Mliowahi kuishi Ulaya: How does it feel kutembea Mjini bila kero za Bajaji, Bodaboda na Machinga?

Mliowahi kuishi Ulaya: How does it feel kutembea Mjini bila kero za Bajaji, Bodaboda na Machinga?

Hizi bajaji na boda ni kama zimetulemaza hivi, naona hapa wenzetu wanatembea tu, sisi nusu kilometer unataka kupanda bajaji, lipo la kujifunza kupitia wenzetu.
Kabla hujafika ulaya au amerika inabidi ujifunze kutembea na kukimbia huko afrika, maana kuna kuwahi bus kwenda job au kuwahi bus kurudi home, ukichelewa hata dk moja linakuacha...so we ni mwendo wa mbio na kutembea kimwendo kufata hizo bus au subway
 
Ukifika Japan utaelewa maana ya utulivu ni kitu gani, Kwa sehemu kubwa unapita mitaa Hadi unaogopa, ni ziiiiiiiiii, hata nzi humsikii, unasikia kelele za ndege Tu, halafu mitaa iko misafiii, Kila kitu kimepangiliwa. Japan vitoto vidogo kabisa vinakwenda shule peke Yao, watu wanafuata Sheria Hadi kwenye barabara nyeupe isiyo na magari....Kila mmoja anaishi dunia Yake, kinyume chake fika India sasa hasa Kwa wale wenzangu na Mimi, TZ si mnasema kuna msongamano, India ni komesha ni kelele zaidi ya Bar, mambo yako hovyo hovyo zaidi ya bongo hakuna miongozo wala cha Sheria sijui za mazingira na kazi, its hell...but ni watu wa kazi, Sijawahi kuona watu wanaopiga kazi kama wale Jamaa hasa hizi manual, hakuna huruma, ndio maana mhindi akija bongo anaona ni peponi na lazima ataku outsmart because they came from very competitive environments...
Sio wahindi wote wapiga kazi...kuna limoja hapa tuko nalo ofisini vivu vivu mpaka mzungu anataka alitimue
 
Kabla hujafika ulaya au amerika inabidi ujifunze kutembea na kukimbia huko afrika, maana kuna kuwahi bus kwenda job au kuwahi bus kurudi home, ukichelewa hata dk moja linakuacha...so we ni mwendo wa mbio na kutembea kimwendo kufata hizo bus au subway
Nimeipenda hii, kwetu bado
 
Ukipanda daladala za sinza ndio utashangaa.

Unaona pisi inapanda kituo hiki inaenda kushuka kituo kinachofuata.

Mtu unabaki kushangaa unatamani umwambie, kuliko kupanda daladala si bora hiyo hela ya nauli angekupa kisha umbebe mgongoni.
Hatari sana, ndio maana miili imekuwa ya ajabu ajabu kwa sababu ya uzembe
 
Ndiyo maana magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanatushambulia mno.
Watu wetu ni malimbukeni sana wa vyombo vya moto.
Utakuta mtu anatoka Magomeni mapipa anaenda mwembechai anataka apande kipando
Kabisa tunaendekeza usasa mwingi alafu magonjwa ya ajabu ajabu yanatupata
 
Back
Top Bottom