Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Kuweka nembo hii kwenye jezi ya Yanga/Simba inawaingizia sh ngapi?
Mtu ambaye hajawahi kupata pesa akiionja tu anataka kujiona anaijua pesa kuliko wengine hata wale waliomtangulia. Leo Yanga ana kiburi cha kukataa kuutangaza utalii wa nchi kisa haumuingizii pesa, maajabu haya.
 
Leo Yanga ana kiburi cha kukataa kuutangaza utalii wa nchi kisa haumuingizii pesa, maajabu haya
Ile ni biashara kama biashara nyingine. Hayo maswala ya uzalendo hayana misingi kwenye sheria za biashara.
Na hiyo biashara ya utalii sio HISANI.
Arsenal anapokea mpunga mrefu kutoka serikali ya Rwanda kwa kuitangaza sekta yake ya utalii.
Hakuna sababu ya Yanga/Simba wasilipwe eti kwa kigezo mfu cha uzalendo.
 
Haier ni GSM
Duuh Ina maana hujui kuwa Hair na GSM ni kampuni mbili tofauti?

Hair ilishawahi kutaka kuweka mzigo man u lakini Dili liligoma tu sasa unaposema ni GSM hapo unakua unakosea
 
Bro huwa naheshimu sana michango yako kule kwenye jukwaa la jamii intelligence ila huku kwenye jukwaa la sports huwa unashindwa kabisa kuwa neutral. Kama kanuni inasema wazi kuanzia hatua ya makundi haitakiwi kuwekwa kifuani kampuni yoyote zaidi ya 1xbet basi moja kwa moja yanga anayo haki ya kuweka mdhamini mwingine bila kusubiri go ahead ya sportpesa maana kwa mujibu wa utaratibu uliopo sportpesa hausuki uko na ilo alitakiwa kulifahamu tangu mwanzo kipindi wanaandikishiana mkataba.
Hivi unafikiri Yanga walikuwa wajinga kupeleka ombi kwa Sportpesa kuona kama wataruhusiwa kuweka mfadhili mwingine?

Unajua ile Visit Tanzania kwenye jezi ya Simba iliwekwa kwa idhini ya Sportpesa na sio maamuzi ya Club?
 
1. Kuna kutumika kwa watu fulani kulazimisha neno fulani likae kwenye jezi za Yanga.

2. Ubinafsi wa sportpesa ( kama walipelekewa ombi la kuwepo kwa mdhamini mpya kwa michuano ya CAF, kwann walikataa hali ya kuwa biashara zao hazifanani, hivyo isinge muathiri)

3. Kujihami kwa sportpesa na kuleta taarifa kwa umma haraka mno, (anaogopa nini na anamuogopa nani)

4. Ulazima wa Yanga kuweka mdhamini mpya lengo ni kuitangaza timu zaidi, je hili sportpesa halitaki.? ( Hataki Yanga ijitangaze zaidi, ili ije kuwa faida kwake pia baadae.?

5. Soka ni biashara, biashara ni matangazo, "visit Tanzania" sio Tangazo la kibiashara kwa Yanga

6. Ikifika mahali mnaleta taarifa kwa umma, basi leteni na mikataba ili tuweze kuwatetea vizuri, (tujue ni nani yupo sahihi na nani ana kosa)
Yani hapo umekaa umewazaa na mpka kumshirikisha mchrpuko wako ndio umekuja na hoja za kimbulula namna hiyo. Kweli utopolo ni utopolo tu hata uwafanyeje
 
Kwenye preliminary stage Yanga walivaa jezi za sportpesa, ile ilikuwa local?
Preliminary stage ile ni ngazi ya awali hivyo hata coverage ni ndogo . Official broadcastiing wa CAF harushi matangazo na hata main sponsor wa CAF haonekani.
 
Hofu ya SportPesa ni pale jezi za Haier zinatakapokuwa maarufu kuliko wao. Ukizingatia wengine wanaona kuvaa SportPesa ni ku promote kamari.
 
