Yah ni kweli majanga hutokea maishani mkuu ni kumshukuru Mungu.
Sikuwapigia simu home, na sijui hata kama wao waliwaambia home. Ila mimi kesho yake nilienda home maana nilikuwa naishi alone nshatoka home, so nilienda nikawa najiongelesha ooh fulani aliumwa akalazwa, nilikuwa pale hospital. Sikusema kama nilikuwa naye na nikampeleka nao home wakaonekana kutokuwa na taarifa.
Wazazi wake yani hawakuonyesha reaction yoyote. Ila sasa mimi nikawa najishtukia. Nilikuwa naenda pale nikaacha. Walikuwa muda mwingine wananiomba nimpeleke mdogo wake huyo binti shule alikuwa anasoma sekondari hasa siku zikifunguliwa muda mwingine mimi nilikuwa nampeleka shule, wakaacha kuniambia nimpeleke sijui waliniona ni fisi.
Aaah mkuu gari mafuta ilikuwa nayo, ila fedha kama fedha sikuwa nayo nilikuwa nimepiga. Halafu nilikuwa naishi bahari beach, so nilimpeleka rabinsia pale tegeta, na kwao ilikuwa hapo Africana.
Kwanza nimepiga simu kwao nikiwa mbuyuni, bahati nzuri baba na mama yake walikuwa maeneo ya wazo so tumekutana pale pale hospital maana hata fedha ya kufungua file ilikuwa buku 10 ningebaki na buku mbili. Ilikuwa noma mtu wangu.