Mnaofurahia Mikopo, Sri Lanka pia iIianza kama sisi

Bora hata tunawekwa wazi kuhusu hii mikopo, kuliko ile tuliyokuwa tunadanganywa Tanzania ni nchi tajiri wakati wanakopa kimya kimya.
Walikopa kimya kimya ila wakaweka wazi matumizi na miradi husika tena ya kimkakati.
Sasa wanakopa kwa sauti na kutumia kwa Ukimya.

Ebu nitolee ufafanuzi wa mapato na matumizi yatokanayo na Tozo za miamala inayoendelea?

Ni mradi gani wa kimkakati ambao umetokana na mikopo lukuki inayoendelea kumiminika kwa sasa?
 
Tofautisha mkopo wako wa kibinafsi na familia yako na huu tunaouongelea sisi ambao sio wa kulipwa na viongozi bali watanzania wote.

Hebu tueleze nini hasa kimefanyika tangu hii mikopo imeanza kukopwa na sifa zikiendelea bila ukomo?
 
hiziz tozo angeziweka mzee magu daah angefanya makubwa
Huo ndio ukweli halisi.mfano tulikuwa tukiona fedha za kuahirishwa sherehe zilivyokuwa zikitumika kwa miradi mbadala na inaonekana.
 
Huwezi kumuelewa mama kama IQ yako ndogo.

Ajira mpya
Nyongeza ya mishahara iliyoshindikana kwa miaka 6
Kupandisha vyeo watumishi
Na hiyo miradi yenu ya Kimkakati, (mfano SGR lot 4,5,6 msiseme ni za awamu ya tano) zinaendelea kama kawaida bila kusahau muendelezo na ukamilishaji wa lot 1,2
Ndege mpya 5,
Ujenzi wa madarasa 15,000 nchi nzima (Hapa hujui ni ajira ngapi zimetengenezwa zikiwemo za wadogo zako???)
Miradi ya usambazaji maji vijijini
Ujenzi wa na uboreshaji wa barabara za vijijini.
Ukamilishaji wa vituo vya afya (Staffing (ajira)/ Madawa/ Vifaa tiba)
Bunge live (mlilosema ni gharama kwa serikali)
Uboreshaji wa sheria za vyombo vya habari
 
Je!
Mbona hatuelezi zinazopotea kwa ufisadi?
Hausemi zinazopotea kwenye matumizi yasiyo na tija kama.

Posho za Warsha.
Posho za zsemina.
Posho za makongamano.
Posho za safari za nje kila uchao.

Gharama za kuendeshea ma V8 yote nchi nzima.
Mfano Meya wa jiji anatumia Land Cruisser V8 4Γ—4.
Ilhali yuko kwenye lami kila siku na angeweza kutumia hata Suzuki Escudo tu.
 
Huo ndio ukweli halisi.mfano tulikuwa tukiona fedha za kuahirishwa sherehe zilivyokuwa zikitumika kwa miradi mbadala na inaonekana.
yani balaaa sema ndo hivyoo now nchi anaendesha kj aisee
 
Kutokuwa na taarifa ni tatizo,
Posho zimeanza awamu ya sita?
Safari za nje??? fuatilia umuhimu na matokeo ya safari anazofanya SSH ndio uje hapa tuzungumze.
V8 zimeanza awamu ya sita??? Pitia hotuba ya bajeti 2022/23 kuna majibu.
Mameya wameanza kutumia V8 baada ya Mwendazake???

Awamu iliyopita mlikuwa mnaedit mpaka report ya CAG kuficha ufisadi baada ya kumuondoa Prof Assad kinyume na katiba.

What is life without haters??????
 
Hao unaowapa vitasa huwa wanatumia kufungia milango au mafuvu ya ubongo wao.

Unasapoti mikopo halafu unajipinga wewe mwenyewe.

Hapa tunaongelea Facts za matumizi zinakoelekezwa hizo pesa baada ya mkopo kupatikana.
Hatuongelei nchi kutokukopa.

Lakini pia tunaangalia ni jinsi gani uongozi uliopo unatumia vipaumbele gani kutokana na Raslimali lukuki tulizonazo nchi hii.

