Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Anayepeleka hizo gunia za mahindi Kenya ni nani?Njoo na mfano wenye mantiki.
 
Unaweza kuhimiza wananchi lakini kama hela ya kununua gesi hawana ni kazi bure. Wanaopikia kuni na mkaa siyo wanapikia kuni na mkaa kwa kupenda. Wanafanya hivyo kwa sababu ni uwezo wao. Wangekuwa na uwezo wa kupikia na gesi wangefanya hivyo.
Punguza bei.

Weka mazingira ya bei ya gesi na umeme kuwa ya chini ndipo wananchi wataachana na kutumia mkaa!

Samia alitakiwa aeleze mambo kama hayo, kwamba dunia isaidie kuweka nishati mbadala kwenye nchi ambazo bado uharibifu haujatokea kwa kiasi kikubwa kama tz ili wananchi wasiendelee kubaribu mazingira.

Na pia angekuja hata na mawazo kwamba wamsaidie hela za kufanya mikakati ya upandaji miti.

Sasa eti tusaidieni hela za kupambana na athali za mabadaliko ya tabia ya nchi! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu huo usumbufu ndio umepitana kiwango.Wengi wetu ni mateso tu.
 
Mada inaongea mambo mengine wewe unaleta habari za Magufuli!

Huyu mtu bado anakuchapa hata baada ya kufa?

Au ni hicho kibendi chake alichokuachia? Bado miezi mingapi ukishushe?
 
Kwani hizo fedha watakazotusaidia kupambana na MABADILIKO YA TABIA YA NCHI hayatohusisha NA HAYO YA UPANDAJI MITI ?!!!

GESI YA MTWARA + BWAWA LA UMEME MWALIMU NYERERE linakwenda kutuinua zaidi💪
 
Kabisa unaamini Tanzaia inaweza kulazimisha hizo ncho zilizoendelea? Unaota?
We huoni mama Samia kila sentensi anaweka neno naomba
Yaan wao waharibu kwa 75% afu sisi ndio tuwaombe tena. Namic sana viongozi kama kina Ghadafi, shavez, Mugabe, waliokuwa wanasema ukweli sio kuomba omba tu.
 
Rais gani nchi hii alituongoza bila ya KUOMBAOMBA NA KUKOPAKOPA?!!!

Yupi huyo unitajie hapa?!!!
Heri kukopa kuliko ombaomba. Unapokopa unaonesha unauwezo wa kurejesha. Ombaomba utafanywa chochote. Kukopa hata nchi tajiri ukopa. Marekani, Ufaransa, Italy na nyinginezo zinamadeni kibao, kwa kukopa.
Ombaomba, ni kutokuwa na akili za ya kufikiri njia nyingine ya kumaliza au kukabiliana na tatizo.
Tanzania hatuna uharibifu mkubwa wa mazingira. Hivyo unapoomba hizo fedha hata wao wanaangalia na kucheka tu.
Katika uharibifu wa mazingira kuna sheria ya "Polutor pay system" hivyo Tanzania hatumo. Hela za nini, tusiwe tunajidhalilisha. Uwezo wa kutunza mazingira yetu bado tunao sisi wenyewe. Shida serikali haijui kupanga miji yetu. Wao wanadhani kujenga kila sehemu ndo maendeleo. Där es Salaam haina sehemu ya kupumlia, hakuna Park au bustani kubwa za miti katikati ya mji hata pembezoni.
Tanzania tunachojua ni kukatamiti na kujenga. Dar nzima utatembea na miji mingine hakuna hata benchi la kukaa mtu apumzike.
Wakati wa Nyerere alijaribu kuimarisha Park ktk miji kadhaaa lkn baadae ziligeuzwa viwanja kujenga.
Sasa tunachoomba ni nini wakati hatujui hata kutunza mazingira. Serikali ni waongo tu ndo maana fedha ya Uviko wao wanajengea madarasa. Wakati walisema tozo itajenga. Hizo fedha zingetumika kuboresha afya.
Watanzania tunapenda ushabiki, badala ya kumshauri kiongozi nini kifanyike chenye maslahi ya Taifa. Na kubwa wataalam wetu wanacopy na kupaste taarifa na hotuba. Ni wavivu kufikiria jumbo jipya. Hivyo kama Rais si mfuatiliaji atajikuta anajikita yaleyale. Kuomba fedha ni falsafa ya nchi za Afrika zikidhani hela ndo suluhisho kwa kila kitu. Hata wakipewa hazitumiki ktk kusudio lililoombewa.
Ndo maana wazungu wanatudharau na kutucheka kuwa tunafikiria hela na misaada kila wakati.
 
Tatizo ni kwamba viongozi wetu wanafyata mkia tu hawajui hali inayoendelea na nini kifanyike hadi Ulaya na Amerika watuambie. Badala ya kuendelea kupoteza matrillioni ya maskini kujenga bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga, tungepaswa kuwekeza kwenye miradi ya nishati safi/jadidi kama vile solar, wind, n.k. Ni muda mfupi sana wa kutumia petrol/dizel umebaki tunapaswa kuwekeza kwenye miundombinu ya renewable energy kwa ajili ya magari/engine za umeme na hydrogen manake huko ndipo tunapoelekea tupende tusipende.
 
