Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Mwaka 2020 nilijitokeza kuweka nia kugombea ubunge kwenye jimbo la uchaguzi la Butiama kupitia Chama cha Mapinduzi. Sikufanikiwa: niliambulia kura mbili za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya.
Wakati wa mchakato, mtani wangu mmoja aliniomba nimkopeshe Sh.50,000. Nilimwambia nikishinda asinirudishie ule mkopo. Tangu wakati huo namtafuta kumpa taarifa kuwa sikushinda. Hapatikani. Nasikia kahama nchi.