Umaskini tunauletaga wenyewe mda ungine.
Yani hapo ni sawasawa una shida umeenda benki alafu wao wanakuambia uwape 8M bure bure.
Hapo ni sawa umewapa benki 8M bure tu bila ya wao kufanya kazi yeyote ile
Tupe formula ya kucalculate time value for money.Unajua maana ya Time value for money??
Wewe kwa akili yako unadhani millioni 9 ya leo uliokopa ni sawa na millioni 9 ya miaka 6 ijayo utakayorudisha?
Inategemea mkuu!! Kuna watu wana mikopo benki tofaut na wametoka kimaisha tu na wapo vizur na marejesho wanafanya kama kawaida!! Kukurudsha nyuma ni dosari tu imetokea ila mkopo ukikuendea vizuri, unakua pazuri! Ni Risky lakin mda mwingnMikopo inarudisha nyuma sana.
Lamakusudi huambiwi Pole. Ungeliachana na hiyo inshu yakukopa umaskini ungelikujia vipi.Mkopo NMB : Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !
Umaskini hauishi kamwe.
Kabla sijaweka formula. Nikikuambia uchukue leo 500000tsh na nikikuambia nikupe hiohio 500000tsh baada ya miaka miwili. Utachukua ipi?Tupe formula ya kucalculate time value for money.
Kaka kakuambia anakatwa 250,000 kwa miaka 6 hivyo ukichukua 250,000 x 12 x 6= 18,000,000 najua hesabu ni ugonjwa wa taifa hivyo nakusameheHuu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya
Mkuu fafanua vzr mana mwezi ujao na mpango wa kukopa kwa hao majamaa.Mkuu haya mabank sio salama kabisa kwa wafanyakazi, nilikopaga benki ya posta, hayo makato yake ...mpka Leo sitamani kukopa tena
Fafanua chief, kwann huna hamu tena? Mana saiv una nyumbaNilikopa nikanunua nyumba ila sina hamu tena.
Kweli hesabu janga la taifa [emoji23][emoji23][emoji23] pitia upya calculation zako kabla hujamzodoa mdau [emoji23][emoji23][emoji23]Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya
Mmmh, matajiri wengi wa kitanzania wanadaiwa sana na mabenki na hivyo vikoba na kila aina ya taasisi za fedha na wengi sana hawalipi mana wakilipa watafilisika kabisa....bank na mikopo ipo kwa ajili ya kumsaidia mtu/kampuni, tatizo hapa bado kuna uholela. Mabank ya kibiashara si sehemu nzuri sana kukopa kama unahitaji kujifanyia maendeleo binafsi. Mabenki ya ushirika (credit unions) na vicoba au ndugu, ni sehemu nzuri kukopa kwa ajili ya kujiendeleza (bila kuhusisha biashara)
So hapo ni asimilia ngapi ?