Kwani Kuna UTAWALA ambao haukuwahi KUWAFURAHISHA WANANCHI kwa miradi hiyo "ukosoayo"?!!!

Watawala nao ni wanasiasa.....yako mambo mengi mazuri WANAYOTUFANYIA ila kumbuka jamii na raia nao ni binadamu WENYE HISIA/WANAOKWENDA KIHISIA....unataka mtawala awe tofauti sana na HULKA ya jamii yake imzungukayo?!!!

Utampatia wapi huyo mtawala?!!

Kama nchi tumepiga hatua kubwa kimaendeleo......tatizo baadhi yetu ni LABDA KUYAFANANISHA MAENDELEO HAYO NA NCHI ZILIZOPIGA HATUA ZAIDI YETU.........


SIEMPRE JMT
NCHI KWANZA
 
Ninadhani kuhimiza wananchi kutumia majiko ya gesi na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ingekua ni jambo la kujadili ndipo kuomba msaada wa kifedha.
Gesi sasa ni 54k, umeme ndiyo huo upo sasa nusu saa baadae haupo. Kwa muktadha huo kuni na mkaa bado utatumika sana.
 
Ndo mtafanywa mashoga sasa ... Huwezi ukawa unategemea tu wanaume wenzio wakulishe na wakuache tu hivyo hivyo
 
Hili la kupanda miti ni muhimu sana, angalau kila kaya ipande miti kumi kwa mwaka.
Nashangaa huku Dar watu wanajenga na kukata miti kila mahali frame wamesahau umuhimu wa miti ndio maana joto linazidi, ukienda Morogoro Hali inasikitisha Yani watu wamekata miti midogo na hawaipandi hata kidogo. Serikali ije na sheria kila nyumba lazima ipandwe miti Ili kulinda nchi na mabadiliko ya tabia ya nchi.
 
Kuongea huwa ni Rais sana like motivational speaker na kilimo Cha matikiti maji, ngoma huko shambani na sokoni, swala la mazingira ni global issues linahitaji kuhusisha wadau wote ikiwemo nchi ambazo zimeendelea kujimwambafai eti Tanzania tunaweza wenyewe kwenye Hilo swala ni kujidaganya budget tu ya mambo mengine ka afya, elimu, miundo mbinu kizungu mkuti sembuse ya kuwekeza kwenye mazingira it's impossible we need a big boost
 
Wakati Marekani wakigawa viwanja wanaweka na sehemu za kupanda miti. Unaweza kuendesha gari usijue kuwa kuna mtaa watu wanaishi mbele kuna msitu uliopangiliwa nyuma ya msitu ni myumba.
 
Kwa upande wangu nilimsikiliza na nilimwelewa kama ifuatavyo;
Tatizo la mabadiliko ya tabia nchi si geni ni la muda mrefu na njia nyingi za namna ya kukabiliana nazo zilishatolewa na si kwamba hazijulikani,
Katika njia zote utekelezaji ndio umekua ukisua sua hasa namna ya kuwezesha ama miundo mbinu hiyo iweze kufanya kazi, ndio maana akasisitizia katika kuwezeshwa ili iwe rahisi katika kuyafanya yale yanayojadiliwa .
 
Wakati Marekani wakigawa viwanja wanaweka na sehemu za kupanda miti. Unaweza kuendesha gari usijue kuwa kuna mtaa watu wanaishi mbele kuna msitu uliopangiliwa nyuma ya msitu ni myumba.
Ila huku Tanzani watu wanakata tu miti na kujenga kila corner, for stance lugalo wanakata miti yote Ile na kujenga frame za maduka na kuisahau umuhimu wa miti kabisa inabidi sheria itamke na iwe lazima kupanda miti
 
Wewe ni mpumbavu, kwa kujibu yasiyokuwepo kwenye andiko unalosoma. Na kwa sababu hiyo hustahiri kujibiwa chochote kwa sababu umeacha uchafu mtupu hapa.

Wewe ni "Matola"? Jina hilo ni kama lina maana maalum kwa jamii ya kiTanzania!

Bure kabisa.
 
Ninadhani kuhimiza wananchi kutumia majiko ya gesi na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ingekua ni jambo la kujadili ndipo kuomba msaada wa kifedha.
sasa watu wenye mawazo kama haya ndio hamtaki kugombea hata nafasi za uongozi. Mawazo kuntu kabisa haya.
 
Wewe ni mpumbavu, kwa kujibu yasiyokuwepo kwenye andiko unalosoma. Na kwa sababu hiyo hustahiri kujibiwa chochote kwa sababu umeacha uchafu mtupu hapa.

Wewe ni "Matola"? Jina hilo ni kama lina maana maalum kwa jamii ya kiTanzania!

Bure kabisa.
Pole mjane.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…