Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ajabu kweli anaongelea watu ambao wazazi wao waliingia nchini toka 1972 hao watoto zao na wajukuu zao warundi tena. Si washakuwa watanzania.

Embu wapunguze kunyanyapaa watu kisa babu zao walikuja kama wakimbizi.
Yeye atuambie asili ya majenerali wote babu zao walitoka wapi na yeye pia
Utakuta wengi ni wa kuja tu
Zambia, Malawi na hata Msumbiji na kwingine

Tuna chuki tu na hayo sio ya kuropoka angesema tumekamata wanajeshi wanaofanya ugaidi na asili zao hapo sawa

Lakini wakimbizi waliokuwa Ulyankulu miaka 40 iliyopita na kuna Doctors wanaotuhudumia au hajui hilo
Kuwa hata anaemchoma sindano anaweza kuwa asili yake mrundi?
 
Cdf anaongea kuhusu wakimbizi lakini mama anaongealea uchaguzi. Kifupi kila mtu hapo alienda na ajenda yake yaani ni sawa mkaenda sehem kwa nia ya kujadili jambo fulani lakini kila mtu akatanguliza shida zake kwanza.

Swali; lengo la mkutano ilikuwa ni kujadili nini?
 
Yaani,haya ndio maoni ya CDF! Anasema kuna watu wanapata uraia, bila serikali kujua!? Kuna ubaya gani, MTU kutoka Rwanda, Burundi, Congo, kuomba uraia? Au kwa vile ni weusi? Mbona wa Asia, wazungu,wapo kibao tu,? Kama jeshi, na taasisi zake za, intelijensia, hawana, tskwimu, na wala hawajuhi hao watu, basi, huyu jamaa, ni kilaza kweli kweli, yaani na jwtz na wao wanalalamika! Kuhusu, wakimbizi haramu! Ingekuwa jeshi lenye weredi, angesema, wamekamata watu 3000+walioingia kinyemera! Fucking stupid
Rudi kwenu
 
Huu ndo ukweli.
Na wengi wamekuwa wakiingia nchini alafu baadae utasikia wanajiita wasukuma. Wamejaa wengi sana mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Katavi na Shinyanga na sasa wamegundua wakiwa huko wanagundulika wameamua kuja mikoa mingine na kujitambulisha kuwa wasukuma au wenyeji wa mikoa husika.
 
Waondolewe haraka !! Sio jambo la kusubiri na si ajabu ni jambo likijulikana muda mrefu !!
 
Hii statement kama haijatolewa kisiasa basi ni statement hatari Sana kwa usalama WA nchi! Je ni akina Nani hao?
Tumeandika sana tangu Jambo Forum (2006) mpaka hii leo Jamii Forum (2024), kuwa kuna raia wa nnje wamepatiwa pasi za Tanzania na wana vyeo huko serikalini,mashirika ya umma na taasisi za umma,lakini vyombo vya dola vimeweka pamba masikioni.

Kuna miaka ya 2010 hivi RSO wa mkoa fulani alipelekewa "dossier" ya mtu fulani mkubwa,akasema atafanyia kqzi,lakini mpaka leo huyo mtu yupo na nafasi kubwa tuu.

Hii inchi ni kama nyeti za kuku upepo uvumapo.
Ipo siku tutalia.
 
Statement ina maswali mengi kuliko majibu wanaashiria nini haswa.

Wamejuaje kuna watu wana nafasi serikalini wakiwa wakimbizi? Wakati statement kama hiyo ulitegemea kutolewa na uhamiaji.

Je wakimbizi wakipewa uraia awaruhusiwi kufanya kazi serikalini au kushiriki siasa.

Je kuna mienendo ya watu walikuwa inawafuatulia katika uchunguzi wao wakabaini hawana makaratasi sahihi ya kushika hizo nafasi

Je wanaashiria uhamiaji inatoa uraia kirahisi without due processes.

Je wanaashiria ni rahisi kupata vitambulisho na huko serikalini hawana system nzuri ya ku-very background ya watu.

Ni statement tata sana with ‘fuzzy logic’ conclusion.
Huna maswali wewe...labda kama unaishi Ulaya..
 
kwa hiyo kagme ana pandikizi lake ndani ya system? Kama vipi waling'oe tu

rudi nyuma kwanza kuanzia mwanzo kabla ya kuanza kuropoka, mlango uliongilia ndio utakao tokea, unavyoishi ishi ndivyo utakavyoishia, what goes around comes around and a deal is a deal, kila mjanja na mjanja mwenzake, kazi iendelee.
 
Samia ameanza kuliagiza jeshi tena kuhusu hizi chaguzi 2 za 2024/2025!!!....

Kwamba Jeshi liwe tayari kwa lolote Lile!

Hii kwa jeshi sio ombi tena!... Ni amri-tekelezi ....Ni tayari!.

Hii ni taa nyekundu tayari kwa vyama vyote kuelekea 2024/25 vijiandae kisaikolojia!

Hii ina Maana chaguzi za 2024/2025 zitakuwa na backup ya jeshi!

Hizi chaguzi hazitakuwa tofauti na ule uchaguzi wa 2019/2020 wa mwendazake.

Hii nchi Bado tuna safari ndefu sana ya kuwa na demokrasia huru.
 
Statement ina maswali mengi kuliko majibu wanaashiria nini haswa.

Wamejuaje kuna watu wana nafasi serikalini wakiwa wakimbizi? Wakati statement kama hiyo ulitegemea kutolewa na uhamiaji.

Je wakimbizi wakipewa uraia awaruhusiwi kufanya kazi serikalini au kushiriki siasa.

Je kuna mienendo ya watu walikuwa inawafuatulia katika uchunguzi wao wakabaini hawana makaratasi sahihi ya kushika hizo nafasi

Je wanaashiria uhamiaji inatoa uraia kirahisi without due processes.

Je wanaashiria ni rahisi kupata vitambulisho na huko serikalini hawana system nzuri ya ku-very background ya watu.

Ni statement tata sana with ‘fuzzy logic’ conclusion.
Hii nchi kuna ujinga mwingi sana
Hii taarifa ya JWTZ ni ya kichochezi na kinafiki , hii sio kazi yao na kwanza wanaposema wakimbizi wamepewa nafasi za maamuzi wanamaanisha mtu mzima kabisa kahamia Tanzania kaomba uraia halafu leo hii ana nafasi serikalini?

Je vipi kuhusu kina Bashe, Kinana, au Shivji na wahindi wengine ,hawa ambao wamezaliwa na kukulia , na kusoma nchini ndio hawa anawazungumzia?
Kama ni hawa? kwa kauli hii fikiria mbuzi inaiishi kipwilimbiu huko vijijini, atafikiria vipi zaidi ya moja kwa moja kuwahhusisha hawa au wengine wengi kuwa ndio wanaozungimziwa
 
Wanamsema Mpango anatoka Burundi!!
Kinana ni mwanajeshi mstaafu. Shivji kwani ni mkimbizi? Anafanya kazi serikalini?
Samia anapanic anajua with a level playing field hawezi kushinda hivyo anaomba msaada wa jeshi!
Hiyo ni hatari anakaribisha wanajeshi wampindue?
 
Yeye atuambie asili ya majenerali wote babu zao walitoka wapi ma yeye pia
Utakuta wengi ni wa kuja tu
Zambia, Malawi na hata Msumbiji na kwingine

Tuna chuki tu na hayo sio ya kuropoka angesema tumekamata wanajeshi wanaofanya ugaidi na asili zao hapo sawa

Lakini wakimbizi waliokuwa Ulyankulu miaka 40 iliyopita na kuna Doctors wanaotuhudumia au hajui hilo
Kuwa hata anaemchoma sindano anaweza kuwa asili yake mrundi?
Mipaka yenyewe wamechora wazungu kwenye Berlin Conference 1885 makabila ya border africa nzima wanaongea lugha moja na upande wa pili. Utakosa vipi wahamiaji.

Tena afadhali ukanda wetu, ukienda West-Africa kuna kipindi nilikuwa naingia club house kusikiliza mijadala ya wanaija, salalee jamaa wana high sentiments na loyal kwa makabila ya mpakani kuliko national loyalty.

Watu waje uwapokee, wewe mwenyewe uwape mahala pa kuishi, halafu uwa restrict kwa miaka zaidi ya hamsini kuwa sehemu ya jamii. Hao watu anaowaongelea si ajabu wamezaliwa Tanzania na wana watoto na wazee wao washafariki, hawa utawaita wageni kweli.

Wanajihami sana wewe ukishakuwa na dira yako, foreign policy unayosimamia na regional politics zako. Huo ndio mwongozo wako wa namna utakavyo interact na dunia na kuhakikisha unausimamia.

Uoga wa nani umemwajiri ni ishara ya uzembe wa ku-monitor watu wako kwenye kutunza siri. Na moles ni tamaa za watu inaweza kuwa hata watanzania wenyewe. Kama huko CIA kuna double agents tena wanao risk kutoa siri za maisha ya watu walio field kwa misingi ya tamaa itakuwa Tanzania.

Wajipange katika shughuli zao za ulinzi sio kunyanyapaa watu, Obama baba yake mkenya, Collin Powell baba yake mjamaca, Rish Sunak wazazi wake wahindi tena wamezaliwa East Africa. Sisi kutwa kuwasimanga watu ambao wazazi wao walikuwa wakimbizi. Huko ni kushindwa kwa nationalism propaganda.
 
Kuna Arabs of Latin America walienda huko 19 century na kuna nchi 11 waliwachagua Marais wenye asili yakiarabu huko
Ila unaweza ukawa na wakuja na wakafanya vizuri kuliko wanaojiita wananchi

GCC wameajiri wa Sudan, Wasomali kwenye majeshi yao mpaka ukienda kama UAE na Qatar mpaka police na traffic ni wamo wengi tu ila husikii hata siku moja wakilalamika kuwa wameiba silaha au wanataka kupindua au usalama wao waarabu upo hatarini
Sisi masikini tunaogopa wakati ndugu zetu wenyewe wanatupiga mizinga kila leo

Nilienda Cairo miaka 35 iliyopita
Nikampa taxi driver $100 alifurahi akaniambia chukua Cairo yote 😄
Hiyo story ya Cairo ndio zao, mwenzao Ashraf Marwan aliwakwamisha Waarabu wenzao dhidi ya Israel juu ya tamaa zake.
 
Hii nchi kuna ujinga mwingi sana
Hii taarifa ya JWTZ ni ya kichochezi na kinafiki , hii sio kazi yao na kwanza wanaposema wakimbizi wamepewa nafasi za maamuzi wanamaanisha mtu mzima kabisa kahamia Tanzania kaomba uraia halafu leo hii ana nafasi serikalini?

Je vipi kuhusu kina Bashe, Kinana, au Shivji na wahindi wengine ,hawa ambao wamezaliwa na kukulia , na kusoma nchini ndio hawa anawazungumzia?
Kama ni hawa? kwa kauli hii fikiria mbuzi inaiishi kipwilimbiu huko vijijini, atafikiria vipi zaidi ya moja kwa moja kuwahhusisha hawa au wengine wengi kuwa ndio wanaozungimziwa
I agree ni kauli ya kunyanyapaa watu
 
Back
Top Bottom