Mlinzi wa Rais kuvaa sare za chama ni sahihi?

Mlinzi wa Rais kuvaa sare za chama ni sahihi?

Wanajukwaa naomba kuuliza hili la walinzi wa Rais Magufuli kuvaa sare za CCM limekaaje?


Wanasiasa mnatuumiza sana akili. Mbona siku za kawaida ambazo huyo huyo aliyevaa Nguo za chama leo huwa havaagi sare na hujakuja kuandika threads hapa?

Au ni sahihi kwa Wanajeshi au polisi wakiwa kazini kutokuvaa sare za kazi?

Bila Shaka jibu ni, kuna vitengo ndani ya polisi au jeshi hawalazimishwi kuvaa sare wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao. Bali watavaa ambacho kitawarahisishia ufanisi wa majukumu. Ndio maana ili kuvaa uhusika wengine huvaa au kuigiza uchizi kulingana na jukumu alilopangiwa.

NB: Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuvaa mavazi ya chama fulani na kuwa mwanachama wa chama husika.
 
Mara mia sasa warejeshe siasa majeshini kama ilivyokuwa mwanzo kabla ya mfumo wa vyama vingi
 
Hii sio sahihi kabisa, ni jambo la kukemewa na kila Mtanzania mwenye akili timamu. Unapoona mtu anatetea ujinga huu, basi ujue huyo ni Mpumbavu na Goigoi mkubwa kabisa. Yule mlinzi ni mtumishi wa serikali ya umma wa Watanzania, anayelipwa kutokana na kodi za Watanzania wote kwa ajili ya kuwakilisha maslahi ya wote. Upumbavu huu wa hiki chama cha majambazi umezidi sasa, yaani hakuna mtu mwenye uthubutu kupinga haya mambo ya kipumbavu ndani ya chama chao?
 
Hawako professional wewe ndiye unayetema pumba.
Hao ni watumishi wa serkali na hawapaswi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.Hivyo wanapo jikankanya huo sio professionalism.
Wabongo huwa hatuna muda wakufanya uchambuzi yakinifu.
Wenzako wako ki professional, wewe unatema pumba. Hivi Rais angekuwa wa Chadema, na hao walinzi wakavaa jezi ya Chadema ungelalamika?
 
Hii mpya, mlinzi yule yuko pale kumlinda Raisi wa Tanzania hata kama pia ni mwenyekiti wa CCM. Anaelindwa ni Raisi na mlinzi yule anatakiwa awe kwenye magwanda yake ya mlinzi wa Raisi ambayo tunayafahamu, hizo nyingine ni mbwembwe za kishamba tu.
Unayafahamu yakoje?
 
Ngoja nikusaidie kitu, ukisoma sheria ya usalama wa Taifa ya Mwaka 1996 imeweka wazi kuwa watumishi wa Idara hiyo hawabanwi na sheria ya utumishi wa umma.

Hivyo unapaswa kuelewa kwamba kutokana na nature ya majukumu yao (kama ulivyoambiwa hapo juu, watu hao wapo kila sehemu, ikiwemo kwenye hivyo vyama vyenu), isingewezekana wao kufanya kazi katika mazingira yanayofanana na watumishi wengine wa umma.

Ni akili ya kawaida tu inahitajika kuweza kuelewa haya mambo. Soma zaidi ili ujenge uwezo wa kujenga hoja kwenye majukwaa kama haya.
Mkuu huyu hawezi kuelewa ata ukimuelewesha kwa viboko
 
Kwanza kabisa Ndugu mtoa mada ninaomba utambue kuwa katika madani za kiulinzi kuna mbinu mbalimbali za kiulinzi, moja ni pamoja na ile atumiaye Kinyonga ya kujibadili kutokana na mazingira kitaalam inaitwa camouflage

pili ninaomba sote tutambue kuwa kuvaa nguo zinazofanana na watu wa chama fulani, sio sifa ya kukueleza kuwa ww ni mwanachama wa chama husika.

Mwisho kabisa nimalize kwa kujibu swali lako, kuwa kuvaa vile kwa walinzi wa MHe. Rais ni halali kabisa, ni sawa tu siku ukimuona amevaa suti,combat au shati la kawaida.
Hizo mbinu akina Kikwete walikuwa hawazijui?
 
Kwwhiyo hata Magufuli hapaswi kuvaa sare za ccm kwenye vikao kama hivyo?
Wewe ni mjinga uliyepitiliza. Hivi hujui kuwa Magu ni mwenyekiti wa CCM na amepata cheo hicho kupitia CCM. Sasa jiulize huyo mlinzi alipata kazi kwa kugombea kupitia CCM? Ndugu yangu, kuna utumishi wa umma na utumishi kwa kofia ya chama. Mmeharibu nchi yetu na mifumo yake yote nyie watu. Namwonea huruma huyo ajaye baada ya kituko hiki kilichopo ambaye ataanza upya kuijenga nyumba yetu. Nyumba yetu kila mahali ni matobo matupu!
 
Wanajukwaa naomba kuuliza hili la walinzi wa Rais Magufuli kuvaa sare za CCM limekaaje?

Imekaaje vipi....yaani ulitaka wavae macombat yenu au vipi? Those are professionals...wanajichanganya for security reasons..mijitu mingine bwana mnleta humu comment za kitoto sana
 
Guys sisiemu muwaache walivo... Kwa sababu ya ubumbumbu wengi wetu watatumia polisi, jeshi na kitengo/idara yoyote kwa maslahi yao na leo itakuwa kesho...kesho itakuwa kama leo, jana na juzi...
 
Back
Top Bottom