Mfanyakazi mwenzangu aliletewa mtoto wa kambo. Mtoto kaja na tabia zake.
Mtoto ni noma, akimuona baba yake tu analilia chakula kilichopo jikoni hata hakijaiva.
Baba wa mtoto anamuuliza mke wake "mbona hao watoto wako hawalii njaa huyu ambaye sio wako ndio analia?" Dada wa watu inabidi amchotee mtoto chakula hata kikiwa kibichi.
Akitaka kununulia watoto wake kitu kama hana hela ya kutosha kumnunulia na huyo wa kambo anaona bora aache, hata kama ni mswaki.
Kuwalazimisha walale mchana sasa, alazimishe wa kwake tu huyo mwingine akilazimishwa anaonekana anateswa. Kwahiyo watoto wa huyo dada wakitoka shule wanapumzika, wa kambo anaenda kupuyanga mtaani.
Kuna ile hali ya kumcontrol mtoto asile sana , au asile vyakula vya aina fulani sana. Haloo utacontrol wa kwako tu usithubutu kumcontrol wa kambo umekwisha[emoji23][emoji23][emoji23]. Sasa huyu dada watoto wake anawawekea chakula cha kawaida, halafu huyo wa kambo sasa anajaziwa chakula kama cha kula watu wa 5. Ukimuuliza kwanini anasema "ukimpa kidogo baba yake anaona unamtesa".
Huu upuuzi mimi kamwe siwezi kufanya, ukiniletea mtoto, nitamlea kwa namna ninayoona mimi inafaa na usiingilie. Tofauti na hapo mwache alelewe na mama yake.