Mkopo alioutoa Madaraka Nyerere wamuhamisha mtu nchi

Mkopo alioutoa Madaraka Nyerere wamuhamisha mtu nchi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
1643264177686.png
WATANI ZANGU
Mwaka 2020 nilijitokeza kuweka nia kugombea ubunge kwenye jimbo la uchaguzi la Butiama kupitia Chama cha Mapinduzi. Sikufanikiwa: niliambulia kura mbili za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya.

Wakati wa mchakato, mtani wangu mmoja aliniomba nimkopeshe Sh.50,000. Nilimwambia nikishinda asinirudishie ule mkopo. Tangu wakati huo namtafuta kumpa taarifa kuwa sikushinda. Hapatikani. Nasikia kahama nchi.
 
Ivi watoto wa Nyerere wanashida gani huwa naona kama wapo wapo tuu...
Tatizo baba yao. Penda sana sifa za kijinga kupeleka pesa na rasilimali zetu kukomboa watu na mataifa uchwara yasiyo nashukran eti akidhani ataacha legacy.

Matokeo yake Kaambulia tu jina lake kubakia kwenye vibarabara uchwara vya uchochoroni kwenye hizo nchi. Na huku kwetu katuachia mifisi na mchwa inatafuna nchi kwa fujo bila aibu.

#MboweSiyoGaidi

#MboweForever
 
Tatizo baba yao. Penda sana sifa za kijinga kupeleka pesa na rasilimali zetu kukomboa watu na mataifa uchwara yasiyo nashukran eti akidhani ataacha legacy. Matokeo yake Kaambulia tu jina...r
Umeandika upuuzi gani huu?

Kwako tatizo la Nyerere ni kusaidia nchi nyingine kupata uhuru wao?

Wewe unaona sifa ni kuliibia taifa kama wanavyofanya hawa waliopo sasa hivi wanaokula kwa urefu wa kamba zao?

Nyerere kutowarithisha watoto wake vyeo huko CCM na serikalini kama wanavyofanya hawa wezi waliopo sasa anaonekana mjinga!

Una akili fupi sana.
 
Tatizo baba yao. Penda sana sifa za kijinga kupeleka pesa na rasilimali zetu kukomboa watu na mataifa uchwara yasiyo nashukran eti akidhani ataacha legacy. Matokeo yake Kaambulia tu jina lake kubakia kwenye vibarabara uchwara vya uchochoroni kwenye hizo nchi. Na huku kwetu katuachia mifisi na mchwa inatafuna nchi kwa fujo bila aibu.

#MboweSiyoGaidi

#MboweForever
Kaacha legacy ndio kwani uongo?
 
Back
Top Bottom