Mke wangu baada ya kupata kazi na mshahara mnono ameanza kunidharau

Mke wangu baada ya kupata kazi na mshahara mnono ameanza kunidharau

Mimi nipo kwenye ndoa,Nina takribani ten years nimebahatika kupata watoto pia.napenda sana kuhudumia familia yangu kulingana na kipato changu.

Mwanzoni nilipooa mwenzangu hakuwa na kazi hivyo mimi ndio nilikuwa na 100*% ya Kila kitu ndani,kwa hyo after baada ya muda wife a akatoa wazo kuwa kwa kuwa yeye yupo home nivutavmpunga kwa mkopo then aanze biashara flani hivi.nilimwambia anipe uhakika wa hicho atakochokifanya kama kitaenda sawa

Nikamwambia na madhara ya hizo loans kama vile life kuwa tight n.k akasema kuwa ataweza kumudu.basi mimi nikavuta mzigo ,nikampatia akaanzisha biashara ,ikawa ilienda poa ,lakini baadae zikatokea shida katika usimamizi biashara ikafeli.kwa hyo akarudi home ,mimi nikawa ndio Kila kitu tena.

Basi Mungu si Athumani mlango mwingine ukafunguka,yeye akaajiriwa lakini hata hyo Hela yake bado ikawa ni ndogo ukilinganisha na take home yangu,lakini kulingana na kazi yake akawa anapata posho na maisha yanaenda. Familia ikaongezeka tukawa na watoto ,ndugu n.k kwa kifupi majukumu yakaongezeka ,.tukajubaliana nivute mzigo tujenge nikaenda benki tukavuta mpunga kweli ,tukaanza kujenga kweli,.

Mimi Hela ikawa ndogo napata kama walau Hela inayolingana na 1/3,basi yeye salary ikaoanda akawa ananizidi mimi walau kwa 59% ya mshahara plus marupurupu.akaanza kuwa na matumiz makubwa kupita hata kipato,akaanza lugha ya dharau kuona sifanyi chochote ndani ya nyumba.

Hakuna kushirikishana jambo lolote,akaanza kudemandi kuwa Sina akili ,Sina mpango wowote kuhusu maisha.mimi sio mtu wa vurugu sana.nakaa kwa kujuta sana kutokana na gharama za maisha,hata mambo yangu mengi nadhindwa kufanya.

Kwa kifupi ninajuta sana sijui nifanye nini jamani.mnaosema kataa ndoa mpo sahihi kwa sehemu wanawake Mungu anawaona,
Kataa ndoa tunaendelea kuchukua mapointi tu
 
huku kwetu hakuna prenup bro. Mki divorce mahakama itaamua huyu achukue kipi na huyu achukue kipi. kuna nchi moja ya kiafrika nilikwenda nikapenda maana mnapooana mnapewa fomu ya kujaza ambayo ina kipengele cha kuoana " in community of property" or"" out of community of property". Ninyi wanandoa mnaamua ndoa yenu iweje. Wengi ninaona wanapenda hii ya out of community of property maana mki dirvorce hamna cha kugawana mali. kila mtu anaishia na mali yake.
PRENUPTIAL AGREEMENT MUHIMU MKUU
 
Huko kuishi nao kwa akili au kuishi nao kwa kutumia nguvu? Kuna mwanamke anatoka nje kwasababu anasema mume wake ni katili hana furaha wala amani akiwa nyumbani. Kwahyo anatoka nje kuitafuta aman na furaha ya moyo mpka nyumani kwake anakuita kifungoni.
📌Huna akili!!!Nenda katafute kwanza akili ulipoipoteza.
 
Ngoja niwaibie Siri vijana wangu, wadogo zangu

Kitu pekee kinachofanya ndoa iwe na amani na furaha itawale kwenye muunganiko huo ni UTII......

Hata siku moja usikubali kuishi kwenye nyumba moja na mwanamke asiye kutii.......

Mwanamke wako anapopoteza UTII kwako mumewe unatakiwa umuache mara moja kwa ajili ya kulinda UTU wako, UHAI wako na AFYA yako kwa ujumla.....

Mwanamke automatic kaumbiwa kumtii mwanamume na kufuata kile ambacho anachoelekeza mumewe(kiwe cha kheri)

Ukiona mwanamke kapoteza UTII kwako mumewe basi lazima kuna mwanaume mwenzio anayemtii.....kwa kuwa moyo wa mwanamke kamwe haubaki tupu....kwa kuwa mwanamke ni kama kifaa kilichoumbwa kwa ajili ya matumizi lakini kinangoja maelekezo tu ndani yake ambaye ni mwanaume........

Ni afadhali kubwa mtengane mapema ukiwa na afya njema na nguvu za kuwahudumia watoto wako hata kama wako mbali

NASISITIZA TENA
MWANAMKE ALIYEPOTEZA UTII KWAKO ACHANA NAYE MARA MOJA.....

Kawaida ya mwanamke hakumbuki fadhila mpaka kule alipopategemea mambo yaende kombo........
Wengi huwa wanapuuza hili na kujifariji tufaraja twa UONGO hatimaye wanaangukia pua.
 
Back
Top Bottom