Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Huyo wa mechi sita anajua baada ya hizo mechi mtaendelea kuvaa jezi mtaani kwahiyo bado mtatangaza biashara yake tu, wale wenye dini zao wasiopenda kamari basi washapata mtoko wa jezi
Na vilevile kawapa jezi ya blue watokane na ile adhma ya kuvaa nguo za njano au kijani
 
Wewe Ndio Huna Akili, MBUMBUMBU Kabisaa Kolo Waheed Wewe, Yani Mtu Anakudhamini Kwa Mechi Sita Tu Za Uhakika Endapo Timu Haitafanikiwa Kuendelea Hatua Inayofata Unaingiza 1.5B…Sasa Huyu Mtu Ukimpa Mkataba Mrefu Itakuwaje ?, Si Kuna Mpunga Wa Maana Hapo..
Usichokijua ni kwamba GSM ni partner wa Haier hata kabla ya mkataba huu, kwa hiyo ni uhuni fulani umefanyika kuizunguka SportPesa
 
Hivi uyu Abbasi Tarimba sindo mwanachama kindakindaki wa Yanga, kulikoni anaingiza siasa kwenye Mpira, Yanga baadaye ya kuona kwamba mdhamini wao Sports pesa anaomba kubadilisha jina na kuweka Visit Tanzania badala ya Sports pesa, Jamaa wakaona apo apo ndo pakupitia maana mkataba unatambua Neno Sportspesa.
Kingine Abbasi tarimba Aachane na hizi Siasa kisa yeye ni mbunge, anataka attention ya kisiasa kwa Timu ya Yanga na Kampuni ya Sportspesa kupata maileg kisiasa.
Nathani tuanze kuwa serious na terms and conditions of business... Tunafeli sana na mwisho wa siku Makampuni makubwa yanaogopa kuja kufanya biashara na Watanzania kwa sababu hizo hizo za kutokuheshimu mikataba.
Sport pesa walijua Abbas Tarimba ni mshabiki lia lia wa utopolo,wakamwajiri,kwa hiyo wasitegemee kushinda hiyo kesi labda wamfukuze kazi kwanza.

Sport pesa ni wapuuzi tu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Nimeona hayo maelezo nikabaki kujiuliza maswali. Yanga ikivaa visit Tanzania je sport pesa watafaidika na kipi hapo?
Ishu ni yanga kupiga pesa huku na huku kwa mabwana wawili
 
Katika watu wanaokula mshahara wa bure ni mwanasheria wa yanga hakuna hata kesi moja aliyoshinda na kawaingiza yanga mkenge mara kibao kule Turkey walivunja mkataba kihini wakapigwa fine wakati walikuwa washafanya booking kesi ya Morrison chalii kesi ya feisal imemshinda yaani yule jamaa ni kilaza nahisi itakuwa kuna ndugu yake pale yanga anayemfanya abaki hadi leo jamaa ni kilaza pro max mpaka hiki kipengele cha sports pesa kimemshinda kukitafsiri kweli.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Kiweke hapa hicho kipengere mkuu tukishuhudie kinasemaje
 
Sijawahi kukukosoa rafiki yangu ila leo tu
Swala la fei sio kushindwa kumlipa. Tatizo ni utaratibu aliotumia Fei kuondoka. Makataba unasema anaruhusiwa kuvunja/ kununua mkataba wake kwa kushauriana na klab NA KUTOA SABABU zinazopelekea kuondoka kwake. Sababu za fei ni mshahara mdogo hiyo kisheria haikupi haki ya kuvunja mkataba.

Angepewa haki mapema kabisa kama angekuwa anadai mshahara halipwi, au hachezeshwi n. k. Kisheria mkataba hauamuliwi kimasirahi tu.

Nitakula mfano Kuna hilo jengo la sido hapo karibu na cbe. Sido walitoa notice wa wapangaji wote wahame ili livunjwe lakini ilifunguliwa kesi na sido walishindwa maana sababu zao zilikuwa ni kutaka kuliboresha jengo huku tayari wana mikataba hai na wapangaji.

Hope utanielewa raftiki. Kuna sheria na ushabiki.
Asipokuelewa na hapa mchape kibao.
 
Aibu kubwa Sana na tamaa iliyopitiliza, timu Ina wanasheria halafu inafanya kosa la kininga kiasi hicho? Sasa hapo wameingia Cha kike ,imesha nyesha tayari soon panapovuja pataonekana. Nilishtuka Mzee mshindo msola kujitoa kwenye kugombea dakika za mwisho, nilishangaa mgombea wa uraisi akimnanga mgombea mmoja wa makamu na kumpigia kampeni wazo wazi mgombea mwingine.

PACTA SUNT SERVANDA
 
kwa maelezo hayo ya SportPesa, sio lazima iwepo Visit Tanzania, panaweza pakawa wazi, lakini sharti pasiwepo mdhamini mwingine kama wao hawapo
Kama sportpesa wangekuwa wanajitambua kuwa uwepo wao upo hadi kwenye michuano ya kimataifa kwa Yanga basi kungewwkwa vipengele vya bonus hadi kwenye michuano ya kimataifa.. lakini wamewekeana vipengele vya bonus endapo Yanga itafanya vizuri kwenye NBC na Azam Federation cup pekee.
 
Hilo unalolisema limeelezewa vizuri na SportPesa kwenye hilo bandiko lao

Means wanatambua sheria za ufadhili wa CAF na ndio maana wao wameweka wazi kuwa Yanga walipeleka ombi kwa SportPesa
kwa ajili ya kupewa ruhusa ya kupata mfadhili mwingine

Ombi ambalo lilikataliwa

Yanga ni kama waliamua kumzunguka kwa nyuma SportPesa na kumleta mfadhili mpya

Katika hili naona Yanga wana hatia
Bro huwa naheshimu sana michango yako kule kwenye jukwaa la jamii intelligence ila huku kwenye jukwaa la sports huwa unashindwa kabisa kuwa neutral. Kama kanuni inasema wazi kuanzia hatua ya makundi haitakiwi kuwekwa kifuani kampuni yoyote zaidi ya 1xbet basi moja kwa moja yanga anayo haki ya kuweka mdhamini mwingine bila kusubiri go ahead ya sportpesa maana kwa mujibu wa utaratibu uliopo sportpesa hausuki uko na ilo alitakiwa kulifahamu tangu mwanzo kipindi wanaandikishiana mkataba.
 
1. Kuna kutumika kwa watu fulani kulazimisha neno fulani likae kwenye jezi za Yanga.

2. Ubinafsi wa sportpesa ( kama walipelekewa ombi la kuwepo kwa mdhamini mpya kwa michuano ya CAF, kwann walikataa hali ya kuwa biashara zao hazifanani, hivyo isinge muathiri)

3. Kujihami kwa sportpesa na kuleta taarifa kwa umma haraka mno, (anaogopa nini na anamuogopa nani)

4. Ulazima wa Yanga kuweka mdhamini mpya lengo ni kuitangaza timu zaidi, je hili sportpesa halitaki.? ( Hataki Yanga ijitangaze zaidi, ili ije kuwa faida kwake pia baadae.?

5. Soka ni biashara, biashara ni matangazo, "visit Tanzania" sio Tangazo la kibiashara kwa Yanga

6. Ikifika mahali mnaleta taarifa kwa umma, basi leteni na mikataba ili tuweze kuwatetea vizuri, (tujue ni nani yupo sahihi na nani ana kosa)
Mwananchi kunywa pepsi hapo nitalipa
 
dawa imekuingia, time will tell mzee dingi
 
Back
Top Bottom