Mliowahi kuishi Ulaya: How does it feel kutembea Mjini bila kero za Bajaji, Bodaboda na Machinga?

Hizi bajaji na boda ni kama zimetulemaza hivi, naona hapa wenzetu wanatembea tu, sisi nusu kilometer unataka kupanda bajaji, lipo la kujifunza kupitia wenzetu.
Ndiyo maana magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanatushambulia mno.
Watu wetu ni malimbukeni sana wa vyombo vya moto.
Utakuta mtu anatoka Magomeni mapipa anaenda mwembechai anataka apande kipando
 
Labda huelewei maana ya uchumi jumuishi. Umachinga barabarani, kazi za Bajaji na bodaboda haziwezi kuleta uchumi jumuishi hata ukiziruhusu hadi ndani ya Ikulu. Uchumi jumuishi unaletwa kwa kazi, ajira au biashara za staha "decent jobs".
 
Watakataza vipi wakati ndio inaficha kwa asilimia kadhaa tatizo la UKOSEFU WA AJIRA?
 
Hata hapa bongo hizo pedestrian walkway zipo hasa kwenye main roads mkuu.
 
Sijafika ulaya ila picha tu nsona hao wanaotembea hapo wa utulivu wa akili, hawa ndio hata wakisema wanaenda kutembea kupunguza stress ndio hawa, sio kwetu hapa tz, kariakoo km uma stress ukienda huko ndio utachizika kabisa..
Ujue kuna watu sio machizi wamechizika na tabu za jiji lile
 
Nadhani
GREECE ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ท,
ITALY ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡น,
SPAIN ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ธ na
PORTUGAL ๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡น
zinazo pikipiki nyingi ukilinganisha idadi ya pikipiki na watu (motorcycles per person) kuliko TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ .

Ngoja wenye rekodi zao waje..
๐Ÿ

GREECE na ITALY zinazo utamaduni mkubwa sana wa scooters na motorcycles.
Katika miji kama Athens, Rome na Naples utaona pikipiki karibu kila mtaa.

Mad Max | RRONDO
 
Labda huelewei maana ya uchumi jumuishi. Umachinga barabarani, kazi za Bajaji na bodaboda haziwezi kuleta uchumi jumuishi hata ukiziruhusu hadi ndani ya Ikulu. Uchumi jumuishi unaletwa kwa kazi, ajira au biashara za staha "decent jobs".
Just imagine bila ajira za Machinga, Bajaji na Bodaboda kwa mamilioni ya vijana kwa wazee hapa Tanzania. Hao wote wangeajiriwa/kujiajiri kwenye kazi zipi 'decent '?. Nafikiri magenge ya uhalifu yangetapakaa kila kona.

Binafsi naunga mkono hizo ajira. Zirasimishwe na kuondolewa vikwazo ila tu serikali wadhibiti uhalifu.
 
Ukishindwa kuishi miji iliyostaraabika kama hiyo basi ujue ule uswahili wa Mbagala, Buguruni, Tandika umekujaa mno kichwani

Binafsi napenda mno utulivu wa aina hiyo badala ya vurugu zetu za hapa Bongoland
Karibu dengaa mkuu ๐Ÿ˜„

Ova
 

Attachments

  • Screenshot_20260530_131331_Gallery.jpg
    286.7 KB · Views: 6
  • Screenshot_20260530_131211_Gallery.jpg
    253.5 KB · Views: 9
Nadhani hizi nchi za Ulaya zifuatazo:-
GREECE ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ท,
ITALY ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡น,
SPAIN ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ธ na
PORTUGAL ๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡น
zinazo pikipiki nyingi (motorcycles per person) kuliko TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ .

Ngoja wenye rekodi zao waje hapa kulinganisha uwiano wa idadi ya pikipiki na watu.
๐Ÿ

GREECE na ITALY zinazo utamaduni mkubwa sana wa scooters na motorcycles.
Katika miji kama Athens, Rome na Naples utaona pikipiki na scooters karibu kila mtaa.
 
Wapewe elimu ya kutosha
Tu

Ova
 
Dah experience hii naitamani sana. Kuna muda mtu unatamani uende ukakae nje ya jiji utafute amani, ila majukumu ndio yanabana. Hapa Dar sahivi kutembea ni kero kuliko mkoa wowote Tanzania.
 
Wabongo mnachekesha sana. Chaos mnaita vibe. Vurugu za bodaboda,bajaj,madaladala unaita vibe? Mtembea kwa miguu kazi yako ni kukwepa bodaboda na magari yamayopita njia za watembea kwa miguu hio ndio vibe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