TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

hivi hilo jina lake la ubini hilary ni kama hilary clinton au limekuwa Christianized kama zitto badala zito, omary badala omari, ally badala ya ali, …
 
1746948944089.jpeg
 
Nimesikitika sana,apumzike kwa amani,Dunia ina siri sana
 
Zanzibar ile jamii siwaamini hata kidogo, huyu hakuwa mzee hata kidogo alikuwa kijana kabisa huyu miaka 66 bado alikuwa mwamba.

Yale majitu ya Zanzibar kule yana roho za husuda na ubaguzi na watu wa Tanganyika,yapo radhi hata yakudhuru,sijui yapoje.

Why mtu aanguke ghafla tu. Mmmmmm mimi huu msiba kiukweli sijaupokea kama ni wa kawaida, una walakini.
Na wewe umeamini aliezaliwa mwaka 1968 atakuwa na miaka 66?

Nimeshangaa hata mmoja halioni hilo

Mda ukifika lazima uchomoke
 
Kipindi kile wanatangaza mpira kupitia idhaa ya kiswahili ya bbc yeye na kikeke walikuwa wanatupa namba ya kutuma sms na ikiwafikia wanaisoma siku moja niliandika sms na akaisoma nilikuwa dukani kwangu aisee nilifurahi sana R.I.P Charles bwana nkangwa
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Hilary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini

Alijiunga na Redio Tanzania mwaka 1981 na kuitumikia hadi mwaka 1994 alipojiunga na kituo binafsi cha Radio One Stereo kinachomilikiwa na IPP

Mwaka 2003 aliondoka nchini na kujiunga na Radio Deusch Welle (DW) nchini Ujerumani, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akiwa Idhaa ya Kiswahili

Mwaka 2015 aliamua kurejea nchini na kujiunga Azam Media ambako alifanya kazi hadi mwaka 2023. Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

Mungu amweke mahala pema peponi mzee wetu.
Apumzike kwa Amani
 
Back
Top Bottom