Mke wangu hawezi kuandaa milo mitatu kwa wakati na hataki msaidizi wa ndani

eMisango ikomeye mjini khunu Wasu…..πŸ˜…
 
Kama maeneo mengine anafanya mambo kwa usahihi isipokua eneo hilo tu, basi mvumilie tu, huku ukiwa unamsaidia kubadilika mdogo mdogo... Si mnasemaga Kila mtu ako na mapungufu yake.
 
Msiwege mnaoa
 
Tafuta mfanyakazi pisi kali zaidi yake mlete alafu Ili asiondoke huyo mfanyakazi mlipe hela zaidi ya wanaopokea wafanyakazi wa kawaida... Baada ya wiki utaona anajua kupika mke
Hataki msichana wa kazi nilishawahi kuleta narudi amesha watomua na kuwalipa pesa zao za usumbufu
 
Mbona kawaida mimi sio muumini wa kuzini ndo nifunge ndoa huyu mwanamke nilimkuta bikra mkuu.
Kumjua mtu sio lazma mzini kuna namna ya kufahamiana mambo madogo madogo Kam hayo ya kupika nk
 
Ndiyo kauli zake sikuzote
Alisahau kuwa mapenzi hayana formula
Ni kweli mke wanyumbani ni mtaamu akiwa anajua kupika na kufanya usafi wa chumbani huo ndo msimamo wangu.
 
Ukiwa unamaindi kila kitu hamtaenda, kazi gani unayofanya ya kula milo mitatu yote nyumbani?! Utaniambia wikiendi basi unaonekana wewe unapenda sana kula. Muda wote unawaza chakula tu.
 
Naomba nije kumfundisha kusonga ugali na kuosha Mwiko πŸ˜… (natania)
 
Au nikuletee MFUNDAMAHALA wa kizaramo ampe training ya masaa tu ili akae sawa
 
Kama hafanyi kazi yoyote mpelekee shule ya mapishi, akigoma mletee msaidizi , akigoma mrudishe kwao akajifunze kupika, akigoma mpige chini. Wanawake wako wengi sana tena watalaam wa jiko.

Swali la kizushi nini kinakuvutia zaidi kutoka kwake, kinachokufanya uvumilie mapungufu yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…