Mlioko kwenye ndoa na watoto wenu wa nje, Mnalitatuaje hili swala?? Msaada jamani naombeni....

Mlioko kwenye ndoa na watoto wenu wa nje, Mnalitatuaje hili swala?? Msaada jamani naombeni....

Kila Mwaka mtoto lazima aende au apelekwe Kwa mama au Baba yake akakae walau mwezi au wiki mbili.

Kama MKE kaolewa basi wakutanie Kwa Bibi Yao. Mpeleke Kwa Bibi upande wa mamaake ukiwa tayari umeshaongea na Mama yake kuwa atakutana na mwanaye Huko.

Kama kila Mwaka itakuwa gharama basi angalau kila Baada y miaka miwili
 
Kuna Kaka yangu mmoja kutoka kwa Baba mkubwa alizaa na mwanamke mmoja miaka kama 12 hivi iliyopita. Ila hawakufanikiwa kuwa pamoja baada ya mtoto kufikisha miaka 4 mama yake alimleta kwa Baba yake na kumpa na kumwambia yeye anaolewa kapata Bwana mpya.

Basi kaka yangu huyu akamchukua mtoto wake. Na yeye akaoa baadae.

Sasa ishu ni hii sasa yafika miaka 8 dogo hajawahi kumuona mama yake tangu anamika 4. Kwa sasa anamika 12 yupo darasa la 6. Kuna kipindi dogo alikuwa anahitaji kuwa karibu na mama yake. Maana viashiria alikuwa anaonyesha anamuitaji mama yake.

Ila jamaa yangu akimpigia mama yake simu wanaishia kuongea tuu na mtoto. Wazazi wake wakamwambia ongea na mzazi mwenzio awe anamtembelea hata 1 wiki moja, ila mwezie wala hana time kabisa.

Sasa msaada jamani hii ishu kama ni wewe ilikukuta au ndugu au rafiki uliisolve vipi ishu kama hii. Msaada jamani.
Angeachana nae tu kama hamtaki mtoto mambo ya siwe mengi baadae mtoto akifanikiwa aache shobo huyo mzazi asije akaanza tamaa ooh mwanangu
 
Angeachana nae tu kama hamtaki mtoto mambo ya siwe mengi baadae mtoto akifanikiwa aache shobo huyo mzazi asije akaanza tamaa ooh mwanangu
Unajua mkuu mama yake kule ni maisha mazuri kinoma. Mume wake anapesa huwaga wanasafiri hata china uturuki kwenda kuchukua bidhaa za biashara zao.

Niliambiwa wanamiliki mpk V8 cruiser hizi. Maisha yao ni fresh sana kuliko hata baba yake huku dodoma.

Sasa tunaamini labda mama yake anaogopa asije kuaribu mahusiano na mume wake.
 
Tunaisi labda mume wake kule anaweza kuwa ndo kikwazo.
Katika hali,tabia na instincts za kawaida,hasa kwa mwanamke,ni ngumu kupenda kwa hiyari awe mbali na mtoto wake.Kuna sababu fiche ya "kiintelijensia"! Si bure.Baba mtoto amueleze mama mtoto hitaji la mtoto waziwazi.Asiikie jibu.Na yawezekana huyo mwanamke alimdanganya mumewe wa sasa kwamba hana mtoto.Watulie wasimuharibie ndoa yake.
 
Unajua mkuu mama yake kule ni maisha mazuri kinoma. Mume wake anapesa huwaga wanasafiri hata china uturuki kwenda kuchukua bidhaa za biashara zao.

Niliambiwa wanamiliki mpk V8 cruiser hizi. Maisha yao ni fresh sana kuliko hata baba yake huku dodoma.

Sasa tunaamini labda mama yake anaogopa asije kuaribu mahusiano na mume wake.
Duh kazi ipo huyo mama ampendi tu mwanae alimtelekeza baba yake angemwambia tu mwanae mama yako alikukimbia
 
Mna
Majibu mnayo sijui mnataka tushauri nini?
Hapo baba mtoto amuhoji kiujanja mama wa mtoto anuani ya makazi yake kisha mtoto akifikisha miaka 12 ampe nauli akamsalimie mama yake siku 5 tu arudi kwa baba yake.

Mama analinda ndoa yake, kwake ndoa muhimu kuliko mtoto wake damu yake. Analinda maokoto yake pia.
Ili wakaharibu ndoa yake kisha JF waanze kutukana single mothers. Wewe unaweza ruhusu mtoto wako akalale kwa mume mwenzio ambaye hujuani nae wala hujui tabia yake?
Huyo mama ndio amfuate mtoto sio mtoto amfuate mama
 
Back
Top Bottom