Mlio karibu na Tundu Lissu mumkanye aache mara moja kuropoka ropoka!

nakupa masaa 24 uwe umerudisha simu yangu, nitakachokufanya tusilaumiane
 
Unachanganya mambo....

Zanzibar ni hifadhi ya wanyamapori ?!!!

Tundu Lissu si tegemeo la watanzania....

Ona alivyo mwongo....

Anasema kuwa MWIBA HOLDINGS imepewa ardhi zaidi ya hekari milioni 2 huko mkoani SIMIYU....sasa ukubwa huo si zaidi ya mikoa 2?!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Rutashubanyuma
Umeongea ukweli na pia umechambua vizuri kwa kina.
Lissu hataki kukubali kwamba yeye ana kasoro.hafanyi tafakuri kabla ya kutamka jambo.

Lissu ni mfuasi wa sifa bila kujali athari zitakazotokaba na utafutaji sifa wake.
Yuko radhi kuwavunjia heshima wenzake ili mradi yeye asifiwe kwa walioko mbele yake.kwa ujumla Lissu ni mbinafsi na mtu wa Visasi.
Hana staha ya kiuongozi na kweli sio Presidential Material.Ni bahati tu kwamba yuko kwenye chama ambacho
"Code& Conduct" sio kipaumbele chao.

Kuhusu Ngorongoro pia uko sahihi isipokuwa idadi uliyoitaja ya Wamasai ni ndogo kuliko uhalisia.
Na ni kweli wanatishia uoto wa asili na mali kale zilizohifadhiwa hapo Ngorongoro kwa faida za kiuchumi kupitia utalii na kihistoria na ndio maana pale ni mojawapo ta maeneo ambayo yanaangaliwa pia na kuhifadhiwa na taasisi za kimataifa kama UNESCO,AWF na FZS.
Kuendelea kuwaacha wamasai na mifugo yao kuongezeka ndani ya hifadhi ni hasara kubwa kwa taifa kuliko madhara ya kuwahamishia eneo lingine tofauti na hapo.

Pia uko sahihi kuliona suala la kuwapeleka eneo tofauti na Handeni.
Kwa pale Sonjo, Sale na Digodigo tayari palikwisha kuwa na migogoro ya kugombea ardhi baina ya jamii mbili tofauti za Wamasai na Wasomjo.
Na hata kuwahi kupiteza maisha ya mamia ya watu huko nyuma.
Hivyo ni jambo ambalo halingewezekana....
Lakini ninayo imani kwamba kuna maeneo mengine pembezoni mwa Monduli na Longido ambako ingefaa zaidi kuwa mbadala wa Handeni.
Na pia wangeendelea kuishi na kutengamana na jamii zao za kimasai na kuzidi kuimarisha na kuudumisha utamaduni na Mila zao za kiasili kwa pamoja.
Tofauti na Handeni ambako wanakwenda kuwa jamii iliyoxungukwa na tamaduni tofauti za kisambaa,Kibondei na kizigua.
Naomba niishie hapo kwa sasa!
 
Mada za kipuuzi hizi.

'Presidential material' ni anayekwambia uongo kwa sauti nyororo na kukuona wewe ni mpumbavu?

Unaambiwa unatakiwa ufunzwe maana ya Katiba kwa miaka mitatu, ndipo upewe ruhusa ya kuwepo na katiba mpya, tena wanayoitengeneza wao na siyo wewe mwananchi?
'Presidential material' ni mtu anayekiuka katiba, hata hiyo mbovu, halafu anarudi nyuma kukwambia wewe hujui katiba, hadi hapo utakapofunzwa?

Akili za namna hii kama siyo za matope, tuziite kitu gani..
Sijakusoma humo ndani umeandika takataka gani, nimejibu tu kichwa cha mada, na huo mstari ulioanzia mada yako ya kipuuzi.

Nyinyi watu mnaudhi sana, ndiyo maana inalazimu tutumie hizi lugha nzito, mnazoziita nyinyi lugha za kuudhi.

Unanifanyia ushenzi, halafu bado unataka nikunyenyekee, eti kwa vile wewe una cheo huko serikalini?

Hovyo kabisa.
 
Uropokaji....

Mwiba holdings imehongwa hekari zaidi ya milioni 2 huko Simiyu [emoji1787][emoji1787]

Hekari milioni 2 ni mkoa mmoja?!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Na kama yeye yuko karibu na Mh. Rais amwambie awe ana jibu hija na siyo mipasho. Yeye ni Rais wa nchi ajitofautishe na kina Kibajaji
Lissu ni mtu wa mipasho....

