Ya jamaa au yangu?
Jamaa alidakwa, akasota ndani kwa muda mrefu pasipo kesi kusikilizwa. binti alikuwa anasoma uganda sasa aliporudi, alikuwa anasoma form 6, akafikia kwake akae siku 3 ndo aende kwao ndipo akafa. so jamaa alikimbia kisha akapiga simu kwa jirani kumwambia ndani kwake kaacha maiti. Alikaa sana zaidi ya miaka 7 ndani kesi hata haisikilizwi. Ila kwa sasa yuko uraiani japo sijui yuko wapi ni muda sana nimesikia taarifa zake.
Mimi alikuja kwangu. Tumekaa kaa tumefanya yetu. Baadae nimekwenda sebuleni narudi namkuta kazima. Haitiki, hajitingishi. Nikimtikisa anaguna tu. Wee asikwambie mtu nilitaka kudata. Nikaanza kumtikisa anaguna tu mapigo yake ya moyo yako chini kabisa.
Nikamkokota hadi bafuni nikamwagia maji, wapi. Nikataka kuwaita majirani, nikaona jau maana hakuwa kavaa. Nikamvisha kwanza. nikatoka nje nikaona isiwe tabu. Nikarudi ndani nikamkokota nikamwingiza kwa gari, hapo nawaza nimpeleke hsptal. shida sikuwa na pesa ya kutosha, na nikawaza nipige simu kwao. Familia zetu zilikuwa family friend lakini hawakuwa wanajua kama mimi natoka na mwenzangu ilikuwa siri kubwa baina yetu.
Mwisho ilibidi nipge simu kwao maana nilimpeleka hsptal akalazwa kapgwa drip za kutosha, pimwa kila kitu kuanzia presha, sukari sijui nini na bado hawakuona tatizo. Alianza stabilize baada saa nane usku toka saa mbili nilipomfikisha hospital.
Kwao walifika hapo na nashukuru Mungu hawakuniuliza nimemtoa wapi, nadhani walijiongeza na bill mzee wake akalipa na wala hakunihoji.
Nilikuwa bado chalii ndo nina mwaka nimemaliza chuo. Baada ya hapo nilikuwa namwogopa kama ukoma.