kile lilichorithishwa.
4. Waislamu wazawa waliendelea kuhubiri dini ya Kiislamu, mafundisho na ujenzi wa nyumbaza ibada.
5. Wakrsto wazawa waliendelea kuhubiri dini, kueneza mafundisho yao, kujenga makanisa, hospitali, shule na kushiriki katika huduma zingine za jamii.
6. Watoto wao pia walirithi approach ya kila kundi hadi leo.
7. Waliojenga shule, hospitali na kushiriki huduma zingine za jamii walijikuta wanasoma kwa idadi kubwa na wanajiriwa sehemu mbalimbali.
8. Ambao hii haikuwa approach yao waliijikuta wanabaki nyuma katika kupata fursa za kusoma na kuajiriwa kama walivyo Wakristo.
9. Mwalimu Nyerere aliona hali hiyo itajenga matabaka katika jamii na hivyo akaamua kutaifisha shule na hospitali za misheni ili watoto wote wasome na hizo shule na hospitali zilizotaifishwa ziliwahudumia pia Waislamu na hata baada ya baadhi kurejeshwa waumini wa dini ya Kiislamu wameendelea kupat huduma sawa katika sehemu hizo.
10. Leo wamemgeuka Nyerere na kumwita mdini na aliyewakandamiza wao.
11. Ni bahati mbaya sana watu kunyea kambi!