Eti Mwiba Holdings imehongwa zaidi ya hekari milioni 2 huko Simiyu....Sasa hekari zaidi ya milioni 2 si zaidi ya mikoa miwili?!! [emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 


Ongezea pia wamasai wengi wametoka Kenya wako Ngorongoro na Loliondo na mifugo yao

Hivyo matajiri wengi wako Kenya na mifugo iko Ngorongoro na Lolindo na wamasai wa Kenya wako kibao wameungana na wamasai wa Ngorongoro na Loliondo, na huwezi wajua yupi wa Tanzania au Kenya, wanaitana na kukaa huko, na kuhamia kiharamu, illegal kabisa, na huwezi wajua hao wamasai, hivyo mifugo mingi na wamasai wengi sana karibu 171,000 wako Ngorongoro na Loliondo, hivyo huharibu kabisa uoto wa asili na hifadhi, wanyamapori wanakimbia na hifadhi inabakia ni mifugo tupu na wamasai, tumshukuru sana Mama Samia na serikali yake, tungeacha miaka 4 au 5 baadae tungepoteza kabisa Ngorongoro na Loliondo sbb ingekuwa ni wamasai tupu na mifugo malaki, na hiyo isingekuwa ni hifadhi tena. Mama Samia aliona hili na hakurudi nyuma, Mungu mlinde mama huyu, kwani miaka michache tusingekuwa na Ngorongoro na Loliondo.

Pia ujue NGOs nyingi sana hutumia hao wamasai na mifugo yao kupata fedha ili kujidai wanawasaidia, na hizo NGOs ziko Kenya na Arusha, so kulikuwa na miradi ya watu na wanapata billions of dollars kupitia hizo NGOs, so Serikali yetu ya Mama Samia, imefanya juhudi kubwa sana kuokoa Ngorongoro na Loliondo, nimefika mara 4 huko, hali ilikuwa mbaya sana hao wamasai wakiendelea kukaa huko, kwani wamekuwa wengi mno na mifugo imechukua kila eneo huko, watalii wakija walikuwa wanaona ng’ombe wengi, kondoo wengi, mbuzi, punda na mbwa na wamasai tupu mbugani, hii sio sawa, tungeua kabisa hizi sehemu muhimu sana za utalii, hivyo tuunge mkono kwa nguvu zote wamasai watolewe huko, kwani si mara ya kwanza Serikali kuhamisha wananchi wake kuokoa sehemu husika au kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa letu, kwani wamasai ni nani?

Tundu Lissu acha apayuke payuke tu, hana akili, hajui lolote, yeye anapiga siasa tu, na mtu kama Tundu Lissu ni kosa kubwa sana kukaa nae chini eti mfanye maridhiano, au kuwe na political dialogue nae, ni kitu hakiwezekani, dawa ya Tundu Lissu ni kutumia nguvu hapo atakuelewa, hana hekima wala busara kabisa, anajifanya mbabe sana, so dawa ya mbabe ni kuwa mbabe zaidi yake, hana adabu kabisa, hatuwezi poteza World Cultural Heritage za Ngorongoro Loliondo kisa wanasiasa wapuuzi kama Tundu Lissu.

Mama Samia usirudi nyuma hata kidogo, moto ni ule ule na ongeza moto zaidi na watakuelewa kuhusu Ngorongoro na Loliondo, akina Tundu Lissu achana nao ni wapuuzi wakubwa.
 
Mbona wengine wamekubali kwenda Msomera Handeni?!!

Ni wapumbavu?!!

Ngorongoro ni turathi ya dunia....pia ni ya watanzania na si wamasai tu....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mambo yanashangaza sana....

Hivi ndugu zetu wakurya wangeachwa wafuge mifugo humu mijini ingekuwaje ?!!!

Kila kitu kina utaratibu wake.....

Ni rahisi kuipoteza hifadhi kwa sababu ya wingi wa mifugo....tena mifugo yenyewe ikiwa ni ya watanzania na ya wakenya.....

Tundu Lissu hana hoja[emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Sidhani km kuna mwenye uwezo wa kumwambia hata kama ingekuwa kweli! Hahaa!
 
....hana adabu....

Unawezaje kuingia makubaliano na mtu asiye na heshima ,utu na mjuaji zaidi ya kila mmoja wetu ?!!!!

Mashabiki wa TL ni mazombi.....[emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
[emoji2956][emoji2956]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…