TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

Kauliza wana JF na bila shaka yuko sahihi. Au wewe umeona amemuuliza marehemu? Siku zote binadamu atakuhukumiwa kwa matendo aliyotenda akiwa hai.
Sasa hakuwa au alikuwa inafaida gani Kwa marehemu?
 
Mungu aipumzishe roho yake Charles Hillary, mahali pema peponi. Aimina.

Yaani Hillary amefariki kimasikhara hivi kweli? Hapa lazima kuna kitu sio bure. Haiwezekani mtu hajamaliza hata mwaka tangu aingie ikulu anafariki kizembe hivi. SMZ lazima watueleze vizuri namna mtanganyika huyu alivyofariki. Hapa bara kuna wazanzibar kibao wameteuliwa na Samia kushika nyadhifa nyeti, mbona wao hawafariki kirahisi hivi?

Kuna umuhimu wa kuita chombo huru, kama vile Scotland Yard, waje wachunguze chanzo cha kifo hiki. Hatuwezi kuridhika tu kwa maneno mepesi kuwa 'amefariki ghafla' ikaishia hapo. Lazima twende mbali zaidi. Mbona wazanzibar waliorundikana hapa Tanganyika wao hawafariki ghafla? Acheni ujinga wenu nyie wala urojo!
 
Lakini mwendazake Chaz alikua mzanzibar. Tanganyika alikua muamiaji tu nae
 
Charles na mzanzibari mbona mkuu.
 
Namkumbuka Kama mmojawapo wa waanzilishi wa jina ‘Kitimoto’ akimaanisha mdudu, aka pork aka mnyama!
Charanga time uliitendea haki, na ulitufanya tukaanza kuzipenda radio za nyumbani tena wakati ulipokuwa radio one na kina Abdala Majura!
 
Huyu alikuwa sio mwenzetu!

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini
Katika kumsikiliza kote hii taarifa sikuwahi kuipenda na kuanzia hapo nikampotezea... Ila walikuwa wakikutana na Marehemu Chilambo au Juma Nkamia (kabla hajawa chizi) au Ryongo wakiwa wanakutangazia kandanda utawapenda.
 
Katika kumsikiliza kote hii taarifa sikuwahi kuipenda na kuanzia hapo nikampotezea... Ila walikuwa wakikutana na Marehemu Chilambo au Juma Nkamia (kabla hajawa chizi) au Ryongo wakiwa wanakutangazia kandanda utawapenda.
Nani alikuwa chizi kati ya uliowataja mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…