Naomba niambie sportpesa kaahidi kutoa bonus ya sh ngapi endapo Yanga watafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa? Maana kwenye NBC na Azam Federation cup limewekwa wazi kiasi cha bonus watakachopata Yanga kutoka kwa sportpesa. Kama hakuna sehemu yoyote ambayo sportpesa katamka kuhusu michuano ya kimataifa. maanake hao sportpesa walijua ukomo wao wa udhamini
Mkataba wa Yanga na Sportpesa ni kwenye swala zima la jezi

Sportpesa pesa kalipia eneo la kifua kwenye jezi ya Yanga kuwa lile ni eneo lake isipokuwa tu kwenye mashindano ya CAF ambayo tayari yameset sheria kwa kutoruhusu mdhamini anyejishughulisha na betting

Kwa maana hiyo sasa kampuni yeyote ambayo haijishughulishi kwenye maswala ya bahati nasibu inapotaka kuingia makubaliano na Yanga ni lazima Sportpesa pesa ndiye awe mru wa mwisho kuidhinisha au kubatilisha hilo ombi

Kwasababu Sportpesa pesa ni mdhamini mkuu na sehemu wanayotaka kuweka logo yao tayari ni sehemu ambayo Sportpesa ameilipia kwa miaka mitatu
 
EXACTLY! Ila hawakutaka kuonekana wanaiiga Simba na wakiacha jezi wazi wataonekana siyo wazalendo kwa kukataa kutangaza utalii, kwa hiyo wakaona liwalo na liwe.

Washukuru huyo Abbas Tarimba ni mtu wao, labda atafanya jambo la kuwasamehe ila hapa wangelipa fidia kubwa sana.
Sportprsa makao makuu yapo uingerexa
 
Mkataba wa Yanga na Sportpesa ni kwenye swala zima la jezi

Sportpesa pesa kalipia eneo la kifua kwenye jezi ya Yanga kuwa lile ni eneo lake isipokuwa tu kwenye mashindano ya CAF ambayo tayari yameset sheria kwa kutoruhusu mdhamini anyejishughulisha na betting

Kwa maana hiyo sasa kampuni yeyote ambayo haijishughulishi kwenye maswala ya bahati nasibu inapotaka kuingia makubaliano na Yanga ni lazima Sportpesa pesa ndiye awe mru wa mwisho kuidhinisha au kubatilisha hilo ombi

Kwasababu Sportpesa pesa ni mdhamini mkuu na sehemu wanayotaka kuweka logo yao tayari ni sehemu ambayo Sportpesa ameilipia kwa miaka mitatu
Haujanijibu swali langu, kwanini sportpesa aweke vipengele vya bonus kwenye mashindano mawili tu ya ndani wakati inashiriki michuano ya kimataifa pia? Je mashindano ya kimataifa haiyahusu sportpesa?
 
Sportprsa makao makuu yapo uingerexa
Basi hao wachina wawe makini zigo lisije likawaangukia wao. Kinachoweza kuwaokoa Yanga ni wanasiasa walio nyuma yao, wanaweza kuitisha SportPesa kuwa mazingira yao ya kufanya kazi nchini yanaweza kuwa magumu. Nchi hii mambo yakibumbuluka huwa hatutafuti chanzo, tunatafuta jinsi ya kuzima so.
 
Sijajua unauelewa gani kwenye masuala ya masoko ila kwa uchache, uuzwaji wa jezi mpya zenye udhamini wa kampuni mpya unaweza kuathiri uvaaji wa jezi zenye nembo ya sportpesa mtaani. Wanunuzi na wavaaji wa jezi ni wale wale. Hilo ni moja tu.
Uuzwaji wa jezi atayeathirika ni GSM, na hii ni kama ana akiba ya jezi za zamani store, vinginevyo Sportpesa ataathirika endapo kama jezi ya zamani itapotea kabisa mtaani na kusababisha nembo yake isionekane popote.
 
Ile ni biashara kama biashara nyingine. Hayo maswala ya uzalendo hayana misingi kwenye sheria za biashara.
Na hiyo biashara ya utalii sio HISANI.
Arsenal anapokea mpunga mrefu kutoka serikali ya Rwanda kwa kuitangaza sekta yake ya utalii.
Hakuna sababu ya Yanga/Simba wasilipwe eti kwa kigezo mfu cha uzalendo.
Sikupingi ila hiyo ni jeuri ya mtu ambaye ndiyo ameijua pesa jana. Yanga kwa ukaribu wake na CCM haina historia ya kuitunishia kifua Serikali. Kama Simba waliweza kufanya hivyo bila shida sioni Yanga atashindwaje.
 
Haujanijibu swali langu, kwanini sportpesa aweke vipengele vya bonus kwenye mashindano mawili tu ya ndani wakati inashiriki michuano ya kimataifa pia? Je mashindano ya kimataifa haiyahusu sportpesa?
Mashindano mawili yapi na yapi?
 
Back
Top Bottom