Mkurugenzi Rombo: Shule iliyoandikisha Wanafunzi Watatu hakuna imani za kishirikina ni maamuzi ya wazazi tu

Hata Moshi Vijijini kuna shule zimekosa wanafunzi wa Darasa la kwanza miaka miwili mfululizo.
Hili nalijua vizuri sana
 
Anayosema ni kweli, wakazi wengi WA rombo wamehamia mijini, shule nyingi zimeshafungwa Kwa kukosa wanafunzi, mfano Kirwa, Amrushu, Kiungwe ipo njiani, na kama hiyo mlembea
Sahihi.
Wadau wasiojua hawawezi kuamini.
Shule zao watoto ni wengi sana
 
Mbona kama kuna viashiria vya ukweli kwenye hoja ya

Sababu zipo kadhaa, baadhi ni Wazazi wengi kuwapeleka Watoto wao kwenye Shule za binafsi, pia maeneo ya mipakani kuna Wazazi wanapeleka Watoto wao kwenda kusoma Kenya.

===== Huu ni UWONGOOOO.

Private Kuna wanaopeleka lakini ,ni wachache mnooo, na haina impact kubwa.

=======

Kwa kuwa tuna ujirani mwema kuna magari yanayokuja kubeba Wanafunzi wanaenda huko kusoma kisha jioni wanawarudisha.
======
Huu ni UWONGOOOO, UWONGO kabisa asilimia 200.

======

Sababu nyingine ni kuwa ‘population’ sio kubwa sana hapa na Watu wengi wamesambaa na wanasambaa hivyo kusababisha baadhi kuwahamisha Watoto wao pia.
======

Huu ndio ukweli HALISI,.

=====

Kingine ni kuwa Kilimanjaro watu wamesoma sana na hivyo suala la kuzaa Watoto wengi sio jambo linalopendelewa sana kama ilivyo maeneo mengine, watu wengi wana Watoto chini ya watatu au wawili.

=======

Huu ni UWONGOOOO UWONGO kabisa asilimia 5000.
 
Huu uzi uishie hapa...Umemaliza kila kitu Watoto wengi wapo private schools
 
Moja Kati ya DED viazi waliyopo nchi hii ni huyu Chacha. Na amedumu sana hapo Rombo.

Mambo ni zig zag.




Angalia Umbali hizi shule zilipo tokea Moshi Mjini ambapo ndio makao makuu ya mkoa.
Ni karibu sana na Mjini.


Hao ni Darasa la 4 walioanza shule miaka 4 iliyopita means kuna baadhi ya hizo shule hazina Class One kwa sasa.

Wazazi wanaojitahidi kwa sasa Huko Kilimanjaro ni wale waliopo maeneo ya milimani.

Wao bado wanajuhudi za kuzaliana.
 

Attachments

  • Screenshot_20240112-095615.png
    62.4 KB · Views: 3
Lete Ukweli wako mkuu.
 
Lete Ukweli wako mkuu.
UKWELI ni kwamba Kilimanjaro hakuna FURSA na maisha ni MAGUMUUUUU.

Mkoa hakuna anayehamia, isipokuwa kila siku wenyeji WANAHAMA. Huku ukikuta mgeni labda mfanyakazi na yeue anatafuta kuhama kila siku.

Huku wachagga wanarudi sikukuu na mwisho wa mwaka.

Pia, shule ni nyingi kutokana na Kilimanjaro ni kimkoa kidogo mnoooo.

Mfano halisi wa hiyo tarafa ya Mashati, ukubwa wake sehemu nyingine ni Kama KIJIJI tu
Sasa Ina kata 6, na kila kata ina sekondari na shule za msingi wakati hakuna watu, wakusoma


Kilimanjaro wanaobaki ni wazee tu na vijana wasio na pa kwenda, ambao wengi ni bodaboda.

Rombo pia kuna tatizo zito la.ulevi ambalo huyo DED anakwepa kulisema ili asiwaudhi wachagga, anawasifia eti wamesoma ndio maana Wana watoto wachache jambo ambalo ni UWONGO kabisa.

Ni kwamba narudia, watu wa Kilimanjaro wengi wako mikoa mingine na wtoto wao wanasoma huko.
 
Watu wa milimani wanaendekeza sana ushirikina na kustarehesha watalii mpaka hawataki kusoma.
 
Kama hujafika kule utaamini stori za kuhadisiwa Ila wazawa tunajua tangu miaka ya 90 hata huo
Tangu miaka ya 90 hata hayo Mambo ya ulevi hayajachanganya na bado shule zilikuwa na wanafunzi wachache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…