Mkoa wa Arusha una wilaya masikini sana

Ngorongoro, Londido, Meru, Monduli unajua kiwanja sh ngapi? Hatuzungumzii Arusha mjini bali Arusha kama mkoa
 
Sasa wakazi wa Ngorongoro ni kabila gani? Pale Wasso/Lolliondo ambapo ni makao makuu, kabila lipi limetawala?
 
Sasa wakazi wa Ngorongoro ni kabila gani? Pale Wasso/Lolliondo ambapo ni makao makuu, kabila lipi limetawala?
Mkuu wewe ni mwenyeji wa mkoa gani kwanza na hapo Loli umefika lini? Maana kwa akili yako unajua kuwa Loli ndio Ngorongoro yote.

Naomba nikufahamishe kuwa Ngorongoro kabila kubwa ni Wamasai na Loliondo ni sehemu ndogo sana tu ya wilaya ya Ngorongoro.

Unapajua Orlpalpal wewe? Nainokanoka? Orgosorok?
 
Wamasai wengi wanaishi mbugani, na kule inafahamika hawaruhusiwi kujenga makazi ya kudumu na ndo maana nikawazungumzia Wasonjo ambao wapo Sare, Digodigo n.k, na Loliondo ndo makao makuu ya Ngorongoro, kuna nini cha maana pale? Tena kwa Ngorongoro bora Monduli kdg. Ngorongoro na Longido ni mtu na mjomba wake, Kwa Arusha mjini sikatai imeendelea sana, ila Wilaya zake hapana kwa kweli, zina hali mbaya sana.
 
Nashukuru mkuu umeliona hilo, Kwa mfano Wilaya za Ruvuma zimeendelea ukifananisha na Wilaya za Arusha, Longido, Ngorongoro, Monduli huwezi kufananisha na Mbinga, Namtumbo, Tunduru, huo ndo ukwel, Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma Zimepitiwa na umeme gridi ya Taifa, zina barabara za lami.
 
Mbinga pameendelea sana. Mji mmoja safi sana.
 
Unaanza kujikanyaga kanyaga sasa.

Anyways asiejua maana haambiwi maana.
 
Nakubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…