Kama mtanzania, inawezekana umepata nafasi kufuatilia yanayojiri nchini Scotland kwenye mkutano unaohusu mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi wengi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alihutubia mkusanyiko huo.
Tofauti na nchi kama China, Marekani na India, Tanzania haihusishwi sana kwa kuwa chanzo cha mabadiliko ya tabia nchi. Umuhimu wa kuhudhuria mkutano huo ni kujumuika na viongozi wengine katika kujadili suala hili na kuwa na mchango unaoweza kuleta manufaa chanya kwa miaka mingi ya baadaye.
Your browser is not able to display this video.
Nimebahatika kuanglia hotuba zote za Rais Samia na kwa bahati mbaya au nzuri, aligusia zaidi kwenye umuhimu wa nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi ambazo hazijaendelea kifedha ili kuweza kukabiliana na tatizo hili la mabadiliko ya tabia nchi.
Labda inawezekana kwamba ni kweli Tanzania inahitaji misaada hiyo lakini kwa upande wa pili haipendezi kuona kwamba mawazo haya ya kuendelea kupata misaada imetawala katika vichwa vya viongozi wetu. Kauli kama hizo zinaweza zisizae matunda.
Ingependeza sana kama Rais Samia angejizatiti zaidi katika kuongelea umuhimu wa kuwa na "balance" katika shughuli za maendeleo, maslahi ya binadamu na mikakati ya kulinda mazingira. Kama Tanzania, angezungumzia changamoto zinazo sababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na mipango yetu haswa katika kipindi ambacho tunatamani uchumi wa viwanda.
Kwa nchi zilizoendelea, umuhimu wa sayansi katika kuvumbua njia mpya zisizo chochea uharibifu wa mazingira zinazoweza kutumika kwenye sekta mbali mbali
Hata mimi nilitegemea hivyo kwamba kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni agenda ambayo imeonekana kuwa changamoto, je sisi japo ni nchi changa kiuchumi tuna idea gani tofauti na maalum ambayo mataifa tajiri yangeweza kuipokea au kuichota na kuitumia kupunguza au kutatua changamoto hiyo?
Mnaona aibu kuomba omba? Mnamuonea aibu nani asiyejua nchi hii ni masikini wa kutupwa na inategemea misaada kuendeshwa? Ndiyo hali halisi nchi masikini kama hii haiwezi kumudu mfano tozo ya kupunguza carbon (carbon tax).
Lazima tusaidiwe au mnataka Watanzania wafe na tai shingoni kwa kuona aibu kutembeza bakuli? Ndiyo maana yule aliyepita aliona aibu za kuomba msaada wa kupambana na Covid-19, wengi wakafa kwa ajili hiyo. Tukubali nafasi yetu hapa duniani kama nchi masikini, tunaotegemea misaada miaka 60 tangu tupate uhuru.

Unaweza kuhimiza wananchi lakini kama hela ya kununua gesi hawana ni kazi bure. Wanaopikia kuni na mkaa siyo wanapikia kuni na mkaa kwa kupenda. Wanafanya hivyo kwa sababu ni uwezo wao. Wangekuwa na uwezo wa kupikia na gesi wangefanya hivyo.
Apatapo fursa ya kwenda nje na kutusemea WATANZANIA basi huinuka baadhi na KUMKOSOA na hata KUMZODOA......
Cha ajabu "mabingwa" hao wanasahau kuwa WAZUNGU "walikwiba" raslimali na nguvu kazi ya afrika kwa miaka mingi tu na wana WAJIBU wa kuturudishia baadhi ya "mambo".
Na mambo yenyewe ni hayo MAFUNGU....tuyachukue tu....hakuna haja ya "kutumia falsafa nyingi" katika dunia isiyo na "mzani" Sawa.......
Ni hasara sana kuongozwa na kiongozi anayewaza kuombaomba pasi na kutafuta suluhu.
Mafanikio na maendelea ni kazi na akili kama kiongozi asilimia 80% ya mawazo yake ni kuombaomba hata ashuke malaika Gabriel hatutoboi.
Kubali hatima yako. Resign to your fate. Bila ya kuombaomba utawatesa watu tena utaua. Hakuna lolote utakalotoboa bila ya misaada zaidi ya nguo na viatu vyako kwa uchovu.
Labda inawezekana kwamba ni kweli Tanzania inahitaji misaada hiyo lakini kwa upande wa pili haipendezi kuona kwamba mawazo haya ya kuendelea kupata misaada imetawala katika vichwa vya viongozi wetu.
Kauli kama hizo hazifai na ingependeza sana kama Rais Samia angejizatiti zaidi katika kuwasilisha hoja na kutafuta suluhisho katika janga hili la mabadiliko ya tabia nchi
Mkuu 'DaudiAiko', rais wako alijipambanua toka mwanzo baada ya kuachiwa nchi kwa kuwa wazi kabisa kwamba kwake kipaumbele na njia ya nchi hii kuendelea ni kuomba misaada toka nje.
Alisema, anakuja kufungua nchi, wewe hukuelewa maana yake ni nini?
Hana imani hata kidogo kwamba nchi hii waTanzania wanao uwezo wa kuiendeleza vizuri sana kwa juhudi zao wenyewe iwapo serikali itaweka mipango ya kuwawezesha kufanya hivyo.
Hutasikia hata mara moja akielezea serikali yake inafanya nini ili kuunga mkono juhudi za wananchi katika kujiletea maendeleo yao. Yeye anaamini wananchi hao watapata maendeleo iwapo watu wengine watakuja hapa kuwaletea wananchi maendeleo. Hiyo omba omba ni sehemu muhimu sana kwake kutimiza adhma yake hiyo potofu.
Na usije ukadhani kwamba sitaki wawekezaji au misaada ije "kusaidia" mipango na juhudi zetu wenyewe kujitafutia maendeleo, la hasha, hawa waje, kama wanaleta mitaji yao kuchimba gesi, wakaribishwe, lakini kwa misingi kwamba ni lazima tufaidike na kazi hiyo. Lakini mategemeo haya siyo ndiyo yawe kipaumbele, kana kwamba bila ya hayo kuwepo hatuwezi kujikwamua sisi wenyewe kwa kufanya kwa bidii na maarifa yale yaliyomo kwenye uwezo wetu.
Vipi, tunashindwa hata kulima kwa tija? Huko nako tunahitaji kufungua nchi waje watulimie mazao hapa, miaka zaidi ya sitini ya kuwa huru?
Hatuwezi hata kusimamia elimu yetu itoe raia wenye uelewa wa nini wanaweza kufanya kwa manufaa ya nchi yao?
Mama hana dira, na kwa bahati mbaya hata huko kwenye chama hakuna tena watu wanaotanguliza maslahi ya nchi hii mbele. Imebaki wachumia tumbo tu kama akina Majaliwa, Mwigulu, Januari na wengineo.
Kipenzi chetu mh.Rais SSH anafahamu fika ya kwamba ,Afrika inachangia 4% tu ya HEWA UKAA....
Mh.Rais SSH analijua hilo kuwa ni nchi mbili tu(Afrika ya kusini& Nigeria) ndizo zenye kuchangia zaidi ya 90% ya hiyo 4%.......
Maana yake ni nini ?!!!
Hapa inabidi mtu atulie na kuacha FALSAFA nyingi za KIHISIA zaidi ya UHALISIA alioutanguliza mh.Rais na jopo la wabobezi wake wa masuala ya kidiplomasia......
My take : Kongole kwake mh.Rais SSH kwa kutuwakilisha vyema kimataifa💪👊😍
Unaweza kuhimiza wananchi lakini kama hela ya kununua gesi hawana ni kazi bure. Wanaopikia kuni na mkaa siyo wanapikia kuni na mkaa kwa kupenda. Wanafanya hivyo kwa sababu ni uwezo wao. Wangekuwa na uwezo wa kupikia na gesi wangefanya hivyo.
Ni hasara sana kuongozwa na kiongozi anayewaza kuombaomba pasi na kutafuta suluhu.
Mafanikio na maendelea ni kazi na akili kama kiongozi asilimia 80% ya mawazo yake ni kuombaomba hata ashuke malaika Gabriel hatutoboi.
Mnaona aibu kuomba omba? Mnamuonea aibu nani asiyejua nchi hii ni masikini wa kutupwa na inategemea misaada kuendeshwa? Ndiyo hali halisi nchi masikini kama hii haiwezi kumudu mfano tozo ya kupunguza carbon (carbon tax).
Lazima tusaidiwe au mnataka Watanzania wafe na tai shingoni kwa kuona aibu kutembeza bakuli? Ndiyo maana yule aliyepita aliona aibu za kuomba msaada wa kupambana na Covid-19, wengi wakafa kwa ajili hiyo. Tukubali nafasi yetu hapa duniani kama nchi masikini, tunaotegemea misaada miaka 60 tangu tupate uhuru.
Apatapo fursa ya kwenda nje na kutusemea WATANZANIA basi huinuka baadhi na KUMKOSOA na hata KUMZODOA......
Cha ajabu "mabingwa" hao wanasahau kuwa WAZUNGU "walikwiba" raslimali na nguvu kazi ya afrika kwa miaka mingi tu na wana WAJIBU wa kuturudishia baadhi ya "mambo"...
Mkuu 'DaudiAiko', rais wako alijipambanua toka mwanzo baada ya kuachiwa nchi kwa kuwa wazi kabisa kwamba kwake kipaumbele na njia ya nchi hii kuendelea ni kuomba misaada toka nje...
Hizi ngonjera zako zilimshinda Nyerere akang'atuka urais akamwachia Mwinyi nchi iko hoi kiuchumi.
Naye yule chizi wa Chato akaja na skili za kijinga kama hizi.
Muelewe yule mama mkitaka awapeleke hivi mnavyotaka nyinyi mtakaoumia ni nyinyi, hakuna Rais anayeumia kutokana na nchi kuwa na hali ngumu.
Hata huyo Magufuli baba wa uwongo kama alivyo shetani hajawahi kuwa na maisha magumu tangu singie serikalini achilia mbali Urais, tena yeye ndio kufuru alikuwa anatembea na begi limejaa pesa, anamgawia anayejisikia yeye kumgawia siku hiyo na huku akiwahadaa na kuwadanganya wajinga wenzake kwamba watembee kifua mbele Tanzania ni tajiri kumbe yeye ndio tajiri, na hilo kundi la wajinga wenzake kina Abunuwasi hawa unakuta wengi hawana uhakika wa milo hata miwili tu.