Mmiliki wa Shule za Tusiime jitafakari na uwalipe wafanyakazi stahiki zao

Hivi baada ya corona kwisha wazazi watalipa full school fees wakati kuna siku kede kede watoto hawapo shuleni na hawafundishwi au kutumia resources za shule?
 
ujumbe wako utawafikia
Mkuu nitashukuru kama kuna uwezekano ujumbe huu ukawafikia nilio wanukuu serikalini.
Kama kuna ufafanuzi kidogo wa sehemu fulani katika mchango wangu naweza kutoa ushirikiano kwenye Private messages (PM) na siyo lazima nijitambulishe jina na mengineyo.

NB: Mimi siyo mwalimu au mmiliki wa shule, I'm just an average Joe in street, sina maslahi yoyote katika hili labda kwa vile mimi ni mzazi tu wa wanafunzi wa kati ya hizi shule.
 
duh samahani Ila nimejikuta nahisikia Tu kukwambia TAFUTA ZAKO HALAFU UFANYE HIVYO UNAVYO SHAURI
 
Wewe ndo umeongea mambo ya msingi. Kuna watu hawajawahi kusimamia hata vibarua wanaleta hoja za kufikirika ambazo haziwezekani.
 
Mtu anayefanya biashara kubwa vile huwezi nambia hana akili nikakubali.
Hii ni misingi ya biashara yake na ndo maana kafika hapa. Angekuwa hana akili ndo naye angekuwa analialia kulipwa salary au biashara ingeshakufa.
Ni kawaida ya matajiri kuwa critisized lakini kwa hili siwezi mlaumu kwa vile sina hakika hali yake kifedha ikoje.

NB: Serikali imetembeza bakuli.
 
Huu ushauri Bora kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kwenye hili bunge stimulus budget haijadiliwi kusaidia watu, biashara na makampuni dhidi ya kufilisika...
 
Pole sana mwalimu.
Mlichagua wawakilishi 50 tangu tarehe 17 April wawawakilishe, hapo ulikaa kinya kusikilizia jibu, wala hukuona madhaifu ya uwakilishi na mapungugu mengine.

Endapo ingekubalika muendelee kupata malipo bila shaka usingekuja humu kulalamikia madhaifu ya mchakato, ila kwa sababu matarajio yako ya kupata salari yameyeyuka ndio unatia mchakato wa vikao mapungufu.

Hayo mambo ya Holding sijui kuchunguzwa matumizi mabaya ya pesa umeyajfahamu wiki hii? Miaka yote ulikuwa wapi?

Inauma kukatushwa mshahara kama wafanyakazi hasa kipindi kama hiki lakini na wewe mtoa mada umejaa majungu, uzandiki na uchawi dhidi ya mwajiri wako.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Worry not,count it done
 
Kwann waajiriwa hawakutunza akiba ili inapotokea janga kama hili waweze kujikimu walau miezi 3 bila kuwa na stress au kugombana na mwajiri.
 
Wazazi hawajalipa ada unataka mmiliki atoe wapi pesa za kuwalipa mishahara? Halafu huwezi kulipa watu ambao hawazalishi kwa sasa. Hii ni biashara siyo non profit organization.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…