Tatizo ni kuwa na serikali iliyojaa michwa huku ikiwa haina ubunifu wa kiuongozi.

Sera ni kusifu na kuteuliwa kisha kutukuza.
 
Hawa wenzetu huwa hawajui adui yao rasmi ni nani!
Hawajui kwamba unapokuwa na deni kubwa kama taifa, ni lazima wananchi wakamuliwe kwa namna yoyote ile mpaka deni litimie kulipwa kila mwezi.

Na hapo ndio digit zinapopanda na kuleta kilio mtaani.
 
Tofautisha mkopo wako wa kibinafsi na familia yako na huu tunaouongelea sisi ambao sio wa kulipwa na viongozi bali watanzania wote.

Hebu tueleze nini hasa kimefanyika tangu hii mikopo imeanza kukopwa na sifa zikiendelea bila ukomo?
Sina mda wa kujichosha kuelimisha mtu ambae ameamua kuwa mpumbavu..

Tafuta sources rasmi za serikali utaona kilichofanyika..

Kuna mada kibao humu zinaeleza hata Leo RUWASA walikuwa live kueleza kilichofanyika so ni wajibu wako kutafuta sio wajibu wangu..

Ulivyo mpumbavu huwa Rais anawaambia kila siku kwamba miradi yote mikubwa ni mikopo huelewi sasa kama wewe unaona hakuna kilichofanyika ila ukiamka asubuh unasafiri kwenye barabara,unatumia maji na unaenda hospital harafu unauliza zinakotumika ni wazi wewe ni mpumbavu.
 
Wewe ni mjinga sasa ka.hata hujui vipaombele vya Serikali na budget read out zipo una maana gani? Why bother kumjibu mpumbavu?
 
Taarifa nyingine anazipata kwa kubishana humu humu jamii forum. Hana kitu kichwani
 
Wengi humu wanaobisha kuhusu huu ukweli unakuta ni walamba asali kwa sasa.
Au waajiriwa sekta ya Umma ambao wanazisubiri ziingie kwenye anga zao ili waendelee kuzinyofoa kwa urefu wa kamba zao.
 
Kuna miradi gani ya siri unayoijua wewe peke yako pamoja na serikali tu?

Tuambie mradi hata mmoja ambao kauanzisha mama yenu, ambao ni wenye tija kwa taifa.
Tangu katiba ilipompa madaraka?
 
Wengi humu wanaobisha kuhusu huu ukweli unakuta ni walamba asali kwa sasa.
Au waajiriwa sekta ya Umma ambao wanazisubiri ziingie kwenye anga zao ili waendelee kuzinyofoa kwa urefu wa kamba zao.
Sijawahi kuipenda CCM, ila kwenye ukweli nitasema. SSH amepokea nchi ikiwa kwenye mzigo mzito wa miradi mikubwa na mapato kidogo, miaka 6 hakuna nyongeza ya mishahara, ajira mpya, watumishi kupandishwa vyeo vitu ambavyo mwendazake hakuviweza.
 
Imagine vitu vidogo kama hivi huelewi eti na wewe ndio msomi huko Chadomo πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†..

Kwamba hujui kwamba Serikali imejenga zaidi ya vituo vya afya 334 Nchi nzima kwa tozo za miamala au?

Sasa mtu kama.wewe una maana gani?
 
Lini mshawai fanyiwa mazur na mkakili kuwa ni kweli lini?
Kipindi cha JPM tuliona matumizi sahihi ya raslimali za nchi hii pamoja na kuzuia michwa kula mbao za maghala ya Taifa.
Sasa walipoona kawabana na wanaelekea kupotea kwenye ramani ndio wakatuondolea mtu wa ukweli.
 
Kuna miradi gani ya siri unayoijua wewe peke yako pamoja na serikali tu?

Tuambie mradi hata mmoja ambao kauanzisha mama yenu, ambao ni wenye tija kwa taifa.
Tangu katiba ilipompa madaraka?
SGR Lot 3,4,5, Magu aliacha Lot 1,2
Ujenzi wa JNHPP Magu aliacha 22% na SSH anakamilisha 78%
Ndege mpya 5
Ununuzi wa locomotive 3 series 10 kwa reli ya MGR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…