Mke wangu kapangiwa kazi Mkoani

Msaidizi yupo na ndio anaplan kwenda naye, hofu yangu ni hali ya hewa kubadilisha hawa watoto maana bado wadogo, mwanzo niliwaza huyu msaidizi abaki lakini niongeze msaidizi wa pili wa kulea watoto.
Kwani we ukisikia shinyanga unawazaje kwani? Hiyo hali ya hewa ina maana unataka kusema hakuna watu wanaoishi au unadhani shinyanga ni jehanamu???
Kwa taarifa yako shinyanga unayoiwazia wala sio kama hiyo. Shinyanga ni town tena pa kishua unless iwe ni shinyanga DC
 
Yaani sijui anadhani shinyanga ni rural sana au wanaishi watu gani sijui.
 
Kambarage, bugweto, burugalila, majengo mapya, mwasele, kitangili, nyanhende karibu na jeshini ndio sehem zilizotulia na zenye nyumba nzuri.
 
Hama Mfuate uishi nae,using'ang'anie kukaa Dar
 
Mwache aende nao Kama unayo nafasi kakae nao hata mwezi mmoja hivi ili kuweka mazingira sawa
 
Mwaka mmoja anaweza achishwa au unasemaje Mkuu, sema mawazo yenu yananisaidia hapa kumake decision
Wacha hizo mwamba mwaka mmoja huwezi kukaa naye wewe mwanaume unataka kutudanganya! Watoto waache waende na mama!
 
Kambarage pa kiduwanzi kule.

Nyumba za kizamani (zile za vyumba vitatu kushoto vitatu kulia katikati korido limejaa madumu ya wapangaji).

Maeneo classic kwa mtu aliyetoka Dar ni Majengo Mapya na Lubaga
Huyu naye anashauri kitu gani hiki? Eti Kambarage! Nyumba ziko Majaengo mapya, Viwanja Vya Mwadui, Bushushu, na Lubaga siyo mbaya!
 
Aende na watoto watasaidia kupunguza kasi ya kupigiwa, japo utapigiwa tu.
 
Tatizo la nchi za kiafrika miundo mbinu ingekuwa ulaya treni za umeme dakika tu upo mji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…