Mkurugenzi wa Shule ampiga Mzazi na kitako cha bastola baada ya kuomba uhamisho wa mwanaye

Mkurugenzi wa Shule ampiga Mzazi na kitako cha bastola baada ya kuomba uhamisho wa mwanaye

Mmeanza tena eti
Ukiniambia Unanijua mimi
Nakuwahi
Safari hatuwaogopi mbwa nyie [emoji23]
 
Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Mkurugenzi wa shule ya Sun Academy, Nguvu Chengula, kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi Alifa Mkwawa, ambaye ni mzazi, kwa kutumia kitako cha bastola baada ya kuombwa uhamisho wa mtoto anayesoma katika shule hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Allan Bukumbi, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 6:00 mchana maeneo ya shule hiyo iliyopo mtaa wa Mawelewele ambapo chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokana na mtuhumiwa kugoma kutoa uhamisho wa mtoto wa mlalamikaji kwa kile kinachodaiwa kuwa hajalipa ada ya mtoto huyo.

Chanzo: EATV
Kamtishia bastola ana kesi ya kujibu huyo.
 
Kuna mijitu mingine sijui serikali huwa inatumia formular gani kuipa silaha.
 
Dadeeeki, Kuna Watu Wana roho ngumu sana, inasemekana Mzazi kaenda kuomba uhamisho wa mwanae basi unaambiwa Mkurugenzi wa hio Shule ambaye ni Diwani wa CCM wa kutegemewa akachomoa bastola akamtwanga jamaa kwa kitako.

This time CCM wasije wakamkana, huyu ni Kada wao na hii ndio tabia yao

20220517_190017.png

20220517_190009.png
 
Polisi wamehalibu chakula ya ubongo,ajabu wa bastola atatoka na wakulima wa dawa miaka30
 
Matajiri wetu hawa ni wao kila kitu mpaka kufuatilia madeni 🤣🤣🤣 kinachofuata ni majanga kama haya
 
Dunia inaenda spidi, Hao kina Chengula ni wakinga naona pesa walizokamata zimewapa hadi jeuri ya kuwatandika wahehe kina Mkwawa
 
Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Mkurugenzi wa shule ya Sun Academy, Nguvu Chengula, kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi Alifa Mkwawa, ambaye ni mzazi, kwa kutumia kitako cha bastola baada ya kuombwa uhamisho wa mtoto anayesoma katika shule hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Allan Bukumbi, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 6:00 mchana maeneo ya shule hiyo iliyopo mtaa wa Mawelewele ambapo chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokana na mtuhumiwa kugoma kutoa uhamisho wa mtoto wa mlalamikaji kwa kile kinachodaiwa kuwa hajalipa ada ya mtoto huyo.

Chanzo: EATV
Hii shule imeyumba sana kwa sasa tokea jamaa amalize fedha zote kwenye kampeni za ubunge 2020
 
Back
Top Bottom