TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

Huyu alikuwa sio mwenzetu!

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini
Na Watanganyika tukakaa kimya. Uliona wapi nchi ndani ya nchi? Achilia mbali mambo ya Vatican, San Marino.
Hili no tamko very fair Kwa kazi yakr

Hatq sisi tuna ardhi nchi nyingi sana tu

Zambia pekee tuna zaidi ya viwanja 10 Lusaka Tena prime areas

Hapo yeye amesoma taarifa ya umiliki wa ardhi ya smz huko bagamoyo

Ulitaka asemeje? Mbona tunakua wajinga aana siku hizi?
Nadhani wewe unazungumzia umiliki wa ardhi kupitia embassy na huwa ni plots siyo farms.
 
R.I.P Charles Hillary,hakika tutakukumbuka daima kwa kazi nzuri,poleni wanahabari wote duniani🙏🙏🙏
 
Hivi Zuhura Yunusi yuko wapi?

Mpuuuzi kweli yule, yani kaacha BBC kaja kutumia na chura kiziwi, ona sasa hata kusikaka hamna na bado kijana tu
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Charles pia aliwahi kuwa mtumishi mwandamizi wa Azam Media Limited kati ya mwaka 2015 na 2023.

Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Hilary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Mtangazaji huyo wa zamani kinara wa Azam News na Mkuu wa UFM Redio ana historia ndefu katika utangazaji akiwa amevitumikia vituo mbalimbali vya habari ikiwemo Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati huo ikiitwa Redio Tanzania na Shirika la Utangazaji wa Uingereza (BBC).


Mungu amweke mahala pema peponi mzee wetu.

RIP
Amina
 
Hivi Zuhura Yunusi yuko wapi?

Mpuuuzi kweli yule, yani kaacha BBC kaja kutumia na chura kiziwi, ona sasa hata kusikaka hamna na bado kijana tu
Crimea acha zako mama tupo naye mpaka baadaye sana.
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Hilary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini

Alijiunga na Redio Tanzania mwaka 1981 na kuitumikia hadi mwaka 1994 alipojiunga na kituo binafsi cha Radio One Stereo kinachomilikiwa na IPP

Mwaka 2003 aliondoka nchini na kujiunga na Radio Deusch Welle (DW) nchini Ujerumani, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akiwa Idhaa ya Kiswahili

Mwaka 2015 aliamua kurejea nchini na kujiunga Azam Media ambako alifanya kazi hadi mwaka 2023. Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

Mungu amweke mahala pema peponi mzee wetu.
Taarifa ya Habari AZAM TV ikisomwa na Charles Hilary na Ivon Kamuntu nilikuwa sibanduki kwenye TV. Mwenyezi Mungu amrehemu. Kwakweli tasnia ya Habari aliitendea haki.
 
Ni wale wale Ile issue ya Zanzibar kumiliki eneo upande wa bagamoyo aliishupalia Sana kuandika matangazo na kuyapost na kwenda kwenye media ngoja af

Hana shukrani. Elimu, kuanzia primary, kazi, jina na maisha kayapatia Tanganyika. Halafu uzeeni anainyea Tanganyika.

Bila RTD angepata kazi DW na BBC ?
 
Na Watanganyika tukakaa kimya. Uliona wapi nchi ndani ya nchi? Achilia mbali mambo ya Vatican, San Marino.
Nadhani wewe unazungumzia umiliki wa ardhi kupitia embassy na huwa ni plots siyo farms.
Bado ni mali waliyopata kihalali
 
Alikuwa akipelekwa Muhimbili ,ina maana huko zanzibar hakuna hosp kubwa?
 
Mkuu mbona unamshambulia mtu kauliza kiungwana kabisa? Kauliza swali zuri sana na hajahukumu chochote. By the way, binadamu kutoa opinion kuhusu marehemu SIYO kuhukumu. Hivi unadhani mtu akisema fulani kipindi cha uhai wake alikuwa ni mwizi, atakuwa ametoa hukumu? Yale yatabaki kuwa maneno yake, na mbele ya haki atahukumiwa kulingana na ukweli wa aliyoyatenda. Hata kama dunia nzima itaimba sifa za marehemu, Mungu anaweza kutoa hukumu ya tofauti.

Sahihi kabisa
 
Kwahy jamaa bado n mkurugenzi huku akiwa mfu? 😂
Ww ndo ujue kuandika Kiswahili vyema.
Nadhani yuko sahihi. Mfano Rais au Mkuu wa majeshi ambaye bado anahudumu (Sitting) tunasema, Mkuu wa Majeshi....... Amefariki dunia au Rais wa Tanzania na Amir jeshi mkuu........ Amefariki dunia kwa ajali ya ndege. Sijui nime eleweka? Kuto kubali ana ni haki ya kila mtu.
 
Back
Top Bottom