Kwanza mimi huwa si deal na mwanamke ambaye hatumii akili anatumia hisia muda wote. Mimi mwanamke napendana nae kwa pande mbili
Pande ya kwanza ni mwanamke kama mpenzi ambako huko ni uzuri wake wa mwili, usafi, ufundi wake kindani, mahaba yake kwangu kama mwanaume wake, na vinginevyo vyote vinavyohusika na mapenzi kwa maana ya raha za dunia.
Na eneo la pili ambalo ndilo nyeti ni eneo la mwanamke kama partner wa maisha kwa maana ya shughuli za kijamii uchumi (social economy) na kijamii siasa ( social political).
Huku napenda namna mwanamke anakuwa msaidizi kwenye kutunza mali na fedha tunazotafuta kwa kuwa mshauri mzuri kwenye matumizi na bajeti na hata kama hayupo vema awe tayari kujifunza na kutafuta maarifa mapya ili kunisaidia kuwa imara.
Lakini pia katika malezi ya watoto wangu awe mama mzuri na awe na influence nzuri kwa watoto kama mama yao na balozi wangu kwa watoto. Sio unawajengea watoto fikra kuwa baba ni mtu tu tupo nae ila hana umuhimu, watoto wasione umuhimu wa jitihada zangu na mchango mkubwa kwao na maisha yetu.
Lakini pia napenda awe kiunganishi kizuri cha familia. Sio tunagombana watoto wanasikia anawaambia baba yenu anataka kunidhuru, huo ufala sitaki kusikia. Awe mtetezi wangu popote pale awe tayari kwenda chini na mimi pale nitakapoporomoka sio anikwepe kutafuta unafuu halafu nikirudi juu alete kwato zake, nitachapa makofi.
Kimsingi hayo ni machache naweza sema kumdescribe mwanamke anavyotakiwa.
Kwa namna umemuelezea mkeo inanipa mashaka wakati unakutana nae ulikuwa una malengo gani na yeye na mlikubaliana nini. Kwasababu mahusiano yanaweza kuwa ni temporary au permanent. Ni vema nyote mkaelewana before hamjaseal the deal.
Sasa mkeo anaonekana hayupo tayari kucommit kwako, inaweza kuwa alikuja kwako kwa lengo la starehe na haya unayomwambia afanye si sehemu ya anachojua mlikubaliana kufanya aidha verbally au nonverbal.
Sasa kama mambo hayaendi ni heri usipoteze muda zaidi. Hao watoto kuwalea haitaki wazazi wanaobishana juu ya majukumu ambayo hata kuku au mbuzi hufanya bila kubishana. Huyu ulie nae ni wazi hataki hayo majukumu unayoshinikiza afanye kwasababu zake binafsi.
Hapo fanya maamuzi magumu. Safari Nzuri ya maisha yako na watoto wako isihujumiwe na mtu ambaye anajua wazi kuwa anakuharibia na anajiharibia. Mpeleke kwao kuwa mnashindwana majukumu, akakae huko atafute cha kufanya maana majukumu yake hayawezi.
Akiwa huko atajitafakari, na akikutafuta kuwa anataka kurudi mwambie akirudi basi aje kitofauti, upuuzi wake aache huko huku aje mpya kwa kufuata malekezo uliyomwambia kinyume chake asitegemee kuvumiliwa bali atarejea huko huko tena.
Kama atarudi na kujirekebisha ni sawa ni mama watoto wako hivyo mpokee na muendelee. Kinyume na hapo, akiamua kuvimba kichwa na kukaa kimya au kama akirejea na madudu yake , ni swala la mwaka m'moja tu kufanya maamuzi ya kutafuta mwanamke mwingine na kulea watoto wako bila kushirikiana na huyo mkeo wa sasa.
Wanawake wapo wengi sana huko nje.