Mkopo NMB: Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Mkopo NMB: Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Status
Not open for further replies.
8 au 9?
Umaskini tunauletaga wenyewe mda ungine.

Yani hapo ni sawasawa una shida umeenda benki alafu wao wanakuambia uwape 8M bure bure.

Hapo ni sawa umewapa benki 8M bure tu bila ya wao kufanya kazi yeyote ile
 
Mikopo inarudisha nyuma sana.
Inategemea mkuu!! Kuna watu wana mikopo benki tofaut na wametoka kimaisha tu na wapo vizur na marejesho wanafanya kama kawaida!! Kukurudsha nyuma ni dosari tu imetokea ila mkopo ukikuendea vizuri, unakua pazuri! Ni Risky lakin mda mwingn
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Tupe formula ya kucalculate time value for money.
Kabla sijaweka formula. Nikikuambia uchukue leo 500000tsh na nikikuambia nikupe hiohio 500000tsh baada ya miaka miwili. Utachukua ipi?
 
Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya
Kaka kakuambia anakatwa 250,000 kwa miaka 6 hivyo ukichukua 250,000 x 12 x 6= 18,000,000 najua hesabu ni ugonjwa wa taifa hivyo nakusamehe
 
1. Tatizo la wakopaji wa TANZANIA wamekwisha kuwa addicted na mikopo

2. Anakopa mkopo benki wa muda mrefu tena ni mfanyakazi na haachi nafasi ya dharura kwenye mshahara wake na baada ya muda anakwenda kwenye vikundi kule nako anaelemewa anakimbilia kwa wale watu binafsi ambao hata viwango vyao vya riba havipo dunia hii na hushikilia mpaka kadi za benki.

3. Akifika kwenye taasisi ya kukopesha yeye maswali yake ni mawili tuu NITAPATA KIASI GANI na NATAPATA LINI

4.Yale masharti yaliyopo kwenye mkataba wa mkopo kama riba kwa mwezi, ada ya mkopo, bima na processing fees haulizi wala hana muda huo na afisa mkopo hawezi kumwambia

5. Taasisi nyingi za kibepari zinazokopesha zinatumia deminishing method katika riba tuu na sio principal hivyo ukienda maamuma wakikuambia reducing method unaingia kichwa kichwa kumbe, wameweka mtego wanajua katika miaka yote 6 huwezi kuvumilia iishe bila kurudi kwao kuomba fedha tena..ndipo unaingia kwenye mtego uitwao TOP UP. Hapo tayari wanakuwa wameshavuna riba yao yoote inabaki pricipal wanakuweka tena kifungo kingine tena unakuta masharti ya riba yalishabadilika wee huna habari

6. Hapo bado hujamkatia afisa mikopo ili akufanyie fasta ukalipe furushi la madeni mengine unayodaiwa....hapo unaununua umaskini unajiona hivi hivi. Fanya tafiti kabla ya kukopa usisukumwe na shida zako..utajuta utakuwa unawafanyia kazi tuu hela yoote wanachukua
 
kiufupi huo mkopo uko fair,ungekua mkopo wa mda mfupi mfano mwaka rejesho lingeweza kuchezea kwenye milioni kila mwezi
 
Tatizo formula za mikopo ya kibongo siyo reducing balance yaani % iwe kwa kila kiasi kilibaki kwa kila mwezi
 
Mkuu haya mabank sio salama kabisa kwa wafanyakazi, nilikopaga benki ya posta, hayo makato yake ...mpka Leo sitamani kukopa tena
Mkuu fafanua vzr mana mwezi ujao na mpango wa kukopa kwa hao majamaa.
 
Nilikopa nikanunua nyumba ila sina hamu tena.
 
Nimewaza ni lini Tanzania itakuwa na kiongozi kama gadaffi, haya mambo ya riba tungeyasikia kwenye redio tu. R.I.P Gadaffi sijui uliwaza nini kuondoa riba kwenye benki zote za Libya. I hope hata Bongo inawezekana hiyo 100%
 
...bank na mikopo ipo kwa ajili ya kumsaidia mtu/kampuni, tatizo hapa bado kuna uholela. Mabank ya kibiashara si sehemu nzuri sana kukopa kama unahitaji kujifanyia maendeleo binafsi. Mabenki ya ushirika (credit unions) na vicoba au ndugu, ni sehemu nzuri kukopa kwa ajili ya kujiendeleza (bila kuhusisha biashara)
Mmmh, matajiri wengi wa kitanzania wanadaiwa sana na mabenki na hivyo vikoba na kila aina ya taasisi za fedha na wengi sana hawalipi mana wakilipa watafilisika kabisa.
Wanachofanya ni kuachia dhamana zao walizokopea ziuzwe na mabenki.
Mabenki mengi yanapata hasara hapo wananufaika na riba kubwa lakini sio faida ya marejesho toka kwa wafanyabiashara.

Hua nashangaa sana sisi waafrika kutumia ile mifumo isiyo na manufaa kwa wengi toka kwa wakoloni na mabeberu lakini Yale ya muhimu tunayaacha tunaweka siasa .
Ningekua rais ningefuta mabenki yote ya kinyonyaji na kuweka Islamic Benki. Vinginevyo washushe riba mpaka 4%.
 
ukichukua mil 18-mil 9 (uliokopa) ni kuwa unalipa 100% riba. mil 9 kama uko mkoa unajenga nyumba kubwa tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom