Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Hii dhana ya wazungu kuiba rasilimali za waafrika miaka 60 baada ya kujiendesha wenyewe ni dhalili sana.
Wajibu wetu ni upi kwenye maendeleo ya dunia tutaombaomba mpaka lini??
Fikra na makuzi gani haya?
Huu upuuzi wa kuhemea hemea ni dhana mbovu ambayo inapaswa kupingwa na wote kwa namna zote
🤣🤣🤣Hivi mkuu wangu una madini ardhini.....tunayachimba sisi "in large scale"?!!!

Uwezo huo tunao?!!

Mbali na kuchimba...je kuyanunua(soko la ndani)?!!!

Iko hivi.....

Ili uchimbe madini(kitalu kimoja) kwa kutolegalega na kutopata hasara huna budi kuwekeza DOLA MILIONI 500 mpaka DOLA BILIONI 1....

Fedha zote hizo unaweza kuzipata kutoka MIKOPO YA BENKI YENYE RIBA KUBWA......

Huna viwanda vya kutengeneza yafuatayo halafu unapandwa "mori wa uchungu na jazba tu":- 🤣

✓Wheel Tractor Scrapers
✓Hydraulic Mining Shovels
✓Large Dozers
✓Rotary Drill Rigs
✓Drag Lines
✓Underground Mining Loaders and Trucks
✓n.k n.k n.k

Looo saalaaleeee 🤣🤣

SIEMPRE SSH💪
NCHI KWANZA👊
 
Sasa kama akili ndio hiyo ulitegemea aseme nini? SSH ni extension ya Msoga wanaamini katika kula bata na kuzurula tu.
FB_IMG_16307140795615105.jpg
 
Wanabodi,

Kama mtanzania, inawezekana umepata nafasi kufuatilia yanayojiri nchini Scotland kwenye mkutano unaohusu mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi wengi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alihutubia mkusanyiko huo.

Tofauti na nchi kama China, Marekani na India, Tanzania haihusishwi sana kwa kuwa chanzo cha mabadiliko ya tabia nchi. Umuhimu wa kuhudhuria mkutano huo ni kujumuika na viongozi wengine katika kujadili suala hili na kuwa na mchango unaoweza kuleta manufaa chanya kwa miaka mingi ya baadaye.

Nimebahatika kuanglia hotuba zote za Rais Samia na kwa bahati mbaya au nzuri, aligusia zaidi kwenye umuhimu wa nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi ambazo hazijaendelea kifedha ili kuweza kukabiliana na tatizo hili la mabadiliko ya tabia nchi.

Labda inawezekana kwamba ni kweli Tanzania inahitaji misaada hiyo lakini kwa upande wa pili haipendezi kuona kwamba mawazo haya ya kuendelea kupata misaada imetawala katika vichwa vya viongozi wetu. Kauli kama hizo zinaweza zisizae matunda.

Ingependeza sana kama Rais Samia angejizatiti zaidi katika kuongelea umuhimu wa kuwa na "balance" katika shughuli za maendeleo, maslahi ya binadamu na mikakati ya kulinda mazingira. Kama Tanzania, angezungumzia changamoto zinazo sababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na mipango yetu haswa katika kipindi ambacho tunatamani uchumi wa viwanda.

Kwa nchi zilizoendelea, umuhimu wa sayansi katika kuvumbua njia mpya zisizo chochea uharibifu wa mazingira zinazoweza kutumika kwenye sekta mbali mbali

Mungu ni mwema, wakati wote
Jamaniee, msisahau Rais wetu ni Mwanamke wa kibongo! Kwao maendeleo na kupendwa ni KUOMBA HELA..
 
Apatapo fursa ya kwenda nje na kutusemea WATANZANIA basi huinuka baadhi na KUMKOSOA na hata KUMZODOA......

Cha ajabu "mabingwa" hao wanasahau kuwa WAZUNGU "walikwiba" raslimali na nguvu kazi ya afrika kwa miaka mingi tu na wana WAJIBU wa kuturudishia baadhi ya "mambo".......

Na mambo yenyewe ni hayo MAFUNGU....tuyachukue tu....hakuna haja ya "kutumia falsafa nyingi" katika dunia isiyo na "mzani" Sawa.......

#Kazi Inaendelea Kwa Kasi & Weledi Zaidi 💪👊😍
We lofa kweli,KWA hyo wakupe KWA mkono huu afu wakupe masharti ya kuingiza sheria zao za kishenzi kama ushoga!

Mnateteaga upumbavu sana
 
Huo ndio ukweriiii ndugu zangu
Mnaona aibu kuomba omba? Mnamuonea aibu nani asiyejua nchi hii ni masikini wa kutupwa na inategemea misaada kuendeshwa? Ndiyo hali halisi nchi masikini kama hii haiwezi kumudu mfano tozo ya kupunguza carbon (carbon tax).

Lazima tusaidiwe au mnataka Watanzania wafe na tai shingoni kwa kuona aibu kutembeza bakuli? Ndiyo maana yule aliyepita aliona aibu za kuomba msaada wa kupambana na Covid-19, wengi wakafa kwa ajili hiyo. Tukubali nafasi yetu hapa duniani kama nchi masikini, tunaotegemea misaada miaka 60 tangu tupate uhuru.
 
Wanabodi,

Kama mtanzania, inawezekana umepata nafasi kufuatilia yanayojiri nchini Scotland kwenye mkutano unaohusu mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi wengi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alihutubia mkusanyiko huo.

Tofauti na nchi kama China, Marekani na India, Tanzania haihusishwi sana kwa kuwa chanzo cha mabadiliko ya tabia nchi. Umuhimu wa kuhudhuria mkutano huo ni kujumuika na viongozi wengine katika kujadili suala hili na kuwa na mchango unaoweza kuleta manufaa chanya kwa miaka mingi ya baadaye.

Nimebahatika kuanglia hotuba zote za Rais Samia na kwa bahati mbaya au nzuri, aligusia zaidi kwenye umuhimu wa nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi ambazo hazijaendelea kifedha ili kuweza kukabiliana na tatizo hili la mabadiliko ya tabia nchi.

Labda inawezekana kwamba ni kweli Tanzania inahitaji misaada hiyo lakini kwa upande wa pili haipendezi kuona kwamba mawazo haya ya kuendelea kupata misaada imetawala katika vichwa vya viongozi wetu. Kauli kama hizo zinaweza zisizae matunda.

Ingependeza sana kama Rais Samia angejizatiti zaidi katika kuongelea umuhimu wa kuwa na "balance" katika shughuli za maendeleo, maslahi ya binadamu na mikakati ya kulinda mazingira. Kama Tanzania, angezungumzia changamoto zinazo sababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na mipango yetu haswa katika kipindi ambacho tunatamani uchumi wa viwanda.

Kwa nchi zilizoendelea, umuhimu wa sayansi katika kuvumbua njia mpya zisizo chochea uharibifu wa mazingira zinazoweza kutumika kwenye sekta mbali mbali

Mungu ni mwema, wakati wote
Ukija mkutano mwingine,utakwenda wewe uhutubie.
 
Apatapo fursa ya kwenda nje na kutusemea WATANZANIA basi huinuka baadhi na KUMKOSOA na hata KUMZODOA......

Cha ajabu "mabingwa" hao wanasahau kuwa WAZUNGU "walikwiba" raslimali na nguvu kazi ya afrika kwa miaka mingi tu na wana WAJIBU wa kuturudishia baadhi ya "mambo".......

Na mambo yenyewe ni hayo MAFUNGU....tuyachukue tu....hakuna haja ya "kutumia falsafa nyingi" katika dunia isiyo na "mzani" Sawa.......

#Kazi Inaendelea Kwa Kasi & Weledi Zaidi [emoji123][emoji109][emoji7]
Umeelezea vizuri sana.Nafikiri itakuwa wamekuelewa,japo watajifanya hawajakuelewa.
 
Yeye anafahamu fika....

Kipenzi chetu mh.Rais SSH anafahamu fika ya kwamba ,Afrika inachangia 4% tu ya HEWA UKAA....

Mh.Rais SSH analijua hilo kuwa ni nchi mbili tu(Afrika ya kusini& Nigeria) ndizo zenye kuchangia zaidi ya 90% ya hiyo 4%.......

Maana yake ni nini ?!!!

Hapa inabidi mtu atulie na kuacha FALSAFA nyingi za KIHISIA zaidi ya UHALISIA alioutanguliza mh.Rais na jopo la wabobezi wake wa masuala ya kidiplomasia......

My take : Kongole kwake mh.Rais SSH kwa kutuwakilisha vyema kimataifa[emoji123][emoji109][emoji7]

#Huo Mpunga uje tu

#Siempre JMT
Hotuba yake ni nzuri.Hakuna nchi duniani isiyopokea misaada,nchi zote duniani zinapewa na kupokea misaada.
 
Mkuu 'DaudiAiko', rais wako alijipambanua toka mwanzo baada ya kuachiwa nchi kwa kuwa wazi kabisa kwamba kwake kipaumbele na njia ya nchi hii kuendelea ni kuomba misaada toka nje.

Alisema, anakuja kufungua nchi, wewe hukuelewa maana yake ni nini?

Hana imani hata kidogo kwamba nchi hii waTanzania wanao uwezo wa kuiendeleza vizuri sana kwa juhudi zao wenyewe iwapo serikali itaweka mipango ya kuwawezesha kufanya hivyo.

Hutasikia hata mara moja akielezea serikali yake inafanya nini ili kuunga mkono juhudi za wananchi katika kujiletea maendeleo yao. Yeye anaamini wananchi hao watapata maendeleo iwapo watu wengine watakuja hapa kuwaletea wananchi maendeleo. Hiyo omba omba ni sehemu muhimu sana kwake kutimiza adhma yake hiyo potofu.

Na usije ukadhani kwamba sitaki wawekezaji au misaada ije "kusaidia" mipango na juhudi zetu wenyewe kujitafutia maendeleo, la hasha, hawa waje, kama wanaleta mitaji yao kuchimba gesi, wakaribishwe, lakini kwa misingi kwamba ni lazima tufaidike na kazi hiyo. Lakini mategemeo haya siyo ndiyo yawe kipaumbele, kana kwamba bila ya hayo kuwepo hatuwezi kujikwamua sisi wenyewe kwa kufanya kwa bidii na maarifa yale yaliyomo kwenye uwezo wetu.

Vipi, tunashindwa hata kulima kwa tija? Huko nako tunahitaji kufungua nchi waje watulimie mazao hapa, miaka zaidi ya sitini ya kuwa huru?

Hatuwezi hata kusimamia elimu yetu itoe raia wenye uelewa wa nini wanaweza kufanya kwa manufaa ya nchi yao?

Mama hana dira, na kwa bahati mbaya hata huko kwenye chama hakuna tena watu wanaotanguliza maslahi ya nchi hii mbele. Imebaki wachumia tumbo tu kama akina Majaliwa, Mwigulu, Januari na wengineo.
Tena hakuna kiongozi mbaya kama mzee wa namungo na nimemdharau sana inaonekana ni mrafi sana sana
 
Hakuna Taifa,wala binadamu,asiyetaka msaada,msaada upo wa kifedha,kimawazo,kuonyeshwa njia,kupewa fikiria.Ni mjinga peke yake ndio,anaweza kuishi kwa kuona aibu,kuomba msaada.Hata wewe mleta mada,hapa uko JF,unatoa mawazo yako,umesaidiwa na aliyanzisha hii forum,wewe kuweza kutoa mawazo,ungekuwa na forum yako,kama hutaki kusaidiwa.
 
Wanabodi,

Kama mtanzania, inawezekana umepata nafasi kufuatilia yanayojiri nchini Scotland kwenye mkutano unaohusu mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi wengi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alihutubia mkusanyiko huo.

Tofauti na nchi kama China, Marekani na India, Tanzania haihusishwi sana kwa kuwa chanzo cha mabadiliko ya tabia nchi. Umuhimu wa kuhudhuria mkutano huo ni kujumuika na viongozi wengine katika kujadili suala hili na kuwa na mchango unaoweza kuleta manufaa chanya kwa miaka mingi ya baadaye.

Nimebahatika kuanglia hotuba zote za Rais Samia na kwa bahati mbaya au nzuri, aligusia zaidi kwenye umuhimu wa nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi ambazo hazijaendelea kifedha ili kuweza kukabiliana na tatizo hili la mabadiliko ya tabia nchi.

Labda inawezekana kwamba ni kweli Tanzania inahitaji misaada hiyo lakini kwa upande wa pili haipendezi kuona kwamba mawazo haya ya kuendelea kupata misaada imetawala katika vichwa vya viongozi wetu. Kauli kama hizo zinaweza zisizae matunda.

Ingependeza sana kama Rais Samia angejizatiti zaidi katika kuongelea umuhimu wa kuwa na "balance" katika shughuli za maendeleo, maslahi ya binadamu na mikakati ya kulinda mazingira. Kama Tanzania, angezungumzia changamoto zinazo sababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na mipango yetu haswa katika kipindi ambacho tunatamani uchumi wa viwanda.

Kwa nchi zilizoendelea, umuhimu wa sayansi katika kuvumbua njia mpya zisizo chochea uharibifu wa mazingira zinazoweza kutumika kwenye sekta mbali mbali

Mungu ni mwema, wakati wote

Kwanza sio kila mikutano lazima aende kuhudhulia. Mikutano mingine unaangalia Ina tija gani kwa Taifa letu. Kwenda ktk mikutano kama huo ni matumizi mabaya ya pesa Yetu ya tozo. Angemtuma balozi wetu wa huko au aliye kalibu na hapo Kwenda kumuwakilisha
 
Acha akomae na hizo hela, hawa mabeberu lazima uende na uzungumze nao na kupambania nchi yako ipate hela,ukijifanya kiburi etc hupati.na hiyo ni misaada na mikopo ya riba nafuu au ulitaka akomae hapa akope mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa, unaambiwa kila mwaka kuna zaidi ya $ billioni mia moja, kwaajili hiyo, sasa nchi zetu maskini unataka tususe
FB_IMG_1635836376672.jpg
 
Mkuu usitake mama kufanya vitu ambavyo hana uwezo navyo huo ndo uwezo wake kutembeza bakuri a.k.a ombaomba
 
Kwanza sio kila mikutano lazima aende kuhudhulia. Mikutano mingine unaangalia Ina tija gani kwa Taifa letu. Kwenda ktk mikutano kama huo ni matumizi mabaya ya pesa Yetu ya tozo. Angemtuma balozi wetu wa huko au aliye kalibu na hapo Kwenda kumuwakilisha
Ataachaje kwenda na Waswahili mnavyopenda kudhurura. Akirudi tu tumeishampangia safari ya kwenda kutembea jamaica.
 
Wafugaji wamejaa maporini wanafyeka misitu/mapori eti wanyama wao wasipotee, hakuna anaejali! Wenye mamlaka wako bize na machinga! Bado mapori ya akiba/tengefu kwa ajili ya kuhifadhi mazingira mnawagawia wananchi wafyeke waishi! Ina maana Mwalimu alikuwa mjinga kuyatenga? Aisee yaani afrika haina viongozi ndiyo maana tramp alikuwa anawadharau sana! Yaani ni mizigo! Ndiyo haibebeki! Mapori yanateketea halafu wanaenda ulaya sijui kusema nini! Sisi wakulima tunasikitika sana!
 
Back
Top Bottom