Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Nchi zilizoendelea zinapaswa kutoa fidia kwa nchi masikini kwani viwanda vyao ndio vinatoa gas nyingi zinazoharibu ozone layer. Tena sio kwa kubembeleza ilibidi iwe ni lazima.
Kabisa unaamini Tanzaia inaweza kulazimisha hizo ncho zilizoendelea? Unaota?
We huoni mama Samia kila sentensi anaweka neno naomba
 
Nchi bila misaada haiendi ndio maana kina mwigulu walikuja na tozo za miamala mkaanza kulia lia, na ujue budget ya nchi 60% inategemea wahisani Sasa acheni kujilisha upepo serikali ikiongeza Kodi mtaanza kulia ka yatima jangwani.
Nchi kuendelea sio tozo Wala misaada Bali kutumia resources zake to the maximum
Tanzania ina kila aina ya rasilimali, itumie hizo kutoka hapa tulipo.
Kachukue mfano wa Singapore au China, alafu uje uone aibu tuliyonayo huku Africa.
 
Mnaona aibu kuomba omba? Mnamuonea aibu nani asiyejua nchi hii ni masikini wa kutupwa na inategemea misaada kuendeshwa? Ndiyo hali halisi nchi masikini kama hii haiwezi kumudu mfano tozo ya kupunguza carbon (carbon tax).

Lazima tusaidiwe au mnataka Watanzania wafe na tai shingoni kwa kuona aibu kutembeza bakuli? Ndiyo maana yule aliyepita aliona aibu za kuomba msaada wa kupambana na Covid-19, wengi wakafa kwa ajili hiyo. Tukubali nafasi yetu hapa duniani kama nchi masikini, tunaotegemea misaada miaka 60 tangu tupate uhuru.
Ndio ni aibu kuomba omba huku Nchini kwako umejaza Rasilimali Asili na Rasilimali watu za kutosha.
 
Nchi kuendelea sio tozo Wala misaada Bali kutumia resources zake to the maximum
Tanzania ina kila aina ya rasilimali, itumie hizo kutoka hapa tulipo.
Kachukue mfano wa Singapore au China, alafu uje uone aibu tuliyonayo huku Africa.
Na nchi zenye resources nyingi ni maskini maana hawana technology ya kuzitumia hzo resources kujitoa kwenye umaskini na hata Hali ya masoko inaamuliwa na wakubwa wa dunia unaweza kuzitumia hzo rasilimali ila kujitoa kwa umaskini ni ngumu maana unapangiwa Hadi bei ya kuuza bidhaa zako
 
Na nchi zenye resources nyingi ni maskini maana hawana technology ya kuzitumia hzo resources kujitoa kwenye umaskini na hata Hali ya masoko inaamuliwa na wakubwa wa dunia unaweza kuzitumia hzo rasilimali ila kujitoa kwa umaskini ni ngumu maana unapangiwa Hadi bei ya kuuza bidhaa zako
Toa solution tufanyeje
 
Ninadhani kuhimiza wananchi kutumia majiko ya gesi na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ingekua ni jambo la kujadili ndipo kuomba msaada wa kifedha.
Ni yale yale ya Maria Magdalena.Kama kuna uhaba wa mkate si wangekula keki?Kipato cha siku kwa watanzania wengi (majority wanaishi vijijini ni shillingi ngapi?)
Wana uwezo wa kutumia gesi.?Tuhimizane tusikate miti ovyo na tukikata mti tupande mti.
 
Hizi ngonjera zako zilimshinda Nyerere akang'atuka urais akamwachia Mwinyi nchi iko hoi kiuchumi.

Naye yule chizi wa Chato akaja na skili za kijinga kama hizi.

Muelewe yule mama mkitaka awapeleke hivi mnavyotaka nyinyi mtakaoumia ni nyinyi, hakuna Rais anayeumia kutokana na nchi kuwa na hali ngumu.

Hata huyo Magufuli baba wa uwongo kama alivyo shetani hajawahi kuwa na maisha magumu tangu singie serikalini achilia mbali Urais, tena yeye ndio kufuru alikuwa anatembea na begi limejaa pesa, anamgawia anayejisikia yeye kumgawia siku hiyo na huku akiwahadaa na kuwadanganya wajinga wenzake kwamba watembee kifua mbele Tanzania ni tajiri kumbe yeye ndio tajiri, na hilo kundi la wajinga wenzake kina Abunuwasi hawa unakuta wengi hawana uhakika wa milo hata miwili tu.
Kweli viazi mviringo ni vingi humu jukwaani.
 
Lini watanzania waliacha kujituma na kufanya kazi kwa bidii?!!!

Unaongea kana kwamba uko ndotoni vile......
Hivi unajua kuwa tanzania ndo nchi pekee ambayo wananchi wake wana muda wa kwenda kupoteza muda.[emoji57]
 
Nchi bila misaada haiendi ndio maana kina mwigulu walikuja na tozo za miamala mkaanza kulia lia, na ujue budget ya nchi 60% inategemea wahisani Sasa acheni kujilisha upepo serikali ikiongeza Kodi mtaanza kulia ka yatima jangwani.
Okay tozo bado zipo bakuli linatembea hadithi zilezile .
Lazima utambue maana ya umaskini kabla ya kupambana nao.
Kikwete hajui kwanini sisi ni masikini ndio maana ushauri wake ni kutembeza bakuli.
Wasomali wanakuja Tanzania kama wakimbizi lakini baada ya miaka kadhaa wanatajiriki formula ni ile ile geuzi rasilimali kuwa bidhaa ziinufaishe dunia uone kama hautikidhi mahitaji yako.
Hiyo ni kuanzia wewe binafsi hadi taifa sio kinyume chake
 
Wafugaji wamejaa maporini wanafyeka misitu/mapori eti wanyama wao wasipotee, hakuna anaejali! Wenye mamlaka wako bize na machinga! Bado mapori ya akiba/tengefu kwa ajili ya kuhifadhi mazingira mnawagawia wananchi wafyeke waishi! Ina maana Mwalimu alikuwa mjinga kuyatenga? Aisee yaani afrika haina viongozi ndiyo maana tramp alikuwa anawadharau sana! Yaani ni mizigo! Ndiyo haibebeki! Mapori yanateketea halafu wanaenda ulaya sijui kusema nini! Sisi wakulima tunasikitika sana!
KAMA UNGELIKUWA WEWE NDIO RAISI UNGEFANYEJE?
 
Hatutaki Rais asiyekuwa na exposure, na muelewe wazi nchi hii haitatawaliwa tena na washamba.

Dosari za mama tunazijuwa tutadeal naye accordingly, lakini never again kukabidhi nchi kwa washamba.
HUU NDIO UKWELI
Ukitaka kuzuia uharibifu wa misitu ni lazima uweke mbadala wa matumizi ya cooking energy
Gesi inabidi iwe rahisi , na ili iwe rahisi utahitaji Ruzuku angalau kwa miaka 5 ya awali ili kuwapeleka watu kwenye kuzowea.
Vifaa vya Gesi viwe rahisi au vitoewe bure kwa angalau miaka 5 ya awali kwa wtu wa vijijini ambao ndio watumiaji wakubwa wa kuni na wa mijini watumiaji wa mikaa.
Mama anaomba Pesa za Kuliwezesha zoezi hili liweze kuharakisha uhufadhi wa Misitu yetu.
Bila ya hivyo sisi pekeyetu hatuwezi, utaidi usambaze Askari msituni kuzuia ukataji miti ambayo inahitajiwa kwa matumizi ya kila siku, hivyo haitawezekana mpaka upate mbadala.
Bakuli linahitajika lijae.
 
Rais kakumbushia utekelezaji wa Maazimio ya Paris. Mataifa makubwa yanayoongoza kuzalisha hewa ya ukaa, kinara akiwa China, US na Urusi na nyingine ziliji commit kutoa karibu Usd 100bilioni kukabilia mabadiliko ya Tabianchi.

Sasa kosa kukumbusha utekelezaji wa ahadi? Ina maana gani sasa kila mara viongozi wakutane halafu hakuna utekelezaji? Nilitegemea tumpongeze Rais wetu kawagonga wakubwa diplomatically...
 
Wanabodi,



Kama mtanzania, inawezekana umepata nafasi kufuatilia yanayojiri nchini Scotland kwenye mkutano unaohusu mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi wengi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alihutubia mkusanyiko huo.

Tofauti na nchi kama China, Marekani na India, Tanzania haihusishwi sana kwa kuwa chanzo cha mabadiliko ya tabia nchi. Umuhimu wa kuhudhuria mkutano huo ni kujumuika na viongozi wengine katika kujadili suala hili na kuwa na mchango unaoweza kuleta manufaa chanya kwa miaka mingi ya baadaye.

View attachment 1996340

Nimebahatika kuanglia hotuba zote za Rais Samia na kwa bahati mbaya au nzuri, aligusia zaidi kwenye umuhimu wa nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi ambazo hazijaendelea kifedha ili kuweza kukabiliana na tatizo hili la mabadiliko ya tabia nchi.

Labda inawezekana kwamba ni kweli Tanzania inahitaji misaada hiyo lakini kwa upande wa pili haipendezi kuona kwamba mawazo haya ya kuendelea kupata misaada imetawala katika vichwa vya viongozi wetu. Kauli kama hizo zinaweza zisizae matunda.

Ingependeza sana kama Rais Samia angejizatiti zaidi katika kuongelea umuhimu wa kuwa na "balance" katika shughuli za maendeleo, maslahi ya binadamu na mikakati ya kulinda mazingira. Kama Tanzania, angezungumzia changamoto zinazo sababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na mipango yetu haswa katika kipindi ambacho tunatamani uchumi wa viwanda.

Kwa nchi zilizoendelea, umuhimu wa sayansi katika kuvumbua njia mpya zisizo chochea uharibifu wa mazingira zinazoweza kutumika kwenye sekta mbali mbali

Mungu ni mwema, wakati wote

Angetaja hata juhudi zilizo ndani ya uwezo wetu za upandaji miti basi ingetosha.

Wewe umeenda kwenye mkutano uwe sehemu ya suluhu halafu unaenda kutangaza njaaa1🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom