Mliowahi kuishi Ulaya: How does it feel kutembea Mjini bila kero za Bajaji, Bodaboda na Machinga?

Mliowahi kuishi Ulaya: How does it feel kutembea Mjini bila kero za Bajaji, Bodaboda na Machinga?

Waulize watu wanaoenda China kwenye miji ya watu milioni 20 kama Guangzhou kama huwa wanakutana na ujinga uliopo Tanzania wa boda, Bajaji na gari zisizo na mpangilio na kelele kila mahali za vispika uchawara vya biashara kila kona.
Kuhusu bajaji, bodaboda, toyo na guta tumekosea kuruhusu vingie mjini.
Na kelele za wauza sumu za wadudua na wakusanya taka vyote siwezi kutetea.
Hata ule uchafu wa mbao za machinga siwezi kuwaunga mkono.
Lakini naunga mkono jiji lenye harakati nyingi za kiuchumi
 
Dah experience hii naitamani sana. Kuna muda mtu unatamani uende ukakae nje ya jiji utafute amani, ila majukumu ndio yanabana. Hapa Dar sahivi kutembea ni kero kuliko mkoa wowote Tanzania.
Ukiwa vizuri kiuchumi
Una mzunguko wa kuingiza
Pesa ahh bora ukaishi kijijini
Mimi kuna wakati nlitamani
Sana kuishi kilosa kati ya ilonga msalabani au pale rudewa au lutindi,korogwe
Kuna mazingira fulani huwa nayapenda

Ova
 
Yes mji niliosoma unaitwa Aberdeen, una watu chini ya laki tatu! Halafu miundo mbinu ipo vizuri
Sasa mji kama huo hata ukisubiri taa zikuongoze una uhakika kuwahi.
Fikiria kutoka Mbozi road uwahi wateja kariakoo njiani kuna maroli yanashusha makontena kwenye bandari kavu zilizojengwa holela.
Kwakweli tutakimbizana tu.
 
Kwa sababu, kwa Tanzania sio Majiji Makubwa wala Miji Midogo, iyo privilege tushaisahau na wengine hawatakaa wakaipata kamwe.

How does it feel kutembea sehemu kama hii?


Bajaji, bodaboda na machinga ni sehemu ya Tanzanian local economies, lakini Ulaya sivyo.

Usidhani serikali za Ulaya zilitunga sheria ya kuzuia bajaji, bodaboda na machinga kuwepo mijini. They just do not exist!
 
Hizi bajaji na boda ni kama zimetulemaza hivi, naona hapa wenzetu wanatembea tu, sisi nusu kilometer unataka kupanda bajaji, lipo la kujifunza kupitia wenzetu.
Ukipanda daladala za sinza ndio utashangaa.

Unaona pisi inapanda kituo hiki inaenda kushuka kituo kinachofuata.

Mtu unabaki kushangaa unatamani umwambie, kuliko kupanda daladala si bora hiyo hela ya nauli angekupa kisha umbebe mgongoni.
 
Bajaji, bodaboda na machinga ni sehemu ya Tanzanian local economies, lakini Ulaya sivyo.

Usidhani serikali za Ulaya zilitunga sheria ya kuzuia bajaji, bodaboda na machinga kuwepo mijini. They just do not exist!
Tatizo kubwa zaidi sio hata uwepo wake bali utaratibu. Wamachinga wawepo ila wasifanye biashara barabarani sehemu za watu kupita, wasiweke vispika vyao vya kelele na pia wasisumbue wapita njia. Boda ndio wendawazimu kabisa, yani wanapita popote bila utaratibu, wanagonga watu, wanagongwa na wanasababisha ajali nyingi sana za hovyo hovyo.
 
Ijapokuwa sijawahi kufika ulaya lakini kwa watu wenye kupenda utulivu wa akili na nafsi hakika ina feel better, lakini kwa kuwa nchi zetu ni maskini na serikali zake dhalimu zenye kujali matumbo yao na maslahi yao, bajaji, boda na machinga zimesaidia pakubwa Watu kutafuta kipato chao halali na kupunguza wimbi la wezi kwa kiasi fulani
Aliyebuni usafiri wa bajaji ña pikipiki anastahili tuzo ya Nobel
Kaepusha mengi sana
 
Kuhusu bajaji, bodaboda, toyo na guta tumekosea kuruhusu vingie mjini.
Na kelele za wauza sumu za wadudua na wakusanya taka vyote siwezi kutetea.
Hata ule uchafu wa mbao za machinga siwezi kuwaunga mkono.
Lakini naunga mkono jiji lenye harakati nyingi za kiuchumi
Boda na Bajaji vinaingia mjini kwa sababu hatuna usafiri mwingine wa kueleweka wa umma, vinginevyo wangekuwa wa kufanya delivery na kubeba mizigo tu ila sio abiria.
 
Nilikua masomoni Scotland wazungu ni wastaarabu sana, imagine kwenye mataa ikiwa nyekundu anasimama kusubiria japokua pande zote hakuna magari!

Cha ajabu sisi weusi tukiona hakuna magari tunapita!
Hii ya kupitia kwenye taa nyekundu bila kusubiria kwa kuamini I hakuna gari..almanusura iondoke na Roho yangu +4 tulikuwa kwenye Toyota harrier... Mjinga yule sijui alikuwa anajiamini nini...=pona pona yetu ilibidi akaivae scania kwa nyuma iliyokuwa imesimama kuliko kukutana head to head na gari iliyokuwa mbele yetu😑😑😑.. kutokuwa wastaarabu na mazoea kunafanya waafrika tunakufa kizembe kila siku
 
Mke wangu amegoma kuhamia nyumba ya mtaa wa Kishua, amesema yeye hayo maisha hakuishi kama Mchawi hayampi furaha.

Na Mimi nampa anavyotaka Sina Makuu, nyumba napangisha tu
Mkuu, labda kama hamna watoto… Kama mnao for the sake of their behavior hameni…

Mkeo akikosa mihogo ya mtaani atajifunza kupika pancake asubuhi au kufreez mihogo…
 
Mkuu, labda kama hamna watoto… Kama mnao for the sake of their behavior hameni…

Mkeo akikosa mihogo ya mtaani atajifunza kupika pancake asubuhi au kufreez mihogo…
Huyo atakuwa anatania tu, mbona kuna mke Manara alisema alimtoa Mbagala uswazi lakini akakubali kuishi ushuani sijui mikocheni au Oysterbay huko anapoishi.
 
1780148409186.jpeg
 
Back
Top Bottom