Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Makolo kaeni kwa kutulia, Sport Pesa ya Tarimba ndiyo Yanga ile ile, mnamaliza MB zenu bure
 
Wanataka sportpesa ajitoe mwenyewe
Ila hili swala naona wakipelekana mahakamani
 
sportspesa hakuna kilichovunjwa ni uwezo mdogo wa kutafsiri mkataba
 
Naomba niambie sportpesa kaahidi kutoa bonus ya sh ngapi endapo Yanga watafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa? Maana kwenye NBC na Azam Federation cup limewekwa wazi kiasi cha bonus watakachopata Yanga kutoka kwa sportpesa. Kama hakuna sehemu yoyote ambayo sportpesa katamka kuhusu michuano ya kimataifa. maanake hao sportpesa walijua ukomo wao wa udhamini
 
Hata mimi nimesikitishwa. Ila makampuni yawe yanatathmini credibility ya uongozi wa club kabla ya kuingia mikataba. Yanga haina uongozi ina wahuni na machawa
Siku hizi mmekua wanahakati wa kutetea haki, baada ya Feisal mmehamia Sportpesa
 
Sijajua unauelewa gani kwenye masuala ya masoko ila kwa uchache, uuzwaji wa jezi mpya zenye udhamini wa kampuni mpya unaweza kuathiri uvaaji wa jezi zenye nembo ya sportpesa mtaani. Wanunuzi na wavaaji wa jezi ni wale wale. Hilo ni moja tu.
 
YANGA NI KUBWA KULIKO SPORTPESA..

VISIT TANZANIA NI TANGAZO LA KIBIASHARA PIA, kama tu la VISIT RWANDA. Yes ni tangazo la kibiashara kuvutua watalii na wawekezaji. YANGA ANAFAIDIKA NINI??

Kama hawataki watupishe, hongera Uongozi kwa kuitafutia klabu pesa na mikataba minono
 
Je mkataba walioingia Yanga na Sportpesa ulikuwa unahusu hadi michuano ya kimataifa?
Kama ulikuwa unawapa haki Sportpesa hadi kwenye mashindano ya kimataifa basi Yanga wamefanya kosa kukiuka mkataba.
Yanga wametoa tamko, wamesema walimuomba Sportpesa ruhusa, sportpesa hakuwajibu
 
Uko sahihi kabisa.
Ishu ni kupata maximum possible mpunga kutokana na udhamini.

Wenzetu hata jezi za mazoezi zina wadhamini tofauti.
Chelsea wana ile 3 na mazoezini wana TRIVAGO.

Kama hawataki wavunje mkataba wasepe.

Hatueki Visit Tz . Yanga siyo Royal tour
 
Tukitoa tottenham ni timu gani umewahi shuhudia?
 
Kwenye preliminary stage Yanga walivaa jezi za sportpesa, ile ilikuwa local?
 
GSM ni muuzaji wa Haier
GSM ni mdhamini wa Yanga
GSM ni kit maker
 
Kwahiyo niulize endapo CUF wangesema kila timu ivae uzi wenye nembo ya 1*Bet, Sportpesa wangesema Yanga atulipe fidia? Na je kama mdhamini wako mkuu ni Sportpesa akija kesho akasema kwenye kifua andika Mo energy utakubali kisa yeye ndiye mdhamini mkuu?
Alafu ukisoma waraka huo unaodaiwa kuwa wa sportpesa inaonekana Yanga hajaenda kuomba ruhusa Sportpesa bali aliwataarifu/kuwafahamisha tu kwamba kwenye mashindano haya tutakuwa na fulani. Mwisho siamini kama kweli ni waraka wa Sportpesa maana una ushabiki ndani